Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akioneesha mbele ya waandishi wa habari Ofisi kwake meno ya tembo vipande 2 yenye thamani ya shilingi 22 hapo jana aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Bartholomeo Mtongwa hapo Machi 8 katika kijiji cha Kilida katika tarafa ya Mamba wilaya ya Mlele ambapo pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na gobole 1 na risasi 14.
Mkazi wa kijiji cha Kilida tarafa ya Mamba wilaya ya mlele Bartholomeo Mtongwa (58) akiwa katika kituo cha polisi cha mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 na gobole moja pamoja na risasi 14 mtuhumiwa alikamatwa hapo machi 7 mwaka huu majira ya saa mbili usiku nyumbani kwake katika kijiji cha kilida.
Na Walter Mguluchuma Mpanda Katavi
oMtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Bartholomeo James Mtongwa 58Mkazi wa Kijiji cha Kilinda Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amekamatwa akiwa nameno vipande viwili vyenye uzito wa kilo 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 22 pamoja na Bunduki moja aina ya Gobore na Risasi 14
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi msaidizi mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo machi 7 mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufutia taarifa ambazo ambazo zililifikia jeshi la polisi pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kupata taarifa kuwa mtuhumiwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria ambapo taarifa hizo zilipatikana hapo Machi 6 kutoka kwa Raia wema
Alifafanua ndipo siku hiyo ya tukio majira ya saa mbili usiku polisi wakiwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walifika kwenye kijiji hicho cha Kilinda nyumbani kwa mtuhumiwa Bartholomeo na kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanikiwa kukamata risasi 14
Kidavashari alieleza wakati askari hao wakiendelea na upekuzi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji walilitilia shaka eneo moja la nyumba hiyo ya mtuhumiwa kutokana na eneo hilo kuonekana kuwa limechimbwa
Alisema ndipo askari walipoamua kuchimba eneo hilo na baada ya kufukua kwa kitambo kidogo walifanikiwa kukuta meno ya Tembo vipande viwili vyenye uzito wa kili 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 yakiwa yamefukiwa ardhini kwenye shimo
Baada ya kukamatwa kwa meno hayo ya Tembo polisi walianza kumhoji mshitakiwa kwa kumtaka awaelekeze sehemu ambayo amekuwa akihifadhi Silaha ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili
Kidavashari alieleza baada ya mahojiano mtuhumiwa aliweza kueleza kuwa bunduki ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili ameificha kwenye eneo linaloitwa King’anda lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Alisema siku ya tarehe 8 Machi majira ya saa nane mchana mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuwapeleka katika eneo la King’anda ndani ya Hifadhi ya Katavi na aliweza kuwaonyesha silaha hiyo Bunduki aina ya Gobore ikiwa imehifadhiwa kwenye kichaka
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wawote mara baada ya upelelezi wa tukio hili utakapo kuwa umekamilika mapema iwezekanavyo pia jeshi la polisi Mkoa wa Katavi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na uwindaji haramu wa rasilimali za Taifa ili kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni