Jumatatu, 13 Aprili 2015
HILLARY CLINTON KUWA RAIS BAADA YA OBAMA?
Bibi Hillary Clinton Mke wa Rais wa Marekani wa zamani na Waziri wa nje wa Marekani alimaliza mda wake.
Ametangaza
Rasmi anagombea mwaka 2016... na amezindua Kampeni yake Jana kupitia chama
cha Democratic...Rais wa Marekani Barack Obama alipoulizwa jana huko
Panama...Anamzungumzaje Bi Hillary Clinton....? Anajibu...... "Namfahamu
Kama Mwana mama mshindani wangu 2008...
Namjua
Kama Msaidizi Wangu akiwa Secretary of state (Waziri wa Mambo ya Nje) Na bado ni Rafiki yangu sana kisha akasema ni mwanamama
anayeweza kuiendeleza Amerika...
ASKARI WAZIDIWA NGUVU NA WANANCHI HUKO MOSHI
Hii si
poa! Raia wenye hasira, katikati ya wiki iliyopita waliwachukua vijana
wawili wanaotuhumiwa kuwa majambazi, waliokuwa mikononi mwa polisi,
ambao majina yao yametajwa kuwa ni Mnubi na White kisha kuwateketeza kwa
moto baada ya kuwabaini kuwa ndiyo waliohusika na uvamizi na uporaji wa
maduka mawili ya huko Mwika-Madukani, Moshi vijijini.
Kesho
yake walikamatwa na wananchi walioshirikiana na polisi, baadaye
kukatokea kutoelewana baada ya jeshi hilo kutaka kuwachukua ili
kuwapeleka mbele ya sheria.
“Polisi
waliwaweka katika gari lao ili waondoke nao, lakini wananchi
waliwachomoa na kuwapa kipigo kisha kuwateketeza kwa moto, askari
walijaribu hata mabomu ya kutoa machozi, lakini wakazidiwa,” kilisema
chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamweli alikiri kutokea kwa tukio hilo
Jumapili, 5 Aprili 2015
Al- Shabab yaonya kufanya mashambulizi zaidi Kenya
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa itikadi kali al-Shabab limeonya
kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Kenya kama lile walilofanya Chuo
Kikuu cha Garissa lililouwa watu 148.
Kwa mujibu wa shirika la uchunguzi wa kijasusi CITE, taarifa iliyotumwa
na kundi hilo kupitia mtandao wao siku ya Jumamosi (Aprili 4) imesema
"miji ya Kenya itachuruzika michirizi ya damu."Wanamgambo hao wa itikadi kali za Kiislamu wamesema shambulio la chuo cha Garissa ni kulipiza kisasi kwa mauaji yaliofanywa na vikosi vya Kenya wakati wakipamnana na waasi wa kundi hilo nchini Somalia.
Taarifa yao iliotolewa kwenye tovuti zenye mafungamano na al-Shabaab na mitandao ya Twitter imesema hivyo vitakuwa vita virefu vya ukatili ambapo raia ndio watakaokuwa wa kwanza kukabiliana na maafa.
Taarifa hiyo ya al-Shabaab imesema hakuna hatua zozote zile za tahadhari au usalama zitakazoweza kuwahakikishia usalama wao,kuzima shambulio jengibe au kuzuwiya umwagaji damu mwengine.
Idadi ya waliouwawa Kenya huenda ikapanda
Idadi ya watu waliouwawa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa Somalia dhidi ya chuo kikuu nchini Kenya huenda ikapanda na kufikia zaidi ya watu147,duru za serikali pamoja na vyombo vya habari zimesema.
Hasira miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo imepanda kuhusiana na kile wanachosema kuwa ni kushindwa kwa serikali kuzuia umwagikaji huo wa damu.Wakiwa wamejifunga miripuko, wapiganaji waliokuwa wamefunika nyuso zao wa kundi la al-Shabaab walikivamia chuo kikuu cha Garissa, kiasi ya kilometa 200 kutoka mpaka wa Somalia, katika shambulio lililofanyika alfajiri siku ya Alhamis.
Tishio la ugaidi lakatiza ibada Mombasa
kanisa la kianglikana Mombasa Kenya
Ibada katika kanisa moja la Kianglikana nchini Kenya ilikatizwa ghafla baada ya tishio la ugaidi siku ya Jumapili.
Waumini walihamishwa kutoka kanisani hilo baada ya gari moja kuingia ndani ya uwanja wa kanisa kimabavu.Kenya iko katika hali ya tahadhari baada ya mauaji ya watu wasiopungua 150 kaskazini mwa taifa taifa hilo.
Ibada hiyo ya Pasaka iligeuka na kuwa mbio za mguu niponye baada ya waumini kuarifiwa kuhusu gari hilo lisilo na nia njema.
Askofu wa kanisa hilo, Julius Kalu, amesema aliarifiwa kuhusu gari ambalo liliingizwa ndani ya uwanja wa kanisa bila hilo idhini kabla ya kusimamishwa kwenye lango kuu la kanisa lenyewe.
Askofu Kalu amesema waliokuwa ndani ya gari hilo walitoroka
Polisi waliitwa, na baada ya kulikagua gari hilo walilivuta hadi makao makuu ya polisi.
Mkuu wa polisi eneo la Mombasa Robert Kitur amesema hawakupata kitu, lakini wamelizuia gari hilo kwa uchunguzi zaidi.
SERIKALI YA KENYA YAMTAMBUA MUUAJI
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wakitoroka shambulio
Serikali
ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya
chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab
CHARLES HILLAY AONDOKA BBC KUTUA AZAM
Miongoni
mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni
Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata
kupitia Radio One pia. Charles
Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha
Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon
Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.
REAL MADRID YAIFUNGA GRANADA 9-1 HUKU RONALDO AKIPIGA 5
REAL
MADRID: Casillas; Arbeloa, Ramos, Varane, Marcelo; Rodriguez (Jese 61)
Kroos (Illaramendi 57), Modric; Bale, Benzema (Hernandez 61), Ronaldo
Subs not used: Navas, Nacho, Coentrao, Silva
GRANADA:
Oier; Foulquier, Mainz, Babin (Murillo 61), Juan Carlos; Fran Rico
(Silvestre 57), Iturra; Ibanez, Rochina (Piti 53), Candeias; El Arabi
Subs not used: Roberto, Nyom, Javi Marquez, Riki
Booked: Piti, Murillo
Goal: Ibanez 74
YANGA YASONGA MBELE LICHA YA KUFUNGWA
Leo APRIL
4 2015 historia imeandikwa kwenye michezo TZ, wawakilishi wetu kwenye
Michuano ya Shirikisho la Soka Afrika, Yanga SC wameikamilisha kazi ya
kutuwakilisha uwanjani Zimbabwe ambapo walikuwa wakipambana na timu ya
nchi hiyo FC Platinum kwenye mchezo wa marudiano.
Matokeo ya mechi ya kwanza ambayo ilichezwa TZ kati ya timu hiyo na
Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa goli 5-1 iliwafanya mabingwa hao
kucheza mchezo huu kwa ujasiri mkubwa sana, huku wenzao wakijiongeza
nguvu ya ziada ili wapate matokeo mazuri nyumbani kwao.

Dakika 90
zilikamilika zikaongezwa nyingine nne lakini haikusaidia kubadili
matokeo hayo,FC Platinum walitoka na ushindi wa goli 1-0, lakini matokeo
hayo bado yanaipa nafasiYanga kuendelea na mashindano hayo huku safari
ya Platinum ikiishia hapohapo nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Mandav
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


