Ijumaa, 13 Desemba 2013

KAMATI TEULE YA BUNGE YA KUCHUNGUZA MIGOGORO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI IKO MOROGORO

Kamati teule ya Bunge ya kuchunguza sababu za matukio ya mara kwa mara ya migogoro kati wakulima na wafugaji ipo mkoani Morogoro kuendelea na kazi hiyo. Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Mhe, Prof Msola (MB) na wajumbe wengine ni pamoja na Mhe J. Selasini (MB) na Mhe Magdalena Sakaya (MB).

WATU SITA WAPOTEZA MAISHA KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI MKOANI KILIMANJARO

Watu sita wamefunikwa na kifusi eneo la Pumwani mkoani Kilimanjaro na wanahofiwa kufa. Watu hao walikuwa wakipakia morram kwenye lori aina ya Fuso ambapo ngema ilikatika na kuwafunika. Juhudi za kufukua kifusi hicho zinaendelea.

Alhamisi, 12 Desemba 2013

BASI LA KAMPUNI YA BURUDANI LAPATA AJALI

Basi la kampuni ya Burdani linalofanya safari zake kati ya Korogwe na Dar es Salaam limepata ajali muda mfupi uliopita maeneo ya Michungwani. Idadi ya waliofariki bado haijajulikana ila maiti na majeruhi ndio wanatolewa katika basi hilo. tutaendelea kukupa taarifa jinsi tunavyozipata. Poleni sana 

Jumatano, 11 Desemba 2013

LICHA YA HUZUNI KWA DUNIA NZIMA, BARACK OBAMA ATIKISA MSIBA WA NELSON MANDELA KWA HUTUBA YAKE JOHANNESBURG.


LICHA ya kuwa ni siku ya huzuni kwa dunia nzima, hotuba ya Rais wa Marekani, Barack Obama imewagusa maelfu ya watu waliokuwa kwenye Uwanja wa FNB katika ibada ya kitaifa kumwaga Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.


Obama aliyetumia dakika 20 katika hotuba yake iliyokuwa ikikatizwa na kelele za kumshangilia, aliwataka vijana wa Afrika na dunia nzima kuiga maisha aliyoishi Mandela kama yeye alivyojifunza mambo mengi kutoka kwa mzalendo huyo.

“Miaka 30 iliyopita nikiwa mwanafunzi, nilisoma Kitabu cha Mandela na tangu siku hiyo nilijifunza, nikajenga roho ya uthabiti. Iliamsha uwajibikaji kwa ajili yangu na kwa ajili ya watu wangu... hakika Mandela amenifanya niwe hivi nilivyo leo. Michelle na mimi tumenufaika sana na Mandela,” alisema Obama na kuongeza:

“Mandela alinifanya niwe mtu ninayesimama mbele yenu leo, alichangia kunifanya kuwa kiongozi bora. Nitaendelea kuiga mfano wake,”

MKUU WA MKOA WA MOROGORO ALAMBA NONDOZ

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Goodluck Ole Medeye (MB) hivi karibuni walitunukiwa shahada ya juu ya heshima (Doctor of Humanity) ya Chuo Kikuu cha California State Christian University.

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kushoto na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mara baada ya kupewa Udaktari wa heshima tarehe 30/11/2013 Morogoro.

Jumamosi, 7 Desemba 2013

MANDELA KUENZIWA KATIKA IBADA YA KIHISTORIA.



Maelfu ya watu wameweka maua kuonyesha mapenzi yao kwa Mandela. 
DUNIA inaendelea kuomboleza kifo cha mzee Nelson Mandela. Jana rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alitangaza siku 10 za maombolezo kwa Mandela aliyefariki Alhamis usiku akiwa na umri wa miaka 95.
 

 Ikulu ya Marekani imesema kuwa rais Barack Obama na mkewe Machelle watakwenda Afrika Kusini wiki ijayo kuungana na viongozi wengine wengi wa dunia, katika ibada ya kumuaga Nelson Mandela. Obama ambaye mwenyewe ni rais wa kwanza mweusi wa Marekani, ataambatana na watangulizi wake wawili, George W Bush na Bill Clinton, ambao pia watasindikizwa na wake zao.

Mwili wa Mzee Madiba utalazwa katika jengo la serikali kwa muda wa siku tatu, kutoa fursa kwa wananchi wa Afrika Kusini kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi waliyempenda. Baadaye mwili wake utasafirishwa kwenda kuzikwa mahali alipokulia Mandela, Qunu.

Ibada ya kumkumbuka Mandela. 
Jana maelfu ya raia wa Afrika Kusini kutoka matabaka yote na rika zote walishiriki katika ibada ya pamoja ya dini mbali mbali, ambayo ilifanyika mjini Cape Town mahali ambapo Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuachiwa huru kutoka jela.

Meya wa jiji la Cape Town Patricia de Lille alisema katika ibada hiyo kuwa watu wa mji huo, weusi kwa weupe, wahindi na wenye damu mchanganyiko, wanaungana kwa mshikamano kumuenzi Nelson Mandela na kukumbuka mchango wake kwa nchi yao.
 
Watu wa matabaka yote wamesononeshwa na kifo cha kipenzi hicho cha dunia Mzee Nelson Mandela. 

Askofu mkuu wa zamani wa kanisa la Angikana nchini Afrika Kusini Desmond Tutu ambaye kama Mandela naye ni mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani, akijipangusa machozi ya huzuni alimsifu Mandela na kusema alikuwa alama ya umoja tangu alipoachiwa huru kutoka gerezani.

Kifo cha Mandela chaiunganisha dunia Nchi kadhaa ulimwenguni zilitangaza maombolezo kwa kifo cha Nelson Mandela. Bendera zilipeperushwa nusu mlingoti katika baadhi ya nchi hizo, zikiwemo za Kiafrika, Marekani, Ufaransa na Uingereza, na kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

India ilitangaza siku tano za maombolezo, na mnara maarufu wa mjini Paris, Eiffel, ulimeremeta kwa rangi za bendera ya Afrika Kusini kwa heshima ya Mzee Madiba.

Pande zenye misimamo tofauti kihistoria zimezungumza kwa sauti moja kumsifu Mandela; Wapalestina na Israel, Dalai Lama na China, Marekani na Iran wote wamemsifu kuwa mtu aliyetetea haki na usawa.

Ibada ya kumuaga Nelson Mandela ambayo itafanyika Jumanne ijayo kwenye uwanja wa mpira mjini Johannesburg inatarajiwa kuwa mojawapo ya mikusanyiko mkubwa ya watu maarufu kuwahi kutokea. DW

MZEE NELSON MANDELA (MADIBA) HATUNAE,


MZEE NELSON MADIBA MANDELA. 

Rais wa zamani wa Africa ya Kusini Mzee Nelson Mandela (miaka 95) maarufu kama mzee Madiba amefariki dunia.

MARA tu baada ya kupokea habari juu ya kifo cha Madiba AlhamisI jioni, rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba na rambi rambi zake  akisema Mandela aliishi na kuifanya ndoto yake kutimia ya kuwa na Afrika Kusini huru na yenye demokrasia. 
Rais Obama alikwenda kwenye  chumba cha White House anakozungumza na waandishi habari wa Ikulu mara tu baada ya kupokea taarifa  za kifo cha  Mandela zilizotangazwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Jumanne, 3 Desemba 2013

MAAJABU YA MWAKA: AFARIKI DUNIA AWEKWA MOCHWARI SIKU 5 SIKU YA KUZIKWA AKUTWA WODINI...!



STORI: MAKONGORO OGING’
SIMULIZI za maajabu zipo nyingi na nyingine zinaendelea kuchukua nafasi, ila hii inaweza kuwa funga mwaka 2013.
Mtanzania Yahya Msemakweli, 34, (pichani) alifariki dunia, akawekwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari), ndani ya jokofu kwa siku tano na

ndugu zake akiwemo mkewe, waliushuhudia mwili wake na kujiridhisha kuwa ni yeye.

Hata hivyo, siku ya sita ambayo ndiyo ilikuwa tarehe ya mazishi, walipoufuata mwili wa Yahya hawakuukuta mochwari, droo aliyowekwa, ilikutwa maiti ya kike, majokofu yote yakafunguliwa lakini hawakuuona.
Siku iliyofuata, yaani siku ya saba, Yahya akakutwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Alitokaje mochwari Temeke hadi Muhimbili wodini? Hakuna anayejua!

Nyongeza ni kwamba kaburi lilishachimbwa, sanda ilishanunuliwa tayari kwa mazishi ya Yahya lakini mambo yalipogeuka, ilibidi wazike mgomba kwa kile kilichoelezwa: “Kimila kaburi huwa halifukiwi tupu.”

HUU NDIYO UTII WA SHERIA BILA SHURUTI KWA ASKARI MBELE YA RAIA, APULIZA BOMU LA MACHOZI KWA ASKARI WAKATI ASKARI HAO WAKIFANYA KAZI YA KUZUWIA MAANDAMANAJI WALIOZINGIRA OFISI ZA SERIKALI NCHINI UKRAINE.

 


Raia hapa juu akiwapulizia bomu la machozi askari polisi wakati maandamanaji zaidi ya 900 waliozingira ofisi za serikali.   TAKRIBANI waandamanaji 1,000 nchini Ukraine wamevamia makao makuu ya ofisi za serikali na kwenye mitaa mbali mbali mjini KIEV leo na kuathiri shughuli za serikali...

DK KIKWETE NA MKEWE WAMJULIA HALI MWENYEKITI WA UDP JOHN CHEYO HOSPITALI YA AGA KGAN JIJINI DAR ES SALAAM


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu7zTi-wCCGYhHv0-sFmnPiaqQ2vACH8_RQ70qg2gDkkgchiEzXDOJhrpMxhj7bcZI5_w3CqmcOKRpisCif_7IPQY6vXQhetRTKWkr9G4uEcN1oUYsvnuoeV88x29dyYaKiuBw7_FQHkN0/s1600/8E9U2010.jpgRAIS Jakaya Kiwete na Mkewe Salma Kikwete akimjulia hali Mwenyekiti wa UDP John Cheyo katika hospitali ya Aga Khan alikolazwa kwa matibabu, na mtoto aliyemk
umbatia Rais ni mjukuu wa Cheyo Gabriel Cheyo. Picha na Fred Maro