Jumatatu, 5 Septemba 2016

POLISI WAKAMATA MAJAMBAZI NA SILAHA


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Der es Salaam limekamata watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi na kukamata silaha na vifaa vya aina mbalimbali zikiwepo bunduki, risasi, redio call, pamoja na sare za askari Polisi katika msako maalum wa kukamata wahalifu.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao walisema wana nyumba wanaishi eneo la Mbezi Chini na kuzikamata silaha hizo kwenye nyumba ambapo pia ilidaiwa kuwa majambazi hao ni raia wa Kenya.
Sirro amezitaja silaha hizo kuwa ni smg tatu, bastola 16, shotgun 3 pamoja na risasi zaidi ya 800.

Mbali na silaha hizo pia Sirro amesema polisi imekamata redio call 12, sare za polisi, Pingu 45 na darubini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni