Jumanne, 19 Mei 2015

MAJAMBAZI SUGU WAKAMATWA MCHANA HUU JIJINI DAR WAKITAKA KUIBA BENKI YA NMB

Majambazi hao wakiwa wametiwa pingu baada ya kukamatwa na jeshi laPolisi jijini Dar. 
Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio hilo. 
Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar es Salaam.Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo. Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni