Polisi nchini India
wanamtafuta Sadhvi Deva Thakur, mwanamke aliyeko mafichoni baada ya
kufyatua risasi kwenye sherehe ya harusi
Shaghaziye bwana harusi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.Kwenye video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katia jimbo la Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur anaonekana akifyatua risasi akitumia bunduki aina ya revolver.
Vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa Sadhvi, ambalo ni jina la kiindi linalomaanisha mwanamke aliye mtakatifu au anayejiita kuwa mungu alingia ukumbni, ambapo alimuomba DJ kucheza wimbo aliotaka na akaanza kucheza densi.
Wakati huo ufyatuaji risasi ulikuwa ukiendelea.
Ni wakati shangaziye bwana Harusi mwenye umri wa miaka 50 alipoangauka baada ya kupigwa rasasi na wengine watatu kujeruhiwa vibaya, ndipo ufyatuaji huo ukasitishwa.
Wakati huo Sadhvi na walinzi wake sita walitoweka. Polisi wamewafungulia kesi ya mauaji na wanajaribu kuwatafuta watu hao saba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni