Askofu mkuu mstaafu wa mji wa Capetown na mshindi wa tuzo la Nobel
Desmond Tutu pamoja na mkewe wamemfungulia mashtaka ya uhalifu mjukuu
wao.
Katika taarifa kupitia wakfu wa Desmond na Leah Tutu
hawakutoa maelezo zaidi, lakini maafisa wa polisi wa Afrika kusini
wamesema kuwa wanachunguza kesi kuhusu uharibifu wa mali kwa makusudi. Mjukuu huyo ambaye anatuhumiwa kuwa mi mlevi alivunja vitu mbalimbali vya babu yake ikiwa ni pamoja na vikomb, sahani nk.Mjukuu huyo Ziyanda Palesa Tutu anatarajiwa kujisalimisha kwa polisi.
Wakfu huo umesema kuwa familia imeshangazwa na kitendo hicho na wanatumai kwamba wataliweka nyuma swala hilo hivi karibuni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni