Ijumaa, 5 Juni 2015

SUAREZ HATAKUTANA NA CHIELINI KESHO

Chiellini na Suarez baada ya tukio la kombe la dunia
Mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini hatakutana na mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez katika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya kupata jeraha.

Beki huyo wa Italy mwenye umri wa miaka 30 alitarajiwa kucheza dhidi ya Suarez ambaye alimng'ata katika michuano ya kombe la dunia mwaka jana.

Lakini mlinzi huyo muhimu atakosa mechi hiyo kutokana na jeraha la shavu la mguu na kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa Juventus.

Suarez kutoka Uruguay alipigwa marufuku ya miezi minne baada ya kumng'ata Chiellini katika bega lake katika kichuano hiyo iliofanyika Brazil.

Akizungumza mapema wiki hii ,Chiellini amesema kuwa angempa salam Suarez kwa kuwa hana ubaya naye

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni