Jumatano, 9 Agosti 2017

Polisi amnunulia mwizi nguo alizoshikwa akiiba dukani

Constable Niran Jeyanesan pictured in an interview

 Alisema kuwa alifika kwenye eneo hilo na kugundua kuwa mtu huyo akiiba nguo ili avae aende kufanyiwa usaili wa kutafuta ajira (interview)

Mwizi wa duka huko Toronto ambaye alishikwa akiiba nguo ili aweze kuivaa kwa usaili alipata fusra asiyoitarajia kutoka kwa polisi ambaye aliitwa kuja kumkamata.
Niran Jeyanesan alikiambia kituo cha habari cha CP24 kuwa mfanyakazi mmoja wa duka la Walmart, aliripoti kuwa mtu huyo wa umri wa miaka 18 alijaribu kuiba shati, tai na soksi.
Alisema kuwa wakati alipofika eneo hilo aligundua kuwa mtu huyo alikuwa akiiba nguo ili avae akienda kufanyiwa usaili wa kutafuta ajira.

Hapo ndipo aliamua kumuachilia na kumnunulia nguo hizo.
"Kijana huyu amekuwa akikumbwa na wakati mgumu maishani na anajaribu kutatua hilo kwa kuitafutia familia yake riziki kwa kujaribu kupata kazi," bwana Jeyanesan alisema.
Akiongea na BBC mkuu wa Jeyanean, Paul Bois alipongeza kitendo hicho. Chanzo BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni