Mwizi mmoja
amekamatwa baada ya maafisa wa polisi kusema kuwa aliwacha ushahidi
muhimu katika eneo la wizi baada ya kushindwa kusafisha choo alichotumia
kwenda haja.
Wachunguzi wanasema kuwa sampuli za mikojo za Andrew
Jensen katika nyumba hiyo ya Los Angeles ya Thousand Oak inafanana na
vinasaba vya data ya FBI.Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 42 alikamatwa mnamo mwezi Julai 28 mwaka huu takriban mwaka mmoja baada ya uvamizi wa nyumba moja mnamo mwezi Oktoba 2016.
Polisi wanasema kuwa wanakusanya ushahidi ulioachwa katika eneo la uhalifu.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Ventura Tim Lohman alisema kuwaAndrew alijisaidia haja ndogo na hakusaficha choo.
''Watu wengine hawajui kwamba DNA zinaweza kupatikana kupitia maeneo mengine mbali na mate na nywele''.
''Tunachunguza ushahidi wowote ambao umeachwa. iwe sigara iliovutwa, ama mkebe ambao umeachwa tutautathmini''.
Bwana Jensen ambaye aliwachiliwa huru kwa dola 70,000 anazuiliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni