Jumanne, 9 Februari 2016

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAZUKA TENA WILAYANI MVOMERO, MBUZI ZAIDI YA 70 ZAKATWA KATWA MAPANGA

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
 Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea uharibifu mkubwa wa kuuawa kwa  mbuzi zaidi ya 70. 

Jumatatu, 8 Februari 2016

WATU 2 WATOLEWA WAKIWA HAI TAIWAN

 Mwili
  Mwili wa mumewe mwanamke huyo huenda ulimkinga
Watu wawili wameokolewa wakiwa hai kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka kufuatia tetemeko la ardhi mjini Tainan, Taiwan.
Wa kwanza alikuwa mwanamke ambaye maafisa wanasema alipatikana chini ya mwili wa mumewe. Mwili wa mtoto wao wa umri wa miaka miwili ulipatikana karibu nao.
Muda mfupi baadaye, mwanamume mmoja pia alipatikana akiwa hai, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

IPO DALILI YA UHAI KATIKA MGODI ULIOPOROMOKA AFRIKA KUSINI

Jamaa za wachimbaji mgodi wa Lily Mine Afrika Kusini
Kuna dalili ya uhai kutoka katika mgodi wa dhahabu kufuatia ajali wiki iliyopita, ambapo watu watatu walifunikwa, waokoaji anasema.
Wachimbaji mgodi watatu wamekwama katika chumba cha taa, baada ya mgodi huo kuporomoka kufuatia kisa ambapo jumba moja lililoko karibu na mgodi huo lilipoporomokea mgodi huo siku ya ijumaa.
Kundi la waokoaji linasema kuwa walisikia mlio wa ukuta ambayo huwa ni ishara ya mawasiliano kati ya wachimba mgodi wakiwa hatarini.
Ishara hiyo ya mawasiliano imeinua matumaini ya wenye mgodi huo kuwa wachimbaji mgodi walioko ardhini wangali hai.
Wafanyakazi zaidi ya 70 wa mgodi huo walifanikiwa kutoka kutoka chini ya ardhi kwa kutumia njia maalum ya dharura baada ya ajali hiyo kutokea Ijumaa katika Lily Mine karibu na mji wa kaskazini mashariki wa Barberton .
Ajali hiyo ilisababishwa na jumba lililoporomokea mgodi huo na kusababisha tani kadhaa za kifusi kuharibu mgodi huo na kufunikia wafanyikazi ardhini

Jumatano, 3 Februari 2016

SIMU ZA SAMARTPHONE SI SALAMA KIVILE ZINAWEZA KUFUATILIWA KIRAHISI

Utafiti umebaini kuwa betri za simu za android zinawezakutumika kufuatilia watumizi
Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.
Uchnguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake.
Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia mbali.
Simu za kisasa ''Smartphone'' hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani ina changamoto tele za kung'amua masafa.
Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubainishwa na ''alogarithm'' muundo msingi wa simu yenyewe.
Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu.
‘’Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ‘’
Jopo hilo linajumuisha Yan Michalevsky, Dan Boneh na Aaron Schulman kutoka idara ya sayansi ya tarakilishi katika chuo kikuu cha Standford pamoja na Gabi Nakibly kutoka kwa kampuni ya Rafael walioandika matokeo ya utafiti wao.
 
Utafiti umebaini kuwa betri za simu za android zinawezakutumika kufuatilia watumizi
‘’Tuna ruhusa ya kuunganisha mtandao na upatikanaji wa nguvu yake.’’
‘’Hizi ni ruhusa za kawaida kwa mfumo huo na inawezekano wa kutoleta huduma kwa upande wa mwathiriwa.
Kuna mifumo 179 ambazo zinapatikana kwenye Anaroid, timu hiyo iliongezea.
Shughuli kama kusikiza muziki au kutumia mtandao wa kijamii inamaliza betri ya simu lakini hii inaweza kupunguzwa kutokana na ‘’kujifunza kwa mashine’’ripoti inasema.
Jaribio hilo lilifanyiwa kwa simu ambazo zinatumia mtandao wa 3G lakini haikuweza kupima nguvu kwa kuwa takwimu zinalindwa na kifaa hicho. BBC

Basi linalotumia umeme wa jua lazinduliwa Uganda

Basi linalotumia umeme wa jua
Basi linalotumia umeme wa nguvu za jua ambalo limedaiwa na watengezaji wake nchini Uganda kuwa la kwanza barani Afrika limeendeshwa hadharani.
Basi hilo la kielektroniki aina ya Kayoola linalomilikiwa na kampuni ya Kiira Motors lilionyeshwa katika uwanja wa Uganda mjini Kampala.