Jumamosi, 10 Januari 2015

MSICHANA WA MIAKA KUMI AJILIPUA NA KUUA 15



Mlipuaji wa kujitolea muhanga ajilipua katika soko moja Nigeria 
 
Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua katika soko moja katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo ni msichana wa miaka kumi.
Duru kutoka hospitali zimeambia BBC kwamba takriban watu 15 wameuawa katika shambulizi hilo.
Hakuna mtu aliyekiri kutekeleza shambulizi hilo kufikia sasa.
Hata hivyo watu wanalishuku kundi la Boko Haram kutokana na misururu yake ya mashambulizi katika mji huo na maeneo mengine ya Nigeria Kaskazini.
Takriban watu elfu ishirini wamelazimika kutoroka na inahofiwa kuwa mamia waliuawa wakati Boko Haram lilipochukua udhibiti wa mji wa Baga na viunga vyake wiki iliyopita (TUKUO)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni