Jumamosi, 13 Juni 2015

KENYA YATISHWA NA SHAMBULIZI LA ALSHAABAB MWEZI WA RAMADHAN

Serikali ya Kenya imeanzisha operesheni kukabili tishio la kigaidi wakati wa mfungo wa kiislamu wa Ramadhan.
Serikali ya Kenya imeanzisha operesheni kukabili tishio la kigaidi wakati wa mfungo wa kiislamu wa Ramadhan.
Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya, Joseph Boinet amesema japo sio wajibu wa Kenya kuweka doria na kulinda usalama ndani ya kambi imewalazimu kuchukua hatua kali kudhibiti utovu wa usalama kufuatia habari za kijasusi zilizodai kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wanatumia kambi hiyo ya wakimbizi kubwa zaidi nchini Kenya kupanga mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.
Bwana Boinet alisema hali ya usalama itaimarishwa vilivyo kufuatia vyanzo vinayoaminika kudai kuwa kundi hilo la Jihad linapanga kutekeleza mashambulizi wakati wa mfungo wa dini ya kiislamu wa Ramadhan.

''Wanataka kuvuruga amani wakati wa kipindi hiki cha dua takakatifu kwa wakenya wasio na hatia kwa kutekeleza mashambulizi na mauaji, lakini tumechukua tayadhari kubwa.''
 
Kenya inalaumu idadi kubwa ya wakimbizi nchini kwa utovu wa usalama
''Tumeimarisha usalama katika taasisi za umma ,vyombo vya usalama, taasisi za mafunzo, makanisa, masoko na maduka makubwa hasa mjini Nairobi, Mombasa and Kaskazini kwa Kenya''
'' Inaumiza sana kuwa wakimbizi ambao tumewapokea katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya wamegeuka na kuanza kushiriki uhalifu na hata kuumiza wenyeji wao.''
Inspekta huyo mkuu alisema kuwa tahadhari hiyo inafuatia vyanzo kamilifu vya kijasusi.
''Sio wajibu wetu kulinda usalama ndani ya kambi lakini sasa imetubidi kuwa waangalifu zaidi kujua nani anaingia ndani ya kambi hizo na ni nani anayetoka humo'' aliongeza Boinnet.
Amesema kuwa serikali ya Kenya imeimarisha uwezo wake wa kupambana na shambulizi lolote la kigaidi ikiwemo kudukua mawasiliano yao kupitia njia ya mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp.
Serikali ya Kenya imekuwa ikilaumu kuwepo kwa wakimbizi wengi wenye asili ya Somalia ndani ya mipaka yake kwa utovu wa usalama.
Mapema mwezi uliopita Naibu Rais wa Kenya bwana William Ruto alitangaza kuwa serikali ya Kenya ingefunga kambi hizo za wakimbizi katika kipindi cha siku 100.
Hatua hiyo iliibua taharuki kubwa miongoni mwa mashirika ya kimataifa ambayo yanashughulikia wakimbizi mbali na washirika wa Kenya kimataifa.
Hatimaye kauli hiyo ilifutiliwa mbali japo Kenya inaendelea kuinyoshea kidole cha lawama kwa kuzorota kwa usalama nchini.
Kundi la wapiganaji wa Al shabaab limekuwa likipigana vita na serikali ya Kenya likiitaka kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa jeshi la muungano wa Afrika AMISON linalolinda amani Somalia na kupambana na Al Shabaab

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni