Jumatano, 1 Oktoba 2014
WANAJESHI WA ISRAEL WAJIUA
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeanza uchunguzi kuhusiana na vifo vya wanajeshi watatu wa utawala huo walioamua kujiua baada ya kurejea kwenye vita kati ya utawala huo na Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Ghaza.
Polisi ya Jeshi la utawala wa Israel imetangaza kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa wanajeshi hao walijiua kutokana na matatizo ya kisaikolojia yaliyosababishwa na ushiriki wao kwenye vita vya Ghaza.
Taarifa zinasema kuwa, wanajeshi hao wa Israel waliamua kujiua kwa kujifyatulia risasi na kwamba silaha walizotumia zilipatikana zikiwa pembezoni mwa miili yao. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanajeshi wawili kati ya watatu walijiua kwenye kambi ya kijeshi iliyoko karibu na mpaka wa Ukanda wa Ghaza.
Nalo gazeti la Maariv linalochapishwa huko Israel limemnukuu mmoja kati ya maafisa wa ngazi za juu wa utawala wa Israel katika hospitali ya wagonjwa wa akili akisema kuwa, jumla ya wanajeshi wanane wa Israel walijiua mwaka jana.
Afisa huyo mwandamizi wa jeshi amesema kuwa, jeshi la Israel halitangazi takwimu za wanajeshi wake wanaojiua kutokana na matatizo ya kiakili jambo ambalo wachunguzi wa mambo wanadhani ni kuogopa lisipunguze morali wa vijana kujiunga na jeshi hilo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni