Ijumaa, 22 Agosti 2014

KIJANA ALIYETAPELI PIKIPIKI AUAWA KAHAMA

Haya twendeni vizuri sasa angalia huko kwako ana nguvu huyu mtu unaona  alivyokaaa
Baada ya kufikishwa hospital ya wilaya ya Kahama kwa matibabu ana baada ya wasamaria wema wakimsaidia nesi kumpeleka kwa dakitari kwa huduma .
Nesi nisaindieni jaamani nipo pekee yangu ndiyo maneno ya nesi anayosema na kumuweka katika kiti cha wangonjwa .
 Jamani muinueni huko tumuweke kwenye kiti kwa ajili ya huduma hospitali ya wilaya ya Kahama
jamani hajakaa vizuri mshikilieni vizuri kwanza
Kijana mmoja anayekadiriwa kwa na umri wa miaka 30-32 ambaye hajafahamika majina wala makazi yake ameuawa kwa kupigwa mawe, kisha kuchomwa moto na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, baada ya kumtuhumu kutapeli pikipiki.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa Nyihogo, eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

Mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa alikodisha Pikipiki hiyo zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la Maegesho ya Daladala na Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya hiyo.

Aidha Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya pikipiki, inadaiwa alimkamata maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi akiwa amemfunga kamba.

Baada ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo wakamuuliza mmiliki huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma Moto.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ni kweli tukio hilo limetoka jana majira ya asubuhi saa 5 kijana moja ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja alikuwa amekamatwa na mwanachi moja ambapo alikuwa ametoroka na pikipiki yake maeneo ya Nyahanga wilayani kahama .

Aidha kamanda Kamugisha alizidi kuelezea kuwa pamoja na tukio hilo kutokea kwa kijana huyo jeshi la polisi linawatafuta watu wote walifanya mauji hayo

MATUKIO KATIKA PICHA:



Hapa ni baadhi ya mwananchi wakijaribu kumtambua kijana huyo.
Twendeni sasa
Jamaani nakufa hayo ni maneno ya huyo kijana akisema kwa tabu sana

Haya kaa vizuri kaka umekwisha fika hapa hospitali
Haya twende sasa
CHANZO KIJUKUU BLOG

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni