Jumanne, 15 Desemba 2015

WATANZANIA WASHAURIWA KUJIHUSISHA NA UFUGAJI WA SUNGURA ILI WAWEZE KUJIONGEZEA KIPATO


 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufugaji wa sungura unaweza ukawasaidia wakulima katika kujiongezea kipato kwa mbali na kuuza nyama yake lakini pia wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake,katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson,akiwaonesha waandishi moja ya sungura wanaopatikana katika shamba hilo, kulia ni Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange, katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
 Sehemu ya mabanda ya kufugia Sungura hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba akifafanua jambo kwa Wandishi wa habari  katika ziara ya mafunzo  kuhusu mradi  huo  katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
 Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii

WATANZANIA wameshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura ili waweze kujiongezea kipato kutokana na mnyama huyo kuwa na faida nyingi.


Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo jana katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoani Pwani.

Dickson alisema, ufugaji wa sungura unaweza utawanufaisha wakulima katika kujiongezea kipato  mbali na kuuza nyama yake wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake

“Tunawafundisha wakulima jinsi ya kufuga sungura ili waweze kunufaika, lakini wanaweza kujiuliza ni wapi wanaweza kuwauza wakishafikia hatua ya kuuzwa, sisi tunawapa soko kwa hiyo kikubwa kwa mkulima ni kufuga tu,” Dickson alisema.

Alisema kampuni yake ina mashamba ya sungura hivyo wanapoingia mkataba na wakulima wanaohitaji kufuga wanakubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuwatafutia masoko ambapo wao wenyewe wananunua sungura hao. 

Alisema mbali na faida ya kuuza nyama yake lakini pia wanaweza kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake.                                                                                  

Naye Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange alisema, kuna umuhimu wa kinamama  kutumia fursa ya ufugaji sungura ili kumudu kuwasomesha watoto wao badala ya kuwategemea waume zao.

Alisema licha ya kuwa sungura hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kuwafuga lakini amekuwa akihakikisha kuwa wanaishi katika mazingira mazuri ili waweze kumpa faida.

“Huu ufugaji kwa kuwa ni mpya watu, wengi wanaweza kujiuliza inakuwaje au masoko watapata wapi...lakini mimi nilipoanza kufuga niliingia mkataba na hii kampuni na wao walinipa masoko ina maana kwa kila sungura wa kilo nne nauza kwa Sh 40,000,” Nyange alisema.

Nyange alishauri wajasiriamali na hasa wanawake kujiingiza katika ufugaji huo ili waweze kufanya mambo yao mbalimbali bila kuwategemea akinababa ambao wakati mwingine wanakuwa na majukumu memgi.

Jumamosi, 12 Desemba 2015

MSAADA MKUBWA UNAHITAJIKA KWA DADA ELIZA ILI AWEZE KUFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI


 
Eliza Juma (30), mkazi wa Mtaa wa Mbwanga Manispaa ya
Dodoma anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa yeyote ataeguswa ili aweze
kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni ambao umekuwa ukiongezeka kila siku.
Akizunguma na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, alisema kuwa
uvimbe huo ambao umekuwa ukiongezeka kila siku umekuwa kikwazo kwake katika
kutekeleza majukumu yake ya kujipatia kipato.

WATUHUMIWA 40 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha waziri wa Sera, Bunge, Kazi ,Vijana,Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, na manaibu Waziri jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Jumanne, 24 Novemba 2015

MASHARTI YA KUSAFIRI NJE HAYA HAPA

Ofisi ya Rais imesambaza mwongozo unaoweka masharti ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kutimiza ili wapewe kibali, ikiwa ni mkakati wa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kudhibiti safari holela za nje.
Rais alitoa agizo hilo baada ya kikao baina yake na makatibu wa wizara kilichofanyika Ikulu siku chache baada ya kuapishwa, akisema ofisi yake ndiyo itakayotoa kibali kwa watumishi ambao wana safari za nje.
Kwa mujibu wa waraka huo, sharti la kwanza linalotakiwa kuzingatiwa na watumishi hao ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Pili, kwa mujibu wa mwongozo huo, maombi yawasilishwe kwa msajili wa hazina kabla ya kwenda kwa Katibu Mkuu Kiongozi ili aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wake na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.
Tatu, mtendaji mkuu wa shirika au taasisi apime maombi ya safari husika ili kuona kama yana tija na yana umuhimu wa kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kongozi, kabla ya kuwasilishwa kwa msajili wa hazina, kwa mujibu wa mwongozo huo.

Jumanne, 10 Novemba 2015

MAPIGANO YA JOGOO YAUA WATU 10

 
Vita vya jogoo vyasababisha vifo vya watu 10

Takriban watu 10 wamepigwa risasi na kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu jogoo yupi aliyeibuka mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico.

Miongoni mwa wale waliouawa ni ni mvulana mwenye umri wa miaka 12 aliyepigwa risasi katika mji wa Cuajinicuilapa.

Watu wengine 7 walijeruhiwa vibaya.

Uchunguzi wa awali uliashria kuwa mashabiki wa jogoo hizo mbili walitofautiana kuhusu ni yupi aliyeibuka mshindi.

Hata hivyo duru zinasema kuwa huenda ukumbi huo wa mapigano ya majimbi ulivamiwa na watu walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Hadi kufikia sasa,haijulikani iwapo magenge yanayoshamiri mjini Guerrero ndiyo yaliyotekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Mwaka uliopita wanafunzi 43 walitoweka katika mji wa Iguala na kuweka tatizo la magenge katika majimbo ya Mexico katika rubaa za kimataifa.

MKURUGENZI WA HABARI IKULU AFUNGASHA VIRAGO

  
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu (pichani) amemaliza mkataba wake na kuondoka huku akiwashukuru watendaji kwa muda wote aliokuwa nao wakimsaidia Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete.

Kuondoka kwake kunampa fursa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kuunda safu mpya ya Kurugenzi ya Mawasiliano. Salva aliteuliwa, kwa mara ya kwanza, na Rais Kikwete kushika wadhifa huo Septemba 17, 2007 na alimaliza mkataba wake Septemba 11, 2015 lakini aliongezewa hadi Novemba 10.

RAIS MAGUFULI KATIKA ZIARA YA GHAFLA MUHIMBILI.AMJULIA HALI HELEN KIJO BISIMBA

gu1
-Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Dkt.Helen Kijo Bisimba aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa katika ajali jana.
gu2
-Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Dkt.Helen Kijo Bisimba aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa katika ajali jana.
gu3
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakati alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo leo na kuwafariji wagonjwa.

Jumamosi, 17 Oktoba 2015

PICHA ZA AJALI YA CHOPA YA FILIKUNJOMBE














BURIANI DEO FILIKUNJOMBE




Deo Filikunjombe (1972 -2015)
Taifa limekumbwa na msiba mzito baada ya kuthibitika kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe (43) na watu wengine watatu kufariki dunia baada ya helikopta (chopa) waliyokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Ludewa mkoani Njombe kuanguka na kuwaka moto katika Mbuga ya Selous.

Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni rubani wa chopa hiyo, Kapteni William Silaa ambaye pia ni baba wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jerry Silaa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema jana kuwa Filikunjombe na watu wengine watatu waliokuwamo kwenye chopa hiyo wamepoteza maisha baada ya chopa waliyokuwa wakisafiria kuanguka na kuwaka moto.