Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
JIJI la Dar es Salaam nchini Tanzania ni moja ya majiji maarufu ambalo limepata nafasi ya 39 katika majiji ambayo watu mashuhuri na watalii wanaweza kutembelea duniani.
Ni majiji makubwa yenye mageuzi ya muonekano na vitu vya kale vya kuvutia pamoja na wanyama wazuri na madhari ya kipwani inayoweza kumvuta mtalii kutoka kokote duniani.
Dar es Salaam ilipata nafasi ya 39 katika sehemu moja tulivu katika pwani ya Afrika Mashariki na mji mzuri kwa ajili ya biashara.
Tanzania inaweza kuwa imejulikana kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na mabonde na milima ya kuvutia bila kusahau mbuga ya wanyama Serengeti.
lakini mapigo halisi ya nchi hupatikana katika mji wake mkubwa, na ndiyo maana Dar es Salaam ikapata nafasi ya 39 duniani.
Watafiti wa mambo ya kale na utalii wanasema taarifa hiyo ya gazeti la New York Times la Marekani itaipa nchi nafasi ya kujulikana zaidi duniani katika sekta ya utalii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni