MBEYA.
KUNDI la vijana 60, juzi walipora mwili wa marehemu
Gabriel Ngalele ukiwa unaombewa kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies Of God
(TAG) eneo la Uyole jijini baada ya kuchoshwa na ibada ndefu ya
mchungaji.
Ibada hiyo ilikuwa ikiendeshwa na
Mchungaji, Edward Mtweve wa kanisa hilo ambaye alijikuta kwenye mazingira magumu
baada ya vijana hao wanaodaiwa kuwa ni madereva wa pikipiki kuvamia madhabahu na
kubeba sanduku lililokuwa na mwili wa marehemu.
Marehemu Ngatele
alikuwa dereva wa pikipiki na alifariki kwenye ajali iliyotokea eneo la Sae
baada ya pikipiki yake kuligonga lori lililoharibika katikati ya barabara.
Katika ajali hiyo, abiria pia alifariki.
Mwili wa marehemu
ulipelekwa katika kanisa hilo, na wakati mchungaji akiendesha ibada kulijitokeza
kelele za hapa na pale na kusababisha mchungaji kuomba utulivu mara kadhaa.
Lakini kelele nyingi zililipuka ghafla zikiwamo za kulalamika kwamba
ibada ilikuwa ndefu na hatimaye vijana wengi walionekana wakiingia kwenye mlango
na kuvamia madhabahu na kutoka na mwili wa marehemu.
Baada ya
kuuchukua mwili, vijana hao walikwenda kwenye makaburi kuuzika wakati naye
mchungaji akiendelea kuhubiri waumini waliobaki ndani ya kanisa.
Mchungaji Mtweve alilazimika kwenda nyumbani baada ya kumaliza ibada
badala ya makaburini, huku vijana nao wakiendelea na taratibu za mazishi kwa
utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa waendesha pikipiki Mbeya, Vicent
Mwashoma.
Mwendesha pikipiki aliyetajwa kwa jina la Bahati Mwasote
alilazimika kuendesha ibada ya mazishi.
Mchungaji Edward Mtweve
alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema alisikitishwa na kitendo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni