Jumatano, 25 Februari 2015

WAKRISTO WANA HALI MBAYA SYRIA

Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State.
Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State.
Duru kutoka kwa jamii hiyo sasa inathibitisha kwamba zaidi ya raia 200 walitekwa nyara Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa kaskazini mwa Syria.
Wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake, watoto na wazee.
Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka.
Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye silaha.
Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristo hawa wa Syria ndio mwanzo unaanza kujitokeza.
 
Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka wanakoishi
Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristo kimetoa madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo.
Kimedokeza kuwa zaidi ya watu mia tatu hamsini wametekwa.
Huku hayo yakiarifiwa waumini wengine wa kikristo wameanza kukimbia vijiji vyao wakihofia kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State.
Na bado vita vinaendelea huku waislamu hao wakikabiliana na waasi wa kikurdi pamoja na washirika wao wa kikristo katika mji wa Hassaka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni