Jumanne, 13 Desemba 2016

Matuta barabarani yaua zaidi ya watu 33 Kenya Tanzania mpoo

Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya

Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya
Siku ya Jumamosi usiku gari linaloaminika kubeba kemikali ambayo inashika moto kwa haraka, lililokuwa safarini kutoka mjini Mombasa kwenda Kampala Uganda, lilihusika kwenye ajali mbaya karibu na mji wa Naivasha ulio Kaskazini Magharibu mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Jumla ya watu 33 waliangamia, wengi miili yao ikichomeka hadi kutoweza kutambuliwa, na wengine kadha wakipata majeraha.
Taarifa zinasema kwa gari hilo lenye nambari za usajili za Uganda lililokuwa limebeba kemikali liligonga tuta katika eneo la Karai karibu na Naivasha mwendo wa saa tatu unusu usiku wakati ambapo watu wa eneo hilo walikuwa wakifunga biashara zao.

Sokwe mvuta sigara awasili Kenya

Manno amekuwa akiishi nchini Iraq ambapo amekuwa akivuta sigara alizokuwa akipewa na wageni

Manno amekuwa akiishi nchini Iraq ambapo amekuwa akivuta sigara alizokuwa akipewa na wageni 
 
Baada ya kutengenishwa na mamake muda mfupi baada ya kuzaliwa, sokwe Manno alisafirishwa hadi nchini Iraq ambapo aliishi akivuta sigara alizokuwa akipewa na wageni huku akipigwa picha na wageni waliokuwa wakimtembelea.
Sokwe huyo mwenye umri wa miaka minne pia angevalishwa nguo kama mtoto na kupewa vinywaji na pipi

Grace Mugabe katika mzozo wa pete ghali ya almasi

Grace Mugabe

  Grace Mugabe
Gazeti la Zimbawe Independent la nchini Zimbabwe, leo hii limechapisha ripoti kuwa mke wa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, Grace Mugabe anashtakiwa kutokana agizo aliloweka kwa pete ghali zaidi ya almasi.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa Bi Mugabe alikuwa amesema kuwa mmewe alikuwa anataka kununua pete hiyo kuadhimisha miaka 20 ya ndoa yao.
Pete hiyo iliagizwa kutoka kwa muuzaji mjini Dubai kutoka kupitia kwa mfanyibiashara mmoja.
Kesi hiyo inaonekana kuwa ngumu na ina madai yanayohusu mmoja wa wanawe wa kiume na mlinzi wake.

Mbabe huko Gambia:Wanasheria wapinga Rais Yahya Jammeh kusalia madarakani

Jammeh aliingia madarakani mwaka 1996 kwa mapinduzi ya kijeshi

Muungano wa wanasheria nchini Gambia umesema kuwa kitendo cha Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kukataa matokeo ya kura zilizoonyesha kuwa ameshindwa katika uchaguzi uliopita ni kuisaliti nchi hiyo.
Muungano huo umeitisha maandamano kwa nchi nzima mpaka pale Jammeh aliyeangushwa katika uchaguzi huo akabidhi madaraka.
Hapo awali Jammeh alikubali kushindwa na kuahidi kuondoka madarakani lakini aliyakataa matokeo hayo siku ya Ijumaa.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kusafiri kuelekea Gambia siku ya Jumanne kwa lengo la kuzungumza na Jammeh ili kuachia madaraka.
Marekani imeonya kuwa nchi hiyo inapitia katika mazingira magumu huku baadhi ya viongozi wa kijeshi wakitajwa kumuunga mkono Jammeh.
Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika unatarajiwa kuwajumuisha Rais wa Nigeria, Ghana, Liberia na Siera Leone.
Kwa upande wake Baraza la usalama la umoja wa mataifa linajadili namna ya kutatua mgogoro huo leo.

Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya Ballon d'Or 2016

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa sasa wameshinda tuzo hii wakipokezana kwa miaka tisa mfululizo
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa sasa wameshinda tuzo hii wakipokezana kwa miaka tisa mfululizo
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.
Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.
Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.

Alhamisi, 8 Desemba 2016

Mwanamke mwenye kilo 500 kufanyiwa upasuaji India

Familia ya bi Abd El Aty inasema kuwa hajaondoka nyumbani kwa miaka 25.

Eman Ahmed Abd El Aty

Mwanamke mmoja raia wa Misri anayeaminiwa kuwa mtu mzito zaidi duniani akiwa na kilo 500, hivi karibuni atasafirishwa kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wake.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka 36, atasafirishwa kwa ndege ya kukodishwa kwenda mjini Mumbai, ambapo daktari Muffazal Lakdawala, anapanga kumfanyia upasuaji.
Ubalozi wa India mjini Cairo ulikuwa umemnyima visa kwa kuwa hakuweza kufika kwenye ubalozi huo yeye binafsi.
Hata hivyo hali ilibadilika baada ya daktari kutoka mji wa Mumbia kuindikia wizara ya mashauri ya Nje ya India kupitia mtandao wa Twitter.
Familia ya bi Abd El Aty inasema kuwa hajaondoka nyumbani kwa miaka 25.
Ikiwa madai kuhusu uzito wake ni ya ukweli basi atakuwa mtu mzito zaidi duniani aliye hai kwa kuwa Pauline Potter aliyekuwa na kilo 272 (ratili 600) mwaka 2010 wa Los Angeles Maekani ndiye anashikia rekosi ya Guinness

Utata mtupu hatima ya faru John

Rhino-216.jpg

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka maafisa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kutoa ufafanuzi kuhusu kuhamishwa kwa faru maarufu kwa jina la John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
Bw Majaliwa amewataka viongozi wa NCAA kuwasilisha kwake nyaraka zote zilizotumika katika kumuhamisha faru huyo kufikia Alhamisi.
Alisema ana taarifa kuwa faru huyo John alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti katika eneo Serengeti mnamo 17 Desemba, 2015.
"… mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200 ambapo mkapewa shilingi milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100 nyingine baadaye," alisema Bw Majaliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania, Bw Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa zozote kumhusu faru huyo zilizotolewa.
"Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,".
Bw Majaliwa pia alimsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili.
Kwa sasa, anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haiwezekani mtumishi awe anachunguzwa na Takukuru halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi? Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini," alisema.
Hifadhi ya Ngorongoro ndilo eneo pekee Tanzania ambapo faru wanapatikana kwa wingi porini, ndani ya kreta. 
Idadi ya  faru ni siri kutokana na sababu za kiusalama.

Jumanne, 6 Desemba 2016

Mzozo wazuka upya kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

Ramani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake.

Ramani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake.
Ramani mpya iliyotolewa na Tanzania ambayo inaonyesha kuwa inaamiliki nusu ya Ziwa linalozozaniwa la Malawi au Nyasa, imezua mzozo mpya na Malawi ambayo inasema kuwa ramani hiyo sahihi.
Ramani ya Tanzania inaonyesha kuwa eneo la Kaskazini Mashariki mwa ziwa hilo ni sehemu ya himaya yake, lakini Malawi nayo inadai kuwa eneo hilo lote ni lake.
Malawi imeomba Umoja wa Mataifa, Mungano wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa kuingilia kati.
  Msukosuko uliibuka mwaka 2011 wakati Malawi ilianza shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo.
Msukosuko uliibuka mwaka 2011 wakati Malawi ilianza shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Malawi, Rejoice Shumba amesema kuwa Malawi imeandika barua kwa mashirika makuu duniani ikiyataka kupuuzilia mbali ramani ya Tanzania.

Hii si mara ya kwanza Malawi imepinga ramani hiyo ya Tanzania.
Msukosuko uliibuka mwaka 2011 wakati Malawi ilianza shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo.
Serikali ya Tanzania bado haijatamka lolote kukuhusu suala hilo.

Nini hasa kinazozaniwa?

Fahari ya nchi na maswala ya kujiendeleza kiuchumi kwa Malawi na Tanzania kila mmoja akisimama kidete kusisitiza msimamo wake.
Kwa Tanzania, ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago Niassa.
Malawi na Tanzania ni koloni za zamani za Uingereza wakati Msumbiji ilikuwa chini ya ukoloni wa Ureno. Uingereza iliichukua Tanzania kutoka kwa Wajerumani baada ya wao kushindwa katika vita vya kwanza vya dunia.
Kando na ripoti za kuwepo mafuta na gesi katika ziwa hilo, ziwa lenyewe ni kivutio kikubwa cha watalii.
Malawi inasema inashauriana na Msumbiji kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika siku za baadaye ili kuzuia mzozo wa kidiplomasia .

Je hii ni mara ya kwanza kwa mzozo huu wa ziwa Malawi kutokea?

Hapana. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania.
Makubaliano hayo yaliafikiwa na Muungano wa Afrika na Tanzania ikaitikia ingawa shingo upande. Mzozo mpya kati ya nchi hizo ukaripotiwa tena kati ya mwaka 1967 na 1968.
Ulichipuka tena mwaka mwaka 2011, Malawi ilipotoa leseni ya kuchimba mafuta kwa kampuni ya British Surestream Petroleum Limited. Sehemu iliyotolewa kwa uchimbaji wa mafuta ni sehemu yenye mraba wa kilomita 20,000 sehemu ambayo Tanzania inasema ni yake.
Vyombo va habari viliripoti mwezi Julai mwaka 2012 kuwa mitumbwi ya wavuvi na ya watalii kutoka Malawi ilivuka na kuingia upande wa Tanzania
Tanzania nayo ikasema kuwa ingetafuta ushauri kutoka jamii ya kimataifa ikiwa nchi hizo hazingeweza kusuluhisha mzozo huo zenyewe.

Hofu ya hatua za kijeshi

Hofu ya mzozo kutokota na kuwa mbaya zaidi ilijitokeza mwaka 2012 wakati Tanzania iliposema kuwa ingelinda mipaka yake na kuzingatia sheria za kimataifa.

Ijumaa, 2 Desemba 2016

Rais wa Gambia kwa sasa Bw Jammeh "kukubali kushindwa"

Bwana Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994

 Bwana Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia anasema kuwa Rais Yahya Jammeh atakubali kushindwa kwenye uchaguzi wa Alhamis
Amesema kuwa si jambo la kawaida kwa rais wa Gambia kukubali kushindwa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.
Hata hivyo hakuna taarifa yoyote kutoka kwa bwana Jammeh ambaye amekuwa nyuma ya kiongozi wa upinzani Adama Barrow kwenye matoke ya kwanza
Bwana Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994 kufuatia mapinduzi ya kijeshi na sasa anawania muhula wa tano na amekuwa akitamba kuwa ataiongoza Gambia kwa miaka bilioni moja.

Alhamisi, 1 Desemba 2016

Mganga auawa kwa kutaka kubaka mteja


MGANGA wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55), mkazi wa kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani hapa ameuawa kwa kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.
Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) aliyekwenda kutibiwa ugumba kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio hilo ni la Novemba 29 mwaka huu, akisema lilitokea majira ya saa tano asubuhi.
Alisema Kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika jicho la kulia na kupigwa kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukulia sheria mkononi.
“Watu hao walijichukulia sheria mkononi baada ya mganga huyo kujaribu kumbaka mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze kupata mtoto”, alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya kumlewesha kwa dawa za kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga kelele na ndipo wananchi walipomvamia mganga huyo.