Mtoto Mwajuma Athuman[6] aliyeokotwa na wanajeshi kambi Pangawe baada ya kukimbia mateso ukatili anaodai kufanyiwa na mama yake mkubwa Bi,Ashura Omar amefichua siri nzito mbele ya Afisa Mtendaji wa kata ya Kingolwira
Mwenyekiti wa Mtaa Tank la Maji kata ya Kingolwira Bw Mohamed Said akiwa na mtoto huyo
Mtoto huyo akiwa na Makovu aliyodai yametokana na kipigo toka kwa mama yake mkubwa
Mtoto huyo hawezi kutembea baada ya mguu wa kushoto uliokuwa na kidonda kuvimba, akidai kidonda hicho pia kimetokana na kichapo toka kwa mama yake huyo.
Mwenyekiti akimbeba mtoto huyo kuelekea ofisi ya Afisa Mtendaji
Mama mkubwa wa mtoto huyo baada ya kuona kamera za Mtandao huu zikimmulika alificha sura yake kwa kuinama
Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw Rubeni Ndimbo [kulia] akimhoji mama huyo aliyeficha sura yake; aliyevaa nguo za kitenge ni Afisa Mtendaji wa mtaa wa Tenk la Maji Bi, lnocencia Mbena Patrick, mwingine aliyekuwepo kwenye kikao hicho ni Mwandishi wa mtandao huu
Baada ya mtoto huyo kieleza kwamba mama yake alimtesa baada ya kugoma kurithishwa uchawi, mwenyekiti huyo wa mtaa alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi
Baada ya kikao hicho kukamiliza mwandishi wa mtandao huu pamoja na mwenyekti wa mtaa huo walijitolea kwenda Zanahati ya Kingolwira na kumtibia mguu mtoto huyo. Pichani wauguzi wa Zanahati hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakimtibu mtoto huyo
Muuguzi akimfunga baada ya kusafisha na kuweka dawa kidonda hicho
Mwajuma akitolewa nje baada ya kupata tiba
Akifanya mazoezi ya kutembea
Dustan Shekidele, Morogoro.
Mtoto huyo mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza akihojiwa kwa zaidi ya masaa 2 na Uongozi wa kata ya Kingolwira alifichua siri ya mama yake huyo ambaye ni Mganga wa Kienyeji kumtesa.
" Kabla sijaanza shule nilikuwa nikiishi na mama kwa upendo mkubwa lakini nilipoanza shule ya chekechea mwaka jana mama alinilazimisha kutembea usiku bila nguo mimi na yeye na watu wengine nilipokataa ndio ananipiga, nikimuuliza anasema anataka kunifundisha uganga"alisema mtoto huyo.
Baada ya kauli hiyo Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw Ruben Ndimbo alipomuuliza mama huyo kuhusiana na madai hayo mazito alikana huku akitishia kumtolea radhi mwanae kwa kile alichodai amemdhalilisha.
TUJIKUMBUSHE
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Pangawe mkoani Morogoro wamemuokota mtoto mwenye umri wa miaka sita, Mwajuma Athuman aliyedai kukimbia mateso kutoka kwa mama yake mkubwa Juni 17, mwaka huu.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinasema Mwajuma ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge mjini hapa, aliokotwa katika vichaka vilivyopo pembeni ya kambi hiyo akitokea Kijiji cha Ngionolo kilichopo jirani ambako ndiko anakoishi mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la Ashura ambaye ni mganga wa kienyeji.
Baada ya kumuokota na kumhoji, wanajeshi hao walimpeleka kwa mjumbe, Magessa Mwita ambaye naye alimpeleka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tangi la Maji, Mohamed Said.
Mwandishi wa habari hizi alimkuta mtoto huyo akiwa na makovu kichwani na kidonda kikubwa mguuni kilichosababisha ashindwe kutembea ambapo alidai kilitokana na kipigo kutoka kwa mama yake huyo.
“Nimekimbia nyumbani, mama ananipiga kila siku nikitoka shuleni, nilifika kambi ya jeshi kwa mtoto mwenzangu ninayesoma naye lakini nilipotea nyumba yao.
“Nilipoona giza linaingia nikaamua kutafuta kichaka nilale ili asubuhi niende shule halafu niondoke na rafiki yangu nikaishi kwao. Juzi ndiyo askari walinikuta na kunileta hapa,” alisema mtoto huyo.
Kuhusu wazazi wake, mtoto huyo alisema mama yake alifariki dunia yeye akiwa na umri wa miaka miwili, baba yake anaishi Mwanza ambako ameoa mke mwingine. Mama mkubwa huyo alipoitwa mbele ya viongozi wa serikali ya mitaa, alikiri kuishi na mtoto huyo, lakini alikanusha kumtesa.
Hata hivyo, mwanamke huyo aling'ang'ania kumchukua mtoto wake ili arejee naye nyumbani, lakini viongozi hao waligoma na kwa zaidi ya siku nne aliishi nyumbani kwa Mohamed Said.
Katika kikao cha pamoja kati ya viongozi wa serikali ya mtaa na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, mama mkubwa huyo na mwandishi wa habari hizi walikubaliana kuwasiliana na mjomba wa mtoto aishiye jijini Dar, Anjelu Shindano ambaye aliahidi kutuma nauli ili mtoto huyo aweze kwenda Mwanza kwa baba yake mzazi.