Baada ya
kutengenishwa na mamake muda mfupi baada ya kuzaliwa, sokwe Manno
alisafirishwa hadi nchini Iraq ambapo aliishi akivuta sigara alizokuwa
akipewa na wageni huku akipigwa picha na wageni waliokuwa wakimtembelea.
Sokwe huyo mwenye umri wa miaka minne pia angevalishwa nguo kama mtoto na kupewa vinywaji na pipiKisha ukakuja msaada kutoka kwa makundi kadha ya kutunza wanyama, na sasa siku za Manno kama mvutaji sigara zimwekwisha baada ya kuwasili katika kituo cha kuwatunza sokwe kilicho nchini Kenya wiki moja iliyopita.
Baada ya siku kadha za safari akiwa amefungiwa kwenye kisanduku kidogo, Manno aliwasili katika kituo cha Ol Pejeta mnamo Novemba 30 ambacho kimekuwa kikiwatunza sokwe walio kwemye hatari wa kuangamia tangu mwaka 1993.
Manno ambaye anaaminiwa kuzaliwa mjini Damascus nchini Syria hajaishi maisha ya kawaida tangu auzwe kinyume cha sheria mwaka 2013 kwa dola 15,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni