BEI YA PETROLI YAZIDI KUSHUKA
Bei ya mafuta
Bei ya mafuta yasiyosafishwa imeripotiwa kushuka zaidi.
Hii ni habari njema kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.
Siku ya ijumaa mafuta yalikuwa yakiuzwa kwa chini ya dola 49 kwa pipa.
Bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa kwa sasa yameshuka zaidi ya nusu tangu mwezi Juni.
Mwandishi
wa masuala ya kiuchumi wa BBC anasema kuwa uzalishaji mkubwa wa mafuta
nchini Marekani na hatua ya nchi za muungano wa kuzalisha mafuta OPEC
kutotaka kupunguza uzalishaji wa mafuta vimechangia kushuka zaidi kwa
bei hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni