Mwanamume mmoja
amekamatwa kwa madai kuwa alimng'ata na kukata kidole cha mtu mwingine
wakati was sherehe ya harusi mjini Sydney Australia.
Mvamizi huyo mwenye umri wa miaka 42 aliingia katika sherehe moja ya harusi siku ya Jumamosi usiku na kujaribu kuiba mkoba.Wakati wageni walipomkabili, mvutano ukatokea ambapo mwanamume huyo alingata kidole cha mtu mwingine.
Kidole kilichong'atwa hakiwezi kuokolea, kwa mujibu wa vyomo vya habari.
Mwanamume aliyeumia alipelekwa hospitalini ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.
Hizo hazikuwa ghasia za mwisho usiku huo kwani polisi walilazimika kuvunja mapigano yaliyotokea nje ya klabu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni