MOROGORO.
MKAZI wa Kijiji cha Bwakila Chini, Kata ya Bwakila
Chini, Maloda Sitini amefariki dunia baada ya kuliwa na mamba tukio lililotokea
katikati ya mwezi uliopita katika Mto Mgeta, Wilaya ya Morogoro.
Diwani wa Kata ya Bwakila
Chini, Mohamed Pesa alisema kuwa marehemu alifikwa na kifo wakati akivuka Mto
Mgeta, Februari 13 mwaka huu na ghafla alikamatwa na mamba huyo aliyemshambulia
sehemu mbalimbali za mwili na baada ya kumzidi nguvu, alimzamisha majini kisha
kumwua na kumla.
Pesa alisema kuwa
ndugu wa karibu wa marehemu walimtafuta ndugu Sitini kwa siku 18 bila mafanikio na
walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kata hiyo.
Alisema kuwa uongozi wa kijiji ulibaini kaliwa na
mamba baada ya kuona mabaki ya vipande vya nguo alizokuwa amevaa marehemu na
ndipo ukawekwa mtego wa kumnasa mamba huyo. Diwani huyo alisema kuwa mamba huyo
alinaswa Machi 2 saa 4 usiku.
“Katika kata yangu kuna tukio la mamba mla watu
kuua mtu na mpango wa kumuua ulitimizwa baada ya kufahamika kuwa mtu mmoja
aliyetambulikwa kwa jina la Maloda Sitibi kufariki dunia kwa kuliwa na
mamba huyo.
"Kwa bahati mzuri,
ushirikiano wa uongozi wa Taasisi ya JUKUMU Society na wananchi walifanikiwa
kumuua kwa kutega mtego uliowezesha kumnasa mamba huyo," alisema
Pesa.
Pesa alisema baada ya
kuuawa, mamba huyo alipasuliwa na tumboni mwake alikutwa na mifupa mbalimbali
ya binadamu, nywele za kichwani na bangili.
Baba mzazi wa marehemu, Mzee Sitibi alichukua
mabaki hayo ya mifupa ya mwanawe na kwenda kuyazika.
Diwani huyo alitoa wito kwa wakazi wa kata hizo
wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa wakati wanakaribia ama kuvuka mito
mikubwa inayopita katika kata hiyo hasa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni