Jumatano, 1 Oktoba 2014

DODOMA HAKUKALIKI KWA WALIOSEMA NO


Wahudumu wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wajumbe waliopiga kura za siri kwa Sura ya 11 hadi 19 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma/Dar. Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika kuondoka Dodoma na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata kutoka kwa wenzao.
Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana jioni kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao wameamua kuondoka Dodoma.

Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya kupitisha Katiba inayopendekezwa.

WALIOKUNYWA TOGWA YENE SUMU WAFIKIA 340

Idadi ya watu waliolazwa hospitalini kwa kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Litapwasi, Kata ya Mpitimbi mkoani Ruvuma imeongezeka kutoka 270 hadi 340.Tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya watu kushiriki sherehe ya Kipaimara ambako walikula, kunywa pombe na togwa na baadaye wale waliokunywa togwa walianza kuumwa matumbo, kuhara na kutapika.
Hadi jana, watu 102 walikuwa bado wamelazwa katika Zahanati ya Lyangweni, Hospitali ya St. Joseph Peramiho na Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.Tayari watu watano wanashikiliwa na Polisi kwa upelelezi kuhusiana na tukio hilo, akiwamo Baba Mzazi wa mtoto Dickson aliyepata kipaimara, Enes Nungu (47).

KESI YA PAPAA MSOFE YAAHIRISHWA TENA


Papa Msofe (katikati) akishuka ngazi za Mahakama ya Kisutu baada ya kesi kuahirishwa.KESI ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Marijan Abubakar ‘Papa Msofe’ na mwenzake, Makongoro Joseph, imetajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kuahirishwa hadi Oktoba 13 mwaka huu kutokana na uchunguzi kutokamilika.

Msofe na Makongoro wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Onesphory Kitoli. Kesi hiyo imetajwa chini ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa

Makongoro Joseph (kulia) akisalimiana na mmoja wa wapambe wake.

Watuhumiwa pamoja na wapambe wao wakitoka mahakamani.

POLISI ACHUNGUZWA NA POLISI KISA KUTOROSHA DENT


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Moita Koka

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linachunguza tukio la askari wake (jina tunalo), iwapo alimtorosha na kumweka kinyumba mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Okaoni, wilayani Moshi Vijijini.


Askari huyo anatuhumiwa kumrubuni mwanafunzi huyo kuwa atamnunulia magauni mawili, blauzi mbili, sketi mbili pamoja na kiasi cha Sh 100,000.

Pamoja na kumtorosha mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, askari huyo na mwanafunzi, walipata ajali ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kutoka mjini Moshi kwenda Kibosho, Septemba 27 majira ya saa 9 alasiri na kulazwa hospitali ya KCMC na baadaye Kibosho Hospitali.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Moita Koka alithibitisha kupata taarifa za askari huyo na tuhuma dhidi yake na kuongeza kwamba maofisa wake wameanza kuchunguza tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa pale itakapothibitika.

“Hata mimi nasikia taarifa hizo za askari kumtorosha mwanafunzi na kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini hilo siwezi kulizungumzia maana halijathibitika, nimetuma maofisa wangu wachunguze wakinipa taarifa nitatoa,” alisema.

Aidha, Kamanda Koka alisema taarifa alizonazo ni juu ya kupata ajali kwa askari wake akiwa amembeba msichana, lakini hajapewa taarifa kama msichana huyo ndiye mwanafunzi anayezungumziwa na kama kweli wana mahusiano ya kimapenzi ama la.

“Kwa ujumla hili tukio hasa upande wa mapenzi siwezi kulizungumzia, ninachofahamu na ambacho nimekitolea maelekezo ni kutaka kupewa taarifa za ajali inayozungumziwa... lakini hili la mahusiano nalo nimetaka nipewa taarifa zake, ikibainika sheria itachukua mkondo wake,” alisema.

Kwa upande wake, diwani wa kata ya Okaoni na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini, Moris Makoi, alithibitisha taarifa za askari kumtorosha mwanafunzi huyo na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi.

Makoi alisema askari na mwanafunzi huyo pia walipata ajali eneo la Memorial barabara kuu ya Moshi/Arusha wakati wawili hao wakirejea Kibosho kutoka Moshi mjini walikokuwa wamejificha.

Naye mwanafunzi huyo, akiwa katika wodi namba tano hospitali ya Kibosho, alikiri kupewa ahadi ya kununuliwa nguo na Sh 100,000 ambazo hakupewa.

Alisema, baada ya kufika mjini Moshi alikwenda kununuliwa vitu hivyo na kwenda nyumba ya kufikia wageni ambako walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wakati wakirejea Kibosho wakiwa na pikipiki hiyo walipata ajali na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

“Wakati tunatoka mjini tulipata ajali na nilipoteza fahamu na majira ya usiku nilijikuta nimelazwa Hospitali ya KCMC na siku iliyofuata yule askari alikuja na kunichukua na kunirejesha nyumbani,” alisema.

Hata hivyo, mwanafunzi huyo alisema baada ya kufika nyumbani maumivu yaliendelea kuwa makali na kuamua kupelekwa katika hospitali ya Kibosho kuendelea na matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Kibosho, Erin Mmassele alikiri kumpokea mwanafunzi hayo na kuongeza kuwa anaendelea vizuri licha ya kuwa na majeraha miguuni.

EBOLA YABISHA HODI MAREKANI

 
Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas. Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.

WANAJESHI WA ISRAEL WAJIUA



Utawala wa Kizayuni wa Israel umeanza uchunguzi kuhusiana na vifo vya wanajeshi watatu wa utawala huo walioamua kujiua baada ya kurejea kwenye vita kati ya utawala huo na Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Ghaza.

Polisi ya Jeshi la utawala wa Israel imetangaza kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa wanajeshi hao walijiua kutokana na matatizo ya kisaikolojia yaliyosababishwa na ushiriki wao kwenye vita vya Ghaza.

Taarifa zinasema kuwa, wanajeshi hao wa Israel waliamua kujiua kwa kujifyatulia risasi na kwamba silaha walizotumia zilipatikana zikiwa pembezoni mwa miili yao. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanajeshi wawili kati ya watatu walijiua kwenye kambi ya kijeshi iliyoko karibu na mpaka wa Ukanda wa Ghaza.

Nalo gazeti la Maariv linalochapishwa huko Israel limemnukuu mmoja kati ya maafisa wa ngazi za juu wa utawala wa Israel katika hospitali ya wagonjwa wa akili akisema kuwa, jumla ya wanajeshi wanane wa Israel walijiua mwaka jana.

Afisa huyo mwandamizi wa jeshi amesema kuwa, jeshi la Israel halitangazi takwimu za wanajeshi wake wanaojiua kutokana na matatizo ya kiakili jambo ambalo wachunguzi wa mambo wanadhani ni  kuogopa lisipunguze morali wa vijana kujiunga na jeshi hilo.

SIKU YA MOYO DUNIANI: UGONJWA WA MOYO UNA TIBA

http://www.corazoncalderon.com/images_1/heart_entrada.gif NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM
MAISHA ya vijana wengi wa Kitanzania yapo hatarini kutokana na unywaji pombe na uvutaji sigara kupita kiasi, unaotajwa kuwa miongoni mwa sababu za kupatwa na ugonjwa wa moyo.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Robert Mvungi, alipozungumza na waandishi wa habari katika Siku ya Moyo Duniani iliyoadhimishwa kidunia jana.

Dk. Mvungi alisema wagonjwa wa moyo wanaofika kupata tiba katika hospitali hiyo ni wastani wa watu 20,000 kwa mwaka na asilimia kubwa kati yao ni vijana.



Hospitali ya Muhimbili
Alisema hali hiyo inachangiwa na mtindo wa maisha ambao wengi wao wamekuwa wakiishi kwa kunywa pombe kupita kiasi, uvutaji wa sigara, kula vyakula vyenye mafuta ya wanyama kwa wingi pamoja na kutokufanya mazoezi.

“Tumekuwa tukipokea watu 20,000 kwa mwaka hapa Muhimbili ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kati yao idadi kubwa huwa ni vijana,” alisema Dk. Mvungi.

Kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa, Dk. Mvungi kupitia Kitengo cha Moyo wameamua kuhamasisha jamii kula vyakula ambavyo havina athari kwao na kuepukana na tabia ya kutokufanya mazoezi ili kuondoa uwezekano wa kupata ugonjwa huo.

“Huu ni ugonjwa hatari iwapo watu hatutachukua tahadhari, kwa sababu kila mwaka takribani watu milioni 17.3 duniani wamekuwa wakifariki dunia kutokana na kuugua ugonjwa huo,” alisema.

Septemba 29 kila mwaka, dunia nzima huadhimisha Siku ya Ugonjwa wa Moyo ambayo huambatana na kaulimbiu mbalimbali kwa lengo la kuielimisha jamii kujua na kufuatilia undani wake.

Kwa upande wake, daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Muhimbili, Dk. Delila Kimambo, alisema maadhimisho kwa mwaka huu yamepewa kaulimbiu isemayo ‘Jenga afya ya moyo, kazini, majumbani na michezoni’, ikilenga kuhamasisha jamii kujenga mazingira mazuri katika kila eneo kwa kukwepa mambo ambayo yanaweza kusababisha kuugua ugonjwa huo.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa ugonjwa wa moyo husababisha vifo vya watu milioni 17.3 kila mwaka.

Ugonjwa huo ni wa pili duniani baada ya malaria unaongoza kwa kusababisha vifo vya watu.

SABABU ZA UGONJWA WA MOYO
Mienendo mibovu ya maisha ikiwamo uvutaji sigara, ulevi, ukosefu wa mazoezi ya mwili na chakula bora kwa kiasi kubwa vinachangia ongezeko la vifo vitokanavyo na ugonjwa huo nchini.

Wataalamu wa afya wanataja sababu nyingine kuwa ni umri, jinsia, historia ya familia, shinikizo la damu, kisukari, msongo wa mawazo na uchafu.

Takribani asilimia 80 ya vifo vya mapema vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vinaweza kuzuilika kwa kuepuka sababu hizo hatarishi.

TAFITI
Utafiti uliofanyika mwaka 2012 na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na WHO, unaonyesha kuwa asilimia 26 ya Watanzania wanakabiliwa na ugonjwa wa moyo huku asilimia 20 kati yao wakiwa wanawake.

Taarifa za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 92.6 ya Watanzania wenye ugonjwa huo hawapo kwenye matibabu licha ya kutambua kuwa wanaugua.

WHO inaeleza kuwa takriban asilimia 40 ya watu wazima katika Bara la Afrika wanaugua ugonjwa huo.

JOHANNESBURG JIJI LENYE PANYA HATARI

Panya hawa wana uwezo wa kula watoto
                   
Mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ni mmoja wa miji inayokua kwa kasi barani Afrika, lakini mji huo unakabiliwa na tatizo la kuvamiwa na panya walionona. Panya hao ambao wana uwezo wa kuwatafuna watoto wadogo majumbani na wengine kufariki dunia.

Maafisa wa halmashauri ya jiji la Johannesburg sasa wamezidisha juhudi ya kupambana na tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda mrefu.

KINANA AENDA MKINGA KWA BAISKELI

01Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi mara baada ya kuwasili katika kata ya Mng’aro Lushoto mara baada ya kushuka milima ya Usambara huku akiendesha Baiskeli pamoja na Nape Nnauye na wananchi wengine wakati msafara wake ukielekea jimboni Mkinga wilaya ya Mkinga, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya mkoa wa Tanga akikagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, Akiongozana na Nape Nnauye.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKINGA TANGA)1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionoza wananchi wakati akishuka milima ya Usambara kwa kutumia baiskeli pamoja na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na wananchi wengine.
2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza wananchi katika msafara wake.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakiendelea na safari pamoja na wananchi.4Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwasili kwa baiskeli katika kata ya Mng’aro Lushoto.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga makofi na Mkuu wa wilaya ya LushotoMhe. Majid Hemed Mwanga kulia wakipiga makofi huku mwadishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo akifurahia mara baada ya kuwasili katika kata ya Mng’aro wilayani Lushoto

BARCELONA HOI KWA PSG

Timu ya Barcelona jana ilionja joto ya jiwe baada ya kukubali kichapo cha goli 3 kwa 2 kutoka kwa timu ya Paris Saint Geman (PSG) katika mashindano ya UEFA 2014. Wafungaji walikuwa David Luiz (PSG) 10'; Lionel Messi (FCB) 11'; Marco Verratti (PSG) 26'; Blaise Matuidi (PSG) 54'; Neymar (FCB) 56'

Mchezaji wa PSG David Luis namba 32 akishangilia bao kwa staili ya aina yake



Mchezaji wa PSG David Luis (kulia)akiwa katika harakati za kufunga goli



Angalia video ya Barca vs PSG


Mchezaji wa PSG David Luis jezi namba 32 akishangilia bao
Wachezaji wa PSG wakishangilia bao

Mchezaji wa Barca akifunga bao

Lionel Messi wa Barca akishangilia bao