Serikali
ya Libya inayotambuliwa kimataifa imesema mashambulio ya Marekani ya
anga nchini Libya, yamemuua mpiganaji mwandamizi wa Kiislam, Mokhtar
Belmokhtar.
Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa
Belmokhtar alikuwa mlengwa wa mashambulio hayo ya Jumamosi, lakini
imesema bado inafanya tathmini ya matokeo ya operesheni hiyo.Mokhtar Belmokhtar mzaliwa wa Algeria anaaminika kuamuru kufanyika kwa shambulio baya katika mtambo wa gesi nchini Algeria miaka miwili iliyopita ambapo wafanyakazi 38 wa mtambo huo waliuawa-- wengi wao wakiwa wageni.
Kifo cha Belmokhtar kimekuwa kikiripotiwa mara nyingi katika siku zilizopita, lakini baadaye kubainika kuwa si habari za kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni