Jumatatu, 6 Januari 2014

MAELFU WAMZIKA DK MGIMWA KIJIJINI KWAKE MAGUNGA IRINGA


Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe, Zakia Bilal (kulia) wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam jana.
 
Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana waliongoza maelfu ya wakazi wa mkoani Iringa na mikoa ya jirani katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga, Dk William Mgimwa (CCM).
 
Pamoja na Rais na Waziri Mkuu, mawaziri mbalimbali, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, watendaji wa wizara, na viongozi wa CCM na vyama vya upinzani walihudhuria mazishi hayyo yaliyofanyika kijijini kwake Magunga, Kalenga Iringa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni