Kijana mmoja ameshambuliwa na kundi la wazee alipokaidi kumwachia kiti mmoja wao ndani ya basi nchini China.
Katika mabasi yanayoelekea eneo la Wuhan, viti vyake vya njano vina maana maalum, kutokana na kwamba viti hivyo vimetengewa wazee, anawake wajawazito ama wagonjwa.
Hata hivyo heshima hiyo imekuwa ikivunjwa ama kukiukwa hasa na vijana.
Lakini kijana mmoja aliyeamua kukaa katika moja ya viti hivyo visivyomuhusu, alionja joto la jiwe baada ya kupewa kipigo na wazee wenye haki ya kukaa katika siti hizo.
Mzee mmoja aliyekaa na kijana huyo alimtaka asimame na kuachia nafasi hiyo ili ampishe mzee aliyekuwa amesimama, lakini kijana huyo alikaidi na ndipo mtafaruku ukaanza kwa kushambuliwa na wazee waliokuwamo katika basi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni