Jumatano, 3 Juni 2015
ANGALIA RAIS ANAYETEMBELEA VW BEETLE TZ VIPI
SERIKALI YAMALIZA MGOGORO NA WAFANYABIASHARA.
Waziri
wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea
kutoa ushirikiano, utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali
kwa maslahi na maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka
uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya
Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
2-
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru
Waziri wa Fedha kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka
hiyo hasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la
ukusanyaji Kodi nchini.
3-
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa
serikali katika utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na kuahidi
kuendelea kutoa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya
taifa ya kuwa na uchumi imara kupitia ukusanyaji wa Kodi.
RAFA KOCHA MPYA WA REAL MADRID
Aliyekuwa kocha wa Napoli Rafa Benitez amethibitishwa kuwa k ocha wa Real Madrid katika kandarasi ya miaka mitatu.
Benitez
mwenye umri wa miaka 55 anachukua mahala pake Carlo Ancelotti ambaye
aliondoka katika kilabu hiyo miezi 12 tu baada ya kuisaidia kushinda
kombe lao la kumi la vilabu bingwa Ulaya.Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa Napoli ,baada kufanikiwa na vilabu kadhaa vya Ulaya.
Baada ya kuisaidia Valencia kushinda kombe la Uefa mwaka 2004,mwaka unaofuatia alielekea Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside.
Miaka miwili baadaye aliisaidia Liverpool kufika katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa Chelsea waliposhinda kombe la Yuropa
FREDRIK SUMAYE AJA NA MPYA ATANGAZA NIA
INTERPOL YASAKA MAAFISA 6 WA FIFA
Shirika
la maafisa wa polisi wa kimataifa Interpol limetoa ilani ya kukamatwa
kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na
ufisadi.
Agizo hilo linawalenga maafisa wanne wa mashirika makuu
pamoja na maafisa wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani
FIFA akiwemo aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita.
Ilani hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe ,lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.
PROFESA MUHONGO ATANGAZA NIA
WAZIRI
wa zamani wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo, ametangaza nia rasmi
ya kuwaomba Wana CCM kumteua kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mwezi Oktoba, huku akisema ni yeye pekee mwenye uwezo wa
kuikwamua nchi katika hali mbaya ya umasikini na ukosefu wa wataalamu,
hali inayoifanya nchi ishindwe kupiga hatua.
MWILI WA MAREHEMU EUGEN ELISHIRINGA MWAIPOSA AAGWA LEO KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA

Marehemu EUGEN ELISHIRINGA MWAIPOSA
TANZIA
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mhe. EUGEN
ELISHIRINGA MWAIPOSA kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 June 2015
nyumbani kwake Dodoma ambako amekuwepo kushiriki Mkutano wa Bunge la
Bajeti.
Mwili wa
Marehemu umeagwa leo tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika
viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani
kwake Ukonga, Dar es Salaam.
BWANA alitoa, BWANA ametwaa. Jina la BWANA lihimidiwe. Amina!
BREAKING NEWS SEPP BLATTER AJIUZULU URAIS WA FIFA
Sepp
Blatter amejiuzulu rasmi urais wa FIFA kufuatia tuhuma za rushwa zinazokabili taasisi hiyo ambayo ndiyo kubwa zaidi duniani inayosimamia soka. Katika hatua inayoshangaza kutoka makao makuu ya FIFA mjini Zurich nchini Uswisi Blatter alisisitiza kuwa anaondoka katika hilo baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka 17 akiwa kiongozi mwenye nguvu zaidi katika masuala ya soka. Blatter kwa sasa anakabiliwa na uchumguzi maalumu kutoka katika shirika la upelelezi la Marekani FBI
ambalo linachunguza kama rushwa hizo ziliruhusiwa na Blatter na timu yake ya uongozi.
Jumatatu, 1 Juni 2015
MZEE RUKSA ATIMIZA MIAKA 90
Rais Mstaafu awamu ya Pili Alhaji Hassan Mwinyi akitoa salamu zake
kwa wageni waalikwa wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa ambapo jana
alitimiza umri wa miaka 90.Sherehe hiyo ilifanyika katika hoteli ya Sea
Cliff na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Mstaafu awamu ya pili
Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa kutimiza miaka 90 wakati wa sherehe ya
kuzaliwa kwake iliyofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es
Salaam jana.Kushoto ni Mkewe Mama Siti Mwinyi.
Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha
ya pamoja na familia yake watoto na wajukuu zake wakati wa sherehe yake
ya kuzaliwa ambapo alitimiza umri wa miaka 90 jana katika hoteli ya Sea
Cliff jijini Dar es Salaa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


