Jumatano, 13 Agosti 2014

CANADA YATOA CHANJO YA EBOLA KWA MAJARIBIO


Serikali nchini Canada inasema kuwa itatoa hadi dozi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa shirika la afya ulimwenguni WHO.
Hii ni kwa elengo la kusadia kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao hadi sasa umewaua zaidi ya watu 1,000.
 
Hatua hii ni baada ya shirika la afya duniani kusema ni sawa kimaadili kutumia dawa ambayo bado infanayiwa majaribio kutibu wagonjwa katika hali ya dharura.
Waziri wa afya nchini canada Rona Ambrose amesema kuwa nchi hiyo imetengeneza karibu dozi 500 za dawa hio lakini haijafanyiwa majaribio kwa binadamu.
Wataalamu wanaonya kuwa huenda ikachukua hadi miezi sita kuunda kiwango cha dawa ambacho kinaweza kutumiwa.
Kampuni moja wa kimarekani ambayo ilikuwa imetengeneza dawa za majaribio inasema kuwa kwa sasa kiwango cha dawa ilicho nacho ni kidogo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni