Jumatatu, 22 Desemba 2014

MAMA AKUTWA AKILISHA PANYA WAKE

KIFO CHA AISHA MADINDA WALIOKUWA NAYE WASAKWA

Kimenuka! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake. 
 
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, zilidai kwamba jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana

Ijumaa, 12 Desemba 2014

ALBINO BADO WANAISHI KWA MASHAKA TANZANIA

Kampenzi kubwa imezinduliwa nchini Tanzania, ikiongozwa na Raisi Jakaya Kikwete, kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo imekuwa na matukio mengi ya mauaji ya albino kwa imani za kishirikina huku wahusika wakiamini kwamba viungo vya walemavu hao vinaweza kuwapatia utajiri.

Pesa itakayokusanywa kutokana na kampeni hiyo, itatumika katika elimu kwa umma .
Mwandishi wa BBC Salim kikeke anaarifu kutoka mjini Mwanza kaskazini mashariki mwa Tanzania.

LOWASSA ANGURUMA ARUSHA

Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa akihutubia wananchi wa Mto wa Mbu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa eneo la Migombani, Mto wa Mbu jijini Arusha jana

PUNDA WAMPELEKEA KENYATTA UJUMBE MZITO

Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa jiji la Nairobi baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.
 Baadhi ya wananchi walishangaa Punda walikuwa wanafanya nini mjini kumbe wanaharakati ndio waliowaleta huko kuonyesha kuchoshwa kwao na kuzorota kwa usalama nchini humo.
 Kauli mbiu hio ilitumiwa mashambulizi yalipofanywa dhidi ya wakenya mjini Mandera Kaskazini mwa Kenya ambapo wanaharakati walipiga kambi katika ofisi ya Rais wiki kadhaa zilizopita kulalamikia ukosefu wa usalama.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.
Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori hilo alisema kuwa alilipwa na mtu fulani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.
Polisi wamesema wanachunguza kujua nani waliofanya kazi hiyo.
Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema mwanaharakati mmoja huku akiwasukuma Punda hao kutoka kwenye Lori.

Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.

WAKUU WA MIKOA WAMJULIA HALI RAIS PROF KIKWETE

Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa mikoa waliowawakilisha wenzao kwenda ikulu leo kumjulia hali na kumpa pole kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita katika hospitali ya Johns Hopkins ya  nchini Marekani hivi karibuni.(picha na Freddy Maro)

Alhamisi, 11 Desemba 2014

VURUGU ZA WAKULIMA NA WAFUGAJI DUMILA MOROGORO

polisi wakiwa kazini
Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  wananchi wa Dumila na  Mbigiri wilayani Kilosa mkoani Morogoro  baada ya kufunga barabara ya Morogoro Dodoma kwa kutumia mawe na kuchoma matairi barabarani katika eneo la dumila na  kusababisha abiria wanaotumia barabara ya Morogoro -Dodoma kukosa mawasiliano kwa zaidi ya masaa sita.
Waandishi wa Malunde1 blog wameshuhudia wananchi hao wakifunga barabara kwa mawe na matairi huku wengine wakionekana na mapanga ambapo wamesema wanalalamikia viongozi wa serikali ya kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kufumbia macho mgogoro wa ardhi na kushindwa kuwachukulia hatua wafugaji wanaowazuia wakulima wasilime katika eneo la Mbigiri.
Vurugu hizo zilidumu kwa muda mrefu na juhudi za kudhibiti wakulima hao zimechukua muda baada ya askari wachache wa kituo cha Dumila kuonekana kuzidiwa nguvu ambapo baadhi ya wakulima wengine  wameonekana wakivamia wakuvunja nyumba za wageni zinazomilikiwa na wafugaji na kupora magodoro na vitu mbalimbali ambapo baadae  vikosi vya jeshi la polisi viliongezwa na kufanikiwa kudhibiti  baadhi ya watuhumiwa na kufungua barabara.




Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema chanzo cha vurugu hizo ni wazee zaidi ya kumi walizuiwa kulima katika mashamba yao mbigiri ambapo walipelekeka malalamiko yao kwa afisa tarafa ambapo wakiwa ofisini kundi la vijana walifika na kufunga ofisi wazee hao pamoja na afisa tarafa hadi walipofika na koOkolewa na jeshi la polisi na katika tukio hilo watu 20 wanashikiliwa  na jeshi la polisi.



Afisa tarafa na wazee walifungiwa ndani wakizungumzia tukio hilo wamesema kuna mgogoro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji na upo katika ngazi za juu huku wakieleza kusikitishwa na hatua za kufunga barabara na kuomba serikali kuingilia kati kutatua mgogoro wa ardhi uliopo.









Hata hivyo katika hatua nyingine Tunaambiwa Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishie Kijiji cha Mketeni wilayani Kilosa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.

Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya wafugaji wa eneo hilo.

Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma matairi.

Kufuatia hali hiyo polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji eneo hilo na kufanya uharibifu.

Majeruhi katika vurugu hizo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

TIB KUTOA MIKOPO KWA VIJANA KUPITIA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI

Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, (NEEC), na TIB Development bank, wametialiana saini makubaliano ambayo yatatoa fursa kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati kupata fursa ya mikopo kwa nia ya kujiajiri wenyewe.
Katika makubaliano hayo TIB itatoa mikopo hiyo ambapo kwa kuanzia kiasi cha shilingi bilioni 1 kimetengwa kwa ajili ya mpango huo utakaoratibiwa na NEEC ambayo itakuwa na jukumu la kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kusaidia namna ya kutayarisha andiko, (Proposal), la miradi kwa nia ya kuomba mikopo.
Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya taasisi hizo mbili, mikoipo hiyo itatolewa Tanzania Bara na inalenga kusaidia miradi ya kilimo, uzalishaji, biashara na huduma kwa lengo la kuwawezesha vijana katika harakati za kukuza uchumi wa taifa.
Taarifa hiyo pia ilifafanua kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa vyama vya ushirika (Cooperatives), na mtu mmoja mmoja (Individual), Viwango vya mikopo itakayotolewa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni shilingi zisizozidi milioni 200 kwa SMEs na washirika au ushirika, wakati shilingi zisizozidi milioni 50 kwa kijana mhitimu wa chuo kikuu mjasiriamali ambaye awe amefaulu mafunzo hayo ya kuwaandaa wajasiriamali yatakayokuwa yakitolewa na NEEC.
Picha ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Dkt. Anacleti Kashuliza, (Kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Peter Noni, wakionyesha waandishi wa habari mikataba hiyo baada ya kuisaini.
Noni wa TIB, (Kulia) na Dkt. Kashuliza wa NEEC, wakibadilishana hati hizo baada ya kusaini
Katibu mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, NEEC, Dkt. Anacleti Kashuliza, (waliokaa kushoto) na mkurugenzi mtedaji wa benki ya maendeleo TIB, Peter Noni, wakisaini makubaliamo hayo. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni afisa wa sheria wa NEEC, Esther Barikie Mbaga, Mwenyekiti wa bodi ya NEEC, Omar Issa, mkurugenzi wa mfuko wa uwezeshaji wa TIB, Prisca V. Chang'a, na mwanasheria na katibu wa bodi ya TIB, Martha J.J.Maeda
"Vijana wasajili kampuni zao kwwnye mamlaka zinazohusika ili iwe rahisi kuaminiwa na benki" Peter Noni
"Kuwawezesha wananchi kiuchumi ndio njukumu letu kuu" Dkt. Anacleti Kashuliza
Shahidi upande wa TIB, ambaye ndiye mwanasheria wa benki hiyo, Martha J.J.Maeda, "akimwaga wino"
Afisa wa sheria wa NEEC, Esther Barikiel Mbaga, akithibitisha kwa kuweka saini yake kuwa makubaliano hayo ni ya kisheria na halali
Baadhi ya viongozi wa TIB, wakifurahia jambo
Picha ya pamoja ya waliohudhuria hafla hiyo

IDRIS RASHIS ATUA DAR

Idris akionekana ni mwenye furaha kubwa sana baada ya kuwasili nchini.
Mama Mzazi wa Idris Sultan akijiandaa kumpokea mwanae.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kati) akijadiliana jambo na Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan pamoja na aliekuwa mshiriki wa shindano hilo,Laveda katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa 2014, Idris Sultan, akizongwa na umati wa watu mashabiki wake huku akiwa na furaha baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Idris ameibuka kidedea na kunyakua taji hilo la Big Brother Africa 2014. Kushoto kwake ni Laveda aliekuwa mshiriki mweza wa Idris.
Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan, akizungumza wakati akihojiwa na waandishi wa habari, baada ya kuwasili nchini.

Jumapili, 7 Desemba 2014

RAIS ATEUA MKUU WA MKOA NA KUHAMISHA KIBAO

index
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.

Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Desemba,2014