NOAH
Kurasa
HOME
CONTACT US
NAFASI ZA KAZI
Jumatano, 13 Agosti 2014
KIBAKA AUAWA MKUNDI MOROGORO KWA WIZI WA PIKIPIKI
Kijana mmoja ambaye jina lake na sehemu anayoishi hafikufahamika mara moja ameuawa kikatili kwa kuchomwa na moto na wananchi wenye hasira akidaiwa kuiba pikipiki maeneo ya katikati ya mji wa Morogoro.
Tukio hilo limetokea jana maeneo ya Mkundi nje kidogo ya mji wa Morogoro
Kwa Mujibu Mashuhuda wa Tukio Hilo walisema waliona P
ikipiki zaidi ya 20 zikitokea Mjini. Na moja ya boda boda hizo zilimbeba Kijana huku akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi huku pikipiki nyingine ilibeba dumu la mafuta na kiroba cha majani makavu, wapofika hapa walimlazimisha kushuka huku wakimshushia kichapo na baadaye walimchoma moto walipojiridhisha amekufa waliwasha pikipiki zao na kuondoka eneo hili kwa mbwembwe.
Boda boda hao walisema walimkamata kibaka huyo akitaka kupora moja ya pikipiki zao”
Uchunguzi uliofanywa umebaini kwa sasa kumekuwa na vita isiyo rasmi kati ya vibaka na bodaboda ambapo vikaba kabla ya kuwapora pikipiki boda boda hao huwafunga kamba kisha kuwauwaa kikatili na baadae kutoweka na pikipiki,na kwamba boda boda hao nao wakifanikiwa kumkamata kibaka wa pikipiki umchoma moto kama walivyofanya kwa kijana huyu.
Mashuhuda wa Tukio hilo Wakiwa Eneo la Tukio
Baadhi ya wananachi wa Kata ya Mkundi wakimshangaa Kibaka huyo ambaye alichomwa moto akidaiwa kuiba pikipiki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni