Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh, Fransisi Miti amesitisha huduma ya kivuko kati ya ulanga na kilombero kwa kutumia pantoni ya kivuko MV. KILOMBERO hadi hapo maji yatakapo pungua kutokana na kivuko hicho kuzidiwa na nguvu ya maji.
Amewaomba wananchi wa wilaya zote mbili kuto kusafiri kwa muda kwa safari zisizo za lazima hadi hapo maji yatakapo pungua huku kwa wale wanao lazimika kusafiri sasa kutumia boti ndogo zilizopo na kuacha kutumia mitumbwi ambayo si salama.
hatariii |
Wakati huo huo maji hapo juzi jioni yalikata mawasiliano ya barabara kati ya Ulanga na Kilombero kwa kuzoa moja ya kalavati upande wa Ifakara ambapo moja ya gari lilisombwa na maji huku nayo pantoni ilisitisha huduma kwa muda baada ya kusombwa na maji na kupelekwa upande wa bondeni.
Mitumbwi na boti ndogo zilionekana zikivusha watu hapojuzi huku nauli katika boti na mtumbwi wa kawaida kwa mtu mmoja ikipanda kutoka shilingi 200 ya kawaida hadi 1000 kwa mtu mmoja huku pikipiki zikisafirishwa kwa kati ya shilingi 3000 hadi 8000.
baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi hapo juzi katika eneo hilo la kivukoni wamesema hali mbaya ya usafiri inayojitokeza sasa nikutokana na uzembe wa kutoyatengeneza makalavati hayo katika msimu wa kiangazi huku mamlaka inayohusika na utengenezaji wa barabara katika eneo hilo ikiendelea kukwangua tuta la barabara hiyo lililo wekwa na campuni ya BENACO miaka hiyo, hali iliyopelekea tutahilo kuwa dhaifu.
Wakati hayo yakiendelea leo imeripotiwa moja ya mchina amejinyonga,
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana zinadai mchina huyo aliyekuwa anahusika na michoro ya ujengaji wa daraja amejinyonga kutokana na upweke uliokuwa unamsibu.
baadhi ya watu wakaribu na vibarua wa ujenzi wa daraja la mto Kilombero ambalo bado halija anza kujengwa hadi sasa licha ya kutakiwa kukamilika mwakani wamesema yawezekana mchina huyo amejinyonga kutokana na hali mbaya iliyojitokeza kutokana na kuzama kwa makaravati ambayowalikuwa wamekwisha jenga.
mvua za mwaka huu katika wilaya ya Kilombero na Ulanga zinadaiwa kuwa ni kubwa kuwahi kutokea ambapo miundombinu ya barabara iomehalibiwa vibaya.
Barabara kutoka lupiro kwenda mahenge eneo la Fimbo |
Mto Kilombero |
Muendesha Mtumbwi Kazini |
Moja ya usafiri unaotumika |
Moja ya karavati yaliyojengwa na wachina |
Karavati jipya |
Eneo la barabara Kivukoni upande wa Ifakara |
Kalavati likiwa limezamishwa na maji |
Kalavati likiwa limemeguka upande |
Foleni ya Magari Kabla ya kufikiakivukoni |
Katapila likiwa limewekwa katikati ya barabara kuzuia njia watu wasipite kutoa nafasi ujenzi uendelee. |
kivukoni- hali halisi |
eneo liliosombwa na maji na kuvunja mawasiliano yaUlanga na Kilombero |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni