Jumatatu, 21 Julai 2014

HALI YA KUTISHA!!! MIILI YA WATU ZAIDI YA 100 YAKAMATWA BUNJU USIKU

Miili ya watu zaidi ya mia moja imekamatwa kwenye machimbo ya kokoto Bunju. Tunaomba radhi kwa picha za kutisha.
 
 
Mmoja ya Kiungo cha Mguu

WAASI SUDAN KUSINI WATEKA MJI



Wanajeshi wa serikali ya Sudan kusini wapiga doria.
Waasi nchini Sudan kusini wanasema kuwa wameuteka mji muhimu wa Nasir katika jimbo la upper Nile.
Wanasema kuwa wameuteka mji huo baada ya kushambuliwa na vikosi vya serikali.
Jeshi la Sudan Kusini limesema kuwa vita vinaendelea katika mji huo,ambao waasi wamekuwa wakishambulia tangu siku ya jumamosi.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa huenda huo ukawa mwisho wa makubaliano ya kusitisha vita yaliotiwa sahihi mnamo mwezi May.
Mji wa Nasir ulikuwa makao makuu ya mda ya ya kiongozi wa waasi Riek Machar ,ambaye alihudumu kama makamu wa rais wa Sudan kusini kabla ya kutofautiana na rais Salva Kiir.

JK AKAGUA SHAMBA LA KAHAWA MBINGA

D92A6133
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.

WANNE WAUAWA MOMBASA



Moja kati ya matukio ya mauaji yaliyowahi kutokea Mombasa
Watu wenye bunduki waliokuwa kwenye pikipiki wamewaua takriban watu wanne katika mji ulioko pwani ya Kenya Mombasa.
Polisi inasema watu hao walikuwa wakifyatua ovyo risasi kwa wapita njia.

Mji huo wa Bandari umeshuhudia ghasia katika miezi ya hivi karibuni huku kukiwepo mashambulio ya mabomu na ufyetuaji wa risasi ambayo wanamgambo wa alshabaab kutoka Somalia wanatuhumiwa kuyatekeleza.

BASI LA AM COACH LAPATA AJALI MSWA NA KUJERUHI SITA


Basi la AM Coach likiwa eneo la tukio katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu
Habari za hivi punde zilizoufikia mtandao huu wa blog ni kwamba Basi la AM COACH lililokuwa linatoka Meatu mkoani Simiyu kwenda Mwanza limepinduka katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Kwa mujibu wa habari kutoka eneo la tukio watu sita wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwani hali za ni mbaya.
 
Miongoni mwa waliojeruhiwa yumo mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Jumapili, 20 Julai 2014

WEMA SEPETU AVALISHWA PETE YA UCHUMBA NA DAIMONDI

Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) akionyesha pete aliyovishwa na Diamond.

Wema Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana akirandaranda na pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa siri kubwa,Baada ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao wamefunga ndoa ya siri.

MWANAMUZIKI MAARUFU WA FM ACADEMIA AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki mwenye sauti tamu wa bendi ya FM Academia aka Wazee Wa Ngwasuma aitwae Digital amefariki dunia muda mfupi alipokuwa amelazwa katika hospital ya Muhimbili jijini Dar, awali tangu wiki iliyopita alikimbizwa hospitali ya Mwananyamala baada ya kuzidiwa na maradhi, na chanzo cha kifo chake hakijaelezwa! poleni FM Academia, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu.
Kwa habari zaidi nitaendelea kuwajuza zaidi, Mungu amlaze mahala pema peponi ameni

IDADI MPYAYA MIILI ILIYOPATIKANA KATIKA AJALI YA NDEGE YA AIR MALAYSIA

malay2
Wafanyakazi wa dharura wa Ukraine wanasema wamekuta miili ya watu 196 katika eneo ilipotokea ajali ya ndege yaMalaysia ya MH17. Jumla ya watu 298 walikuwemo ndani ya ndege hiyo wakati iliporipotiwa kutunguliwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi la ukanda wa Donesk siku ya Alhamisi. Nchi za Magharibi zimekosoa vikwazo vinavyowekwa katika eneo ilipotokea ajali na kuitaka serikali ya Urusi kuweka shinikizo kwa serikali ya Ukraine kuruhusu kuingia katika eneo hilo.

malay
Waangalizi wa kimataifa wanatarajia kutembelea eneo hilo tena hapo baadae.
Serikali zote Ukraine na Urusi zimetuhumiana kwa kuitungua ndege hiyo iliyokuwa ikiruka kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur.

BENKI YA FBME YAFUNGWA?


Benki Kuu ya Tanzania inapenda kukanusha habari zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa kesho Jumatatu Benki ya FBME itafungwa na shughuli zote za benki hiyo zitakuwa chini ya Benki Kuu.
Habari hizi si za kweli na kwamba benki hiyo haipo chini ya usimamizi wa Benki Kuu na itaendelea kutoa huduma kama kawaida.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI, BENKI KUU YA TANZANIA.

Jumatano, 16 Julai 2014

MSHUKIWA WA MABOMU YA BOKO HARAM AREJESHWA NYUMBANI


Aminu Sadiq Ogwuche aliletwa mjini Abuja kutoka Sudan Jumanne
Mshukiwa wa mashambulizi mawili ya mabomu mjini Abuja nchini Nigeria, ambayo yaliwaua watu 75 , amerejeshwa nchini Nigeria kutoka Sudan.

Boko Haram ni nani?

  • Boko Haram lilibuniwa mwaka 2002.
  • Nia na lengo la kundi hilo ilikuwa kupinga elimu ya kimagharibi.
  • Lilianza kufanya mashambulizi mwaka 2009
  • Maelfu wameuawa hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
  • Kundi hilo pia limeshambulia makao makuu ya UN mjini Abuja
  • Takriban watu milioni 3 wameathirika
  • Kundi hilo lilitangazwa kuwa la kigaidi na Marekani mwaka 2013

Aminu Sadiq Ogwuche, alikamatwa mjini Khartoum mwezi Mei baada ya shirika la polisi wa kimataifa Interpol kutoa waranti ya kumkamata.
Anatuhumiwa kwa kupanga mashambulizi yaliyofanyika katika kituo cha basi mapema mwaka huu ambayo Boko Haram ilikiri kuyafanya.
Maelfu ya watu wameuawa nchini Nigeria mwaka huu peke kutokana na mashambulizi ya Boko Haram wakitaka kuruhusiwa kuunda jimbo lenye kufuata sheria za kiisilamu Kaskazini mwa nchi.