Jumanne, 28 Juni 2016

URENO YATWAA KOMBE LA EURO 2016 SHEREHE ZAENDELEA

 
Hii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji  hilo. 
 
Kundi kubwa la mashabiki wa Ureno limeendelea kusheherekea bada ya timu yao ya taifa kuifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2016 mjini Paris.
Ureno imeshinda 1-0 katika muda wa nyongeza na kuwaacha mashabiki wa Ufaransa katika hali ya simanzi ndani ya dimba la Stade de France huku mitaa ya Lisbon ikirindima kwa shangwe kubwa.

Ureno illicheka karibia mda wote bila huduma ya nyota wake Cristiano Ronaldo aliyeumia na kutolewa nje dakika 25 ya mchezo huo na baadaye kurejea na kulinyanyua kombe hilo.
Ronaldo amesema kombe hilo ni kwa ajili ya Wareno wote pamoja na wote wanaioshabikia timu hiyo mjini Paris.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.

GESI LA HELIUM YAGUNDULIWA TANZANIA

 
 Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania
Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.

Jumanne, 21 Juni 2016

TANZANIA YATENGENEZA CHOPA YAKE

Ndege aina ya helikopta
Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linatengeza ndege .Gazeti la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi .
Gazeti la Zambia,Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.
Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily New

GHASIA MBAYA ZATOKEA AFRIKA YA KUSINI



Vizuizi vya polisi vikiwaka moto mjini Pretoria.
Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzuia ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu na inasema kuwa maafisa wa polisi walifyatuwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao kwa mawe.
Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.
Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
Serikali ya Afrika Kusini imeomba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo

MJI WA DODOMA WAKUMBWA NA GONJWA LA AJABU




Hofu na wasi wasi umezidi kutanda huko mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania baada ya kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana.

Hadi sasa jumla ya watu saba wamefariki na wengine 21 kulazwa katika hospital ya mkoa mjini Dodoma baada ya kuzuka ugongwa huo ambao hadi sasa madaktari hawaujui wala tiba yake haijajulikana.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kutapika, kuharisha, ngozi na macho kuwa ya njano pamoja na kuumwa na tumbo.

Kufuatia kuibuka kwa ugonjwa huo tayari kumetengwa wodi maalum katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Dodoma katikati mwa Tanzania ambapo pia karantini imewekwa na hakuna anayeruhusiwa kukaribia mahali hapo zaidi ya madaktari ambao nao pia wanaingia kwenye wodi kuwaona wagonjwa kwa tahadhari kubwa. CHANZO BBC

Jumatatu, 20 Juni 2016

KUNGUNI WAPANDA MATATU BURE NAIROBI

Magari mengi ya usafiri jijini Nairobi, Kenya, maarufu kama "matatu" yana kunguni, kwa mujibu wa gazeti la standard la nchi hiyo.
Kondakta mmoja anaripotiwa kuliambia gazeti la Standard, kuwa wadudu hao wanatishia kuharibu biashara ya kutoka na sababu kuwa watu wengi kuhofia kupanda "Matatu" kwa sababu watang'atwa na wadudu hao lakini wanaweza kuwapeleka majumbani kwao.

kunguni akiwa  ameshiba
Wadudu hao husambazwa na wateja kutoka kwa nyumba zao bila kujua, ambao kisha hubaki kwenye viti vya magari.
Sasa wahudumu wa sekta ya usafiri jijini Nairobi, wameanzisha kampeni ya kuangamiza kungunu hao kwa kunyunyiza dawa na pia kuwataka abiria kutoa habari ikiwa wataona wadudu hao.

Jumamosi, 18 Juni 2016

ITALIA YAINGIA 16 BORA FAINALI EURO

Sweden  

 Italia walifunga bao dakika ya 88
Timu ya taifa ya Italia imefika hatua ya muondoano katika michuano ya ubingwa wa Ulaya baada ya kujipatia ushindi dhidi ya Sweden.
Ushindi wa Italia ulitokana na bao la pekee la mechi hiyo, lililofungwa na Eder dakika za mwishomwisho.
Ishara zilionesha kana kwamba mechi hiyo ingemalizika sare tasa hadi pale Eder alipokimbia na kufikia mpira kutoka kwa Simone Zaza nje kidogo ya eneo la hatari dakika ya 88.
Sweden hawakupata kombora hata moja la kulenga goli kwa mechi ya pili mfululizo.


 
Mshambuliaji nyota Zlatan Ibrahimovic alinyamazishwa mechi yote.
Italy wanaongoza Kundi E na alama sita. Sweden wamo nambari tatu na alama moja.

MWALIMU JELA MIAKA 90 KWA KUNAJISI WATOTO

 

Mwalimu afungwa miaka 90 kunajisi wanafunzi
Mwalimu mmoja wa shule ya msingi katika eneo la kati nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake.

JK KUENDELEA KUPAA: ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba

KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya (EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya  Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Caribean na Pacific.
Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk.  Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018

Ijumaa, 10 Juni 2016

WATOTO SITA WAFA UBATIZONI ZIMBABWE

 
 Robert Mugabe
Watoto sita wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini Zimbabwe. Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake ni ya baridi; watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.

Polisi nchini Zimbabwe wamewatia mbaroni watu wawili ambao ni wafuasi wa dhehebu moja la Kikristo.

Pia walisema kuwa wamemkamata mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii na ambaye alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake.

Wakili apigwa na kuchaniwa nguo mbele ya majaji China

Wakili wa China aliyepigwa na kuchaniwa nguo akitoka mahakamani
Mawakili wengi wa China wamenyanyaswa, kukamatwa na hata kufungwa jela lakini picha ya mmoja wao aliyekuwa na nguo zake zilizochanwa na maafisa wa polisi imevutia hisia nyingi nchini China.

Wu Liangshu alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Qingxiu akiwa amevalia koti lake na suruali nyeusi akiwa mtanashati kabisa lakini alipotoka alikuwa hana koti na suruali yake kuchanwa hadi nguo ya ndani ikionekana.

Yeye na mawakili wengine waliwaambia maafisa wa mahakama kwamba alishambuliwa na maafisa watatu katika mahakama moja mbele ya majaji wawili ambao walikataa ombi lake la kutaka kuanzisha kesi katika mahakama ya wilaya ya Nanning Mkoani Guangxi.

Bw Wu alipewa nguo nyengine lakini alijua uwezo wa kile alichokuwa akipanga kukifanya.''Asante alisema''.
Wakili huyo baadaye alitembea kupitia mlango wa mbele akiwa amebeba nakala zake za mahakamani akiwa na kalamu iliowekwa katika mfuko wa shati liliposuliwa.

Baadaye alipigwa picha nje ya jengo hilo la mahakama na picha hiyo kusambazwa. Hii ilikuwa na maana ya kutuma ujumbe kewa nchini China mawakili wananyanyaswa. Meseji sent

Ijumaa, 3 Juni 2016

Video yawatia matatani wanafunzi waliofanya mtihani India

 
Bihar wazazi wakipanda kuta kusaidia watoto wao
Wanafunzi 14 walioongoza katika matokeo ya mtihani wa mwisho katika jimbo la Bihar nchini India watalazimika kufanya tena mtihani kufuatia madai kwamba walihusika na udanganyifu, serikali ya jimbo hilo imsema.
Uamuzi huo uliafikiwa baada ya mmoja ya wanafunzi hao Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 kuviambia vyombo vya habari kwamba sayansi ya siasa inahusisha kupika.