Jeshi
la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi
wa Dumila na Mbigiri wilayani Kilosa mkoani Morogoro baada ya kufunga
barabara ya Morogoro Dodoma kwa kutumia mawe na kuchoma matairi
barabarani katika eneo la dumila na kusababisha abiria wanaotumia
barabara ya Morogoro -Dodoma kukosa mawasiliano kwa zaidi ya masaa sita.
Waandishi
wa Malunde1 blog wameshuhudia wananchi hao wakifunga barabara kwa mawe
na matairi huku wengine wakionekana na mapanga ambapo wamesema
wanalalamikia viongozi wa serikali ya kuanzia ngazi ya kijiji hadi
wilaya kufumbia macho mgogoro wa ardhi na kushindwa kuwachukulia hatua
wafugaji wanaowazuia wakulima wasilime katika eneo la Mbigiri.
Vurugu
hizo zilidumu kwa muda mrefu na juhudi za kudhibiti wakulima hao
zimechukua muda baada ya askari wachache wa kituo cha Dumila kuonekana
kuzidiwa nguvu ambapo baadhi ya wakulima wengine wameonekana wakivamia
wakuvunja nyumba za wageni zinazomilikiwa na wafugaji na kupora magodoro
na vitu mbalimbali ambapo baadae vikosi vya jeshi la polisi
viliongezwa na kufanikiwa kudhibiti baadhi ya watuhumiwa na kufungua
barabara.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema chanzo cha vurugu hizo
ni wazee zaidi ya kumi walizuiwa kulima katika mashamba yao mbigiri
ambapo walipelekeka malalamiko yao kwa afisa tarafa ambapo wakiwa
ofisini kundi la vijana walifika na kufunga ofisi wazee hao pamoja na
afisa tarafa hadi walipofika na koOkolewa na jeshi la polisi na katika
tukio hilo watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Afisa
tarafa na wazee walifungiwa ndani wakizungumzia tukio hilo wamesema
kuna mgogoro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji na upo katika
ngazi za juu huku wakieleza kusikitishwa na hatua za kufunga barabara na
kuomba serikali kuingilia kati kutatua mgogoro wa ardhi uliopo.
Hata hivyo katika hatua nyingine Tunaambiwa Chanzo cha vurugu hizo
kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishie Kijiji cha
Mketeni wilayani Kilosa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la
Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.
Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata
wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi
ya wafugaji wa eneo hilo.
Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia,
wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma
ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma
matairi.
Kufuatia hali hiyo polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao
pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni
zinazomilikiwa na wafugaji eneo hilo na kufanya uharibifu.
Majeruhi katika vurugu hizo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni