Jumatatu, 30 Mei 2016

SHEKHE AUAWA KATIKA FUMANIZI

JESHI la Polisi Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Likweso, Tarafa ya Mchoteka, Ally Mchumwa
kwa tuhuma za mauaji ya Shekhe wa kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Zubery Mwombeji, alisema tukio hilo limetokea Mei 22, mwaka huu, baada ya mtuhumiwa (Mchumwa), kumfumania akifanya tendo la ndoa na mkewe.

"Mauaji haya yametokea saa tatu asubuhi wakati marehemu ambaye amefahamika kwa jina la Seleman Mwalabu (45), mtuhumiwa na mkewe Mariamu Husein, wakisaidiana kuvuna njugu shambani.

"Wakati wakiendelea na kazi hiyo, mtuhumiwa alitoka kidogo na kumuacha marehemu pamoja na mkewe wakiendelea na kazi hiyo, aliporejea hakuwakuta shambani hivyo akashtuka," alisema.

Kamanda Mwombeji alisema wakati mtuhumiwa akiwa katika kwenye sintofahamu hiyo, alisikia sauti ikitoka porini jirani na shamba lake hivyo aliamua kwenda na kumkuta mkewe na mtuhumiwa wakiwa uchi wa mnyama ikiashiria wametoka kufanya tendo la ndoa.

Kutokana na hali hiyo, mtuhumiwa alichomoa kisu na kumchoma nacho marehemu shingoni, kufariki papo hapo na yeye mwenyewe akajisalimisha kwa uongozi wa Serikali ya kijiji na baadaye kupelekwa polisi.

Aliongeza kuwa, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake baada ya uchunguzi kukamilika

SAMATTA AIPELEKA GENK EUROPA LEAGUE


Tarehe May 29, Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufuzu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).
Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi.

Alhamisi, 19 Mei 2016

DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 3 KUTUMIKA KUANZISHA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji toka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bwana Mlingi Mkucha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu (kulia) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.


Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

JUMLA ya dola Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.Kauli hiyo imetolewa Leo mini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari mini Dodoma.

Jumatatu, 16 Mei 2016

Lidege likubwa zaidi duniani latua Australia

Antonov An-225 Mriya ndiyo ndege refu na nzito zaidi kuwai kujengwa.
Maelfu ya watu nchini Australia wanaopenda ndege walikusanyika kutizama ndege kubwa zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini humo.
Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito wa tani 117.

KITISHO CHA BOMU CHAAHIRISHA MECHI YA MAN U

 
 Hofu ya kuwepo bomu uwanjani imesababisha mechi ya Manchester United na Bournemouth kuahirishwa.

Mechi ya mwisho katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old Trafford.

Jumatatu, 18 Aprili 2016

TETEMEKO LAUA WATU 272 ECUADOR

Rescue workers search the rubble of a collapsed building for victims in Guayaquil, Ecuador, on Sunday, April 17. A magnitude-7.8 quake struck off Ecuador's central coast on Saturday, April 16, flattening buildings and buckling highways. It's the deadliest quake to strike the South American country in decades.
Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 katika vipimo vya Ritcher limeikumba nchi ya Ecuador na kuua watu wapatao 272 na kujeruhi wengine 2500.

Tetemeko hilo ni kubwa na limekumba maeneo ya pwani ya nchi hiyo.

Juhudi za uokozi zinaendelea.

KUNGUNI NOMA!!! SASA WAWA SUGU KWA SUMU

 
Kumuua kunguni sugu kunaweza kuhitaji dawa yenye makali mara elfu moja zaidi ya ile inayohitajika kuua wadudu wasio sugu.

Huenda kunguni wakawa sugu kwa dawa, hali ambayo itasababisha wadudu hao kuwa na uwezo kuhimili makali ya dawa ya kuua wadudu.
Idadi ya watu inayozidi kuongezeka na safari za kimataifa zimesadia mdudu huyo kuwa kero kwenye mahoteli kote duniani.

BARCA KIPIGO CHA TATU MFULULIZO





Messi
 Messi alifunga bao lake la 500

Miamba wa Uhispania Barcelona wamepokea kichapo cha tatu mtawalia La Liga baada ya kulazwa na 2-1 Valencia nyumbani kwao Jumapili.
Hii ni mara yao ya kwanza kushindwa mechi tatu mfululizo ligini tangu 2003.
Kitulizo pekee kutoka kwa mechi hiyo ni kwamba mshambuliaji wao matata Lionel Messi kufunga bao lake la 500.
Ivan Rakitic aliingiza wavuni krosi iliyotoka Guilherme Siqueira na kuwapatia Valencia uongozi wa kushangaza.

Jumamosi, 16 Aprili 2016

TETEMEKO LA PILI LAIKUMBA JAPAN

 
Tetemeko hilo lilisababisha kuporomoka kwa majengo
Maafisa nchini Japan wanasema kuwa tetemeko kubwa la ardhi limewaua takriban watu 19 na kusababisha uharibifu mkubwa.
Tetemeko hilo ambalo ni la pili kukumba kisiwa cha Kyushu ndani ya siku mbili, limesababisha kuporomoka kwa majengo, limeharibu barabara pamoja na mifumo ya maji na umeme.
Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.3 kwenye vipimo vya Richter.

Alhamisi, 14 Aprili 2016

MTU MREFU ZAIDI DUNIANI AWASILI MAURITIUS

 
Sultan Kösen ana urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51.
Mtu mrefu zaidi duniani raia wa Uturuki Sultan Kösen aliye na urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51 amewasilia nchini Mauritius leo asubuhi.
Sultan alilakiwa na umati katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi, kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye ukusara wa facebook wa mtandao wa habari wa nchi hiyo.