Mwalimu mmoja wa
shule ya msingi katika eneo la kati nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha
miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake.
Jumamosi, 18 Juni 2016
JK KUENDELEA KUPAA: ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
KITUO
cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya
(EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais
Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador)
wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Caribean na Pacific.
Katika
barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora,
CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,
ameteuliwa kwa kutambua mchango na juhudi zake katika kukiendeleza
kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika
wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha
katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa
kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na
uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani
na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya
mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk.
Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni
ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani
na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof.
Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018
Ijumaa, 10 Juni 2016
WATOTO SITA WAFA UBATIZONI ZIMBABWE
Robert Mugabe
Watoto sita
wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika
mto nchini Zimbabwe. Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo
ambao maji yake ni ya baridi; watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana
na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.
Pia walisema kuwa wamemkamata mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii na ambaye alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake.
Wakili apigwa na kuchaniwa nguo mbele ya majaji China
Wakili wa China aliyepigwa na kuchaniwa nguo akitoka mahakamani
Mawakili wengi wa
China wamenyanyaswa, kukamatwa na hata kufungwa jela lakini picha ya
mmoja wao aliyekuwa na nguo zake zilizochanwa na maafisa wa polisi
imevutia hisia nyingi nchini China.
Yeye na mawakili wengine waliwaambia maafisa wa mahakama kwamba alishambuliwa na maafisa watatu katika mahakama moja mbele ya majaji wawili ambao walikataa ombi lake la kutaka kuanzisha kesi katika mahakama ya wilaya ya Nanning Mkoani Guangxi.
Bw Wu alipewa nguo nyengine lakini alijua uwezo wa kile alichokuwa akipanga kukifanya.''Asante alisema''.
Wakili huyo baadaye alitembea kupitia mlango wa mbele akiwa amebeba nakala zake za mahakamani akiwa na kalamu iliowekwa katika mfuko wa shati liliposuliwa.
Baadaye alipigwa picha nje ya jengo hilo la mahakama na picha hiyo kusambazwa. Hii ilikuwa na maana ya kutuma ujumbe kewa nchini China mawakili wananyanyaswa. Meseji sent
Ijumaa, 3 Juni 2016
Video yawatia matatani wanafunzi waliofanya mtihani India
Wanafunzi 14
walioongoza katika matokeo ya mtihani wa mwisho katika jimbo la Bihar
nchini India watalazimika kufanya tena mtihani kufuatia madai kwamba
walihusika na udanganyifu, serikali ya jimbo hilo imsema.
Uamuzi
huo uliafikiwa baada ya mmoja ya wanafunzi hao Ruby Rai mwenye umri wa
miaka 17 kuviambia vyombo vya habari kwamba sayansi ya siasa inahusisha
kupika.Jumatatu, 30 Mei 2016
SHEKHE AUAWA KATIKA FUMANIZI
JESHI la Polisi Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Likweso, Tarafa ya Mchoteka, Ally Mchumwa
kwa tuhuma za mauaji ya Shekhe wa kijiji hicho.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Zubery Mwombeji, alisema tukio hilo limetokea
Mei 22, mwaka huu, baada ya mtuhumiwa (Mchumwa), kumfumania akifanya tendo la ndoa na mkewe.
"Mauaji haya yametokea saa tatu
asubuhi wakati marehemu ambaye amefahamika kwa jina la Seleman Mwalabu
(45), mtuhumiwa na mkewe Mariamu Husein, wakisaidiana kuvuna njugu
shambani.
"Wakati wakiendelea na kazi hiyo, mtuhumiwa alitoka
kidogo na kumuacha marehemu pamoja na mkewe wakiendelea na kazi hiyo,
aliporejea hakuwakuta shambani hivyo akashtuka," alisema.
Kamanda
Mwombeji alisema wakati mtuhumiwa akiwa katika kwenye sintofahamu hiyo,
alisikia sauti ikitoka porini jirani na shamba lake hivyo aliamua kwenda
na kumkuta mkewe na mtuhumiwa wakiwa uchi wa mnyama ikiashiria wametoka
kufanya tendo la ndoa.
Kutokana na hali hiyo, mtuhumiwa
alichomoa kisu na kumchoma nacho marehemu shingoni, kufariki papo hapo
na yeye mwenyewe akajisalimisha kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baadaye
kupelekwa polisi.
Aliongeza kuwa, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika
SAMATTA AIPELEKA GENK EUROPA LEAGUE
Tarehe May 29, Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufuzu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).
Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi.
Alhamisi, 19 Mei 2016
DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 3 KUTUMIKA KUANZISHA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kushoto)
akiongea na Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi
wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo
mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu
pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji toka Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC), Bwana Mlingi Mkucha.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe.
Dkt. Dalaly Kafumu (kulia) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa
Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba
chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei,
2016. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles
Mwijage.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
JUMLA
ya dola Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa
Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.Kauli hiyo
imetolewa Leo mini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari mini Dodoma.
Jumatatu, 16 Mei 2016
Lidege likubwa zaidi duniani latua Australia
Maelfu ya watu
nchini Australia wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa
zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini
humo.
Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila
ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito
wa tani 117.KITISHO CHA BOMU CHAAHIRISHA MECHI YA MAN U
Hofu ya kuwepo bomu uwanjani imesababisha mechi ya Manchester United na Bournemouth kuahirishwa.
Mechi ya mwisho
katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na
Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old
Trafford.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


