Jumatano, 13 Mei 2015

HAMAD RASHID ATANGAZA RASMI KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

 
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed
Mbunge wa Wawi kupitia chama cha wananchi, CUF ameamua kutogombea tena ubunge na kuwaaga rasmi wabunge wenzake baada ya kutumikia tangu 1977 na sasa ameamua kugombea urais kupitia chama cha ADC Zanzibar.
Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed aliyasema hayo wakati akitoa hoja leo Bungeni Dodoma katika muendelezo wa hoja za Bunge la Bajeti lililoanza Mei 11 mwaka huu.
Itakumbukwa mbunge alikuwa na mgogoro na chama chake cha sasa na kupelekea kufukuzwa uanachama hatua ambayo aliipinga mahakamani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni