Maafisa wa polisi
wanachunguza baada ya kangaroo kupatikana amepigwa risasi huku
akishikilia mvinyo wa pombe mjini Melbourne Australia.
Maafisa wa
wanyama pori nchini Australia wanasema mnyama huyo aliigwa risasi mara
tatu na baadaye kufungwa akiwa ameketi katika kiti.Iliripotiwa mwezi uliopita lakini mamlaka ilitoa picha wiki hii katika harakati za kutafuta habari.
Hukumu ya mauaji ya myama huyo kinyume cha sheria ni faini ya hadi dola 36,500 za Australia na hadi kifungo cha miaka miwili jela.
Idara ya mazingira, ardhi, maji na mipango ilisema kuwa inashirikiana na maafisa wa polisi kutatua uhalifu huo.
Lazima ilichukua muda mrefu kumuweka kangaroo huyo katika hali aliyokuwa kanda kando ya barabara.
Hesabu ya hivi karibuni ya kangaroo nchini Australia ni milioni 34.3
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni