kwa kuchangia pakubwa ghasia zilizozuka baada ya Bwana Gbagbo kukataa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanywa Desemba 2010.
Kulingana na mashtaka yanayomkabili mke wa Gbagbo na washtakiwa wenzake, walitumia wapiganaji wa kiraia katili kuwashambulia wafuasi wa mshindi wa Uchaguzi huo, Rais Alassane Ouattara, ingawa wafuasi wake pia wanadaiwa kutekeleza ukatili ambao kwa ujumla ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.
Gbagbo na mkewe walitiwa mbaroni Aprili 2011, ambapo Simone, alizuiwa katika jela moja Kaskazini mwa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika lakini mumewe akapelekwa katika mahakama ya ICC iliyoko The Hague.
Mahakama ya Ivory Coast imekataa katakata wito uliotolewa na makundi mengine kuwa Simone Bgagbo apelekwe The Hague, ambako mumewe anashtakiwa, yakidai kuwa mwanamke huyo na washtakiwa wenzake wanapaswa kukabiliana na makali ya sheria nyumbani.
Hadi kufikia leo alasiri Bi Gbagbo, mwenye umri wa miaka 65, hakuwa amefikishwa mahakamani.
Kwa zaidi ya mwezi mmoja, wanasiasa, waandishi wa habari na wafuasi kadhaa wa Gbagbo
wamehojiwa mahakamani walipokuwa wakitoa ushahidi dhidi ya washtakiwa hao wanaoandamana na Bi Gbagbo.
Washtakiwa pamoja na wanasiasa kutoka upinzani wanadai kuwa mahakama itapendelea walioshinda
katika uchaguzi kwa sababu wanayo mamlaka juu ya taasisi zote za kutoa haki nchini.
Hakuna mtu yeyote aliye na uhusiano wa karibu na Ouattara aliyefanyiwa uchunguzi au kushtakiwa kuhusiana na ghasia hizo zilizokumba mji mkuu wa taifa kwa zaidi ya miezi mitano ingawa wengi wanafahamu kuwa upande wake pia ulichangia pakubwa ghasia zilizokumba taifa hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni