Katika karibu kila
jambo duniani, mwanadamu huhitajika kutumia akili ili kufanikiwa. Bila
shaka, iwapo utatarajia uwazidi watu wengine hasa katika kuwapora au
kuwaibia basi utahitajika kuwa na ujanja zaidi. Lakini maeneo mbalimbali
duniani kunao wahalifu ambao walionekana kupungukiwa.
Majuzi kwa
mfano, wanaume wawili kutoka Skegness, Lincolnshire, walijipiga picha
wakiiba pesa kutoka kwenye mitambo ya kucheza Kamari Bradford,
Uingereza. Hawakuenda mbali, kwani walikamatwa muda mfupi baadaye
Benjamin Robinson, 30, alifungwa jela miezi 32, naye Daniel Hutchinson
akahukumiwa kifungo cha miezi sita jela ambacho kimeahirishwa.
Hawako peke yao. Hapa ni msururu wa wahalifu wengine waliojichongea:
1. Jambazi aliyejitapa Facebook
Andrew
Hennells alikamatwa baada yake kuandika kwenye Facebook akijisifu
kuhusu mpango wake wa kushambulia duka la jumla la Tesco eneo la King's
Lynn, Norfolk.