Boko Haram wazidi kumlaza macho Raisi Jonathan
Moyo
Kundi la wapiganaji la kiislam la Boko Haram,wamevamia shule
moja ya mafunzo ya kipolisi. Kituo hicho cha mafunzo kilichoko kwenye kitongoji
cha Gwoza kiko karibu na mpaka wa nchi ya Cameroon ambacho hufundisha maofisa wa
Polisi nchini Nigeria.
Kikundi hicha Boko Haram pia kinasemekana kuudhibiti mji wa jirani na Gwoza
uitwao Buni Yadi.
Nalo shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa
takwimu ya vifo vilivyosababishwa na kundi hilo kuua watu zaidi ya elfu kumi
mpaka sasa tangu walipoanzisha harakati za kutaka upande wa kaskazini mwa
Nigeria uwe chini ya utawala wa Kiislam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni