Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel
Adebayor ameandika maelezo marefu kwenye akaunti yake ya Facebook
kuelezea visa anavyofanyiwa na familia yake wakiwemo mama, kaka na dada
zake. Adebayor anawashutumu ndugu zake kwa tamaa ya mali zake. Licha ya
kuwafanyia mambo mengi ikiwemo kuwajenga nyumba, kuwanunulia magari na
kuwapa mitaji ya biashara, wameendelea kumtupia shutuma nyingi.
Tumeitafsiri post hiyo kwaajili yako. Sehemu ya maelezo hayo marefu
inasema: SEA,
nimezihifadhi habari hizi kwa muda mrefu
lakini nadhani leo ni muhimu kuziweka wazi baadhi yake kwenu. Ni kweli
masuala ya kifamilia yanapaswa kusuluhishwa ndani kwa ndani na sio
hadharani lakini nafanya hivi ili pengine familia zote zinaweza
kujifunza kutokana na kile kilichotokea kwangu. Pia weka akilini kuwa
hakuna chochote kati ya haya kinahusiana na pesa. Nikiwa na miaka 17,
kwa mishahara yangu kama mcheza soka, nilijenga nyumba kwaajili ya
familia yangu na kuhakikisha kuwa wapo salama. Kama nyote mnavyojua,
nilishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008. Nilimpandisha pia
mama yangu jukwaani kumshukuru kwa kila kitu. Katika mwaka huo huo,
nilimleta London kwaajili ya kufanyiwa vipimo mbalimbali. Baada ya mtoto
wangu wa kike kuzaliwa, tuliwasiliana na mama yangu kumjulisha lakini
muda mfupi alikataa simu na hakutaka kujua chochote. Nikisoma maoni yenu
ya hivi karibuni, baadhi ya watu walisema mimi na familia yangu
tungemtafuta T.B Joshua. Mwaka 2013, nilimpa mama yangu fedha ili
amtafute (Joshua) nchini Nigeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni