Mwanamume huyo alikuwa akinywa pombe hapa Copenhagen, mji mkuu wa Denmark
Mkazi mmoja wa mji
wa Oslo anajutia aliyoyafanya akiwa amelewa mkesha wa Mwaka Mpya baada
ya kugundua kwamba alikuwa anadaiwa $2,220 (£1,640) sawa na shilingi za Kitanzania milioni 5 kwa kutumia teksi.
Mwanamume
huyo wa miaka 40 hivi alikuwa amesafiri kupitia mataifa matatu, kuanzia
Copenhagen nchini Denmark, akapitia Sweden, na kisha akafika Oslo
nchini Norway. Alipofika nyumbani, aliingia ndani na hakumlipa nauli dereva wa teksi. Dereva
huyo alijipata amekwama baada ya betri ya gari lake yake kuisha chaji
akiwa nje ya nyumba ya mwanamume huyo akisubiri atoke nje na pesa
amlipe. Aliamua kuwapigia simu polisi. Kupitia Twitter, polisi wa Olso wanasema walimkuta mwanamume huyo akiwa amelala fo fo fo kitandani na kumwamsha. Alikubali kulipa pesa alizokuwa anadaiwa. Mwanamume huyo hana historia ya kutekeleza uhalifu, kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Norway ya NRK. Safari hiyo ya kutoka Copenhagen hadi mtaa wa Abildso mjini Oslo ilikuwa ya umbali wa 600 km (maili 372). Huenda akafikiria kutumia ndege siku zijazo... Na dereva wa teksi? Gari jingine lilifika kumsaidia..
Hili ni fundisho kwa walevi kufanya maamuzi ya busara wakiwa wamelewa.
Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.
Taarifa
iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni
Covenant
Bank For Women (Tanzania) Limited,
Efatha Bank Limited,
Njombe Community
Bank Limited,
Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na
Meru Community Bank Limited.
BoT
imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha
56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na
41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu
ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki;
kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya
ufilisi.
“Kwa
mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na
Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya
Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe
04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.”
“Uamuzi
huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki
hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya
Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu huo
wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea
kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za
wateja wake.”
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea
kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta
uhimilivu katika sekta ya fedha.
Rais Donald Trump
amemshambulia msaidizi wake wa zamani wa Ikulu ya White house Steve
Bannon,kwamba alipoteza akili zake mara tu alipopoteza ajira yake.Trump
amefikia hatua hiyo kufuatia Bannon kunukuliwa na kitabu kipya
kilichopishwa akiwa anaelezea jinsi mtoto wa rais Trump alivyokutana kwa
siri na kundi la watu kutoka Urusi ili kupanga njama za uchaguzi.
Ndani
ya kitabu hicho kilichoandikwa na mwandishi wa habari Michael
Wolff,afisa huyo wa zamani wa ikulu ya Marekani,ameelezea namna ambavyo
Donald Trump mtoto,mwanaye rais Trump alivyopewa taarifa na Urusi
zilizolenga kummaliza kisiasa Bi Hillary Clinton ili yeye aweze
kushinda.
Hata hivyo kutokana na shutuma hizo ndani ya kitabu
hicho zilizopewa uzito na afisa huyo wa zamani wa ikulu ya white
house,rais Donald Trump amesema kuwa lolote la kuweza kumuathiri yeye
binafsi na urais wake pia,bali amesisitiza kuwa amegundua kuwa ofisa
huyo hakupoteza kazi yake tu lakini alipoteza akili zake pia.
''Steve alikuwa ofisa aliyekuwa akifanya kazi kwaajili
yangu,mara baada ya mimi kuteuliwa kuwania urais baada ya kuwabwaga
wagombea wengine 17,'' amesema Trump.
Amesema pia kuwa Steve
anafanyayote hayo kwa maslahi binafsi,akifikiri kuwa suala la ushindi si
rahisi kama ilivyokuwa katika ushindi wangu,hana lolote la kuweza
kufanya kuhusiana na historia ya ushindi wetu ambao ulipatikana kwa kura
za wanawake na wanaume waliokuwa wamesahaulika.
Steve Bannon, ni
afisa wa zamani wa rais Trump nayetajwa kuwa mtu muhimu na alibuni kauli
mbiu ya rais Trump Marekani kwanza yaani America first kabla kuacha
kazi mwezi August mwaka jana.
Suvarnabhumi ni uwanja wa ndege kubwa zaidi nchini Thailand
Familia moja kutoka Zimbabwe wamefanya uwanja wa ndege mjini Bangkok kuwa makazi yao kwa karibu miezi mitatu.
Kwa
mujibu ya ofisi ya uhamiaji wa Thailand, watoto wanne wenye umri chini
ya miaka 11 na watu wazima wanne walifika jijini Bangkok mwezi wa Mei,
lakini walikataa kurudi Zimbabwe kwa misingi ya usalama wao.
Taarifa
yao iliibuka baada ya mfanyakazi wa uwanja wa ndege huo alipoweka picha
katika mtandao wa kijamii wa Facebook, akimpatia mtoto wa kike
Mwafrika, zawadi ya Krismasi.
Picha hio,ambayo imefutwa sasa,
iliambatana na ujumbe wa Kanaruj Artt Pornsopit akisema kuwa familia
hiyo ilikuwa ikiishi katika jengo hili kwa miezi mitatu kwa sababu ya
"hali ya sintofahamu" nchini mwao. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamekuwa wakitoa msaada wa chakula kwa familia hio.
Msemaji wa ofisi ya uhamiaji Pol Col Cherngron
Rimphadee aliiambia BBC kuwa awali familia hiyo iliwasili nchini
Thailand kama watalii. Walijaribu kupanda ndege kutoka mjini Bangkok
mwezi Oktoba hadi mji wa Barcelona nchini Uhispania kwa kupitia Kieve
nchini Ukraine.
Lakini walikatiliwa kuingia katika ndege kwa sababu ya kukosa vibali vya kuingia Uhispania.
Pamoja
na hayo walishindwa kurudi tena na kuingia nchini Thailand sababu
kibali chao cha mwanzo cha kitalii kilichowakubalia miezi mitano
kilipitwa na wakati na ilibidi walipie faini kubwa. Familia hiyo imekataa kurudi Zimbabwe ikisema wanahofia usalama wao baada ya vurugu iliyotokea Novemba iliyomwondoa madarakani rais Mugabe aliyedumu kwa miaka 37.
Hata hivyo, kwa sasa hamna taharuki yeyote inayoendelea nchini
Zimbabwe, kwa baadhi nchini humo wameyashuku madai yao kuhofia usalama
wao.
Kwa mujibu wa Col Rimphahdee familia hiyo imewasilisha maombi
ya kuomba makazi kwa Umoja wa Mataifa, wakati wakihudumiwa na
wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi.
Aliimabia idhaa ya
BBC Thai kuwa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR ,
limeomba familia hiyo ibaki nchini Thailand wakati jitahada za
kuwapeleka nchi nyingine zikifanyika.
Nchi ya Thailand haina sheria ya kuwapatia makazi wakimbizi au watafuta hifadhi.
Picha ya ndani ya jengo la uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi
Takriban watu 40,000 wamedaiwa kudanganywa na tapeli huyo
Mahakama moja ya Thailand imemuhukumu tapeli mmoja zaidi ya kifungo cha miaka 13,000 jela.
Pudit Kittithradilok ,34, alikiri kumiliki mradi mmoja wa piramidi ambao aliwaahiidi wawekezaji kupata mapato ya hali ya juu.
Takriban watu 40,000 walikubali kuwekeza kiwango cha $160m katika kampuni yake.
Mahakama ilisema kuwa alijihusisha na vitendo vya kutoa mikopo na makosa 2,653 ya udanganyifu.
Baada ya kukiri ,mahakam hiyo ilipunguza hukumu hiyo na kumpatia kifungo cha miaka 6,637 na miezi sita.
Huenda asihudumu zaidi ya miaka 20 kwa kuwa sheria ya Thai inatoa miaka 10 kwa makosa mawili aliyopatikana nayo.
Waendesha
mashtaka waliambia mahakama kwamba Pudit aliandaa semina ambapo
waliohudhuria walishawishiwa kuwekeza katika kile alichosema ni biashara
zinazohusiana na ujenzi ,urembo, uuzaji wa magari yaliotumika uuzaji wa
bidhaa nje ya nchi miongoni mwa vitu nyengine.
Kulingana na gazeti la Bangkok Post, wawekezaji waliahidiwa mapato makubwa na marupurupu iwapo wataleta wanachama wapya.
Na
kama mradi mwengine wowote wa Piramidi, wawekezaji waliowekeza fedha
zao wa kwanza wanalipwa kuwalipa wanachama wao wa kwanza.
Pudit alikuwa anazuiliwa katika jela ya Bangkok tangu alipokamatwa mwezi Agosti wakati aliponyimwa dhamana.
Mahakama ilizipiga faini kampuni zake mbili ilio sawa na dola milioni 20 kila moja.
Pudit na kampuni zake aliagizwa kulipa takriban dola milioni 17 kwa waathiriwa 2,653 pamoja na riba ya kila mwaka ya 7.5%
Kwa kawaida, Mwaka Mpya unapowadia, watu hujiwekea maazimio na malengo mengi ya kutimiza katika mwaka husika.
Mara nyingi huwa ni kupunguza uzani, kufanya mazoezi zaidi, kuacha kuvuta sigara, kujifunza lugha mpya na kadhalika.
Lakini mara nyingi malengo haya huwa hayatimizwi.
Hatuwezi
kukuambia ni maazimio gani yanafaa kuwekwa, lakini kuna utafiti
uliofanywa ambao unaweza kukuelekeza jinsi ya kujiwekea malengo ambayo
utaweza kuyatimiza na pia njia bora zaidi ya kuhakikisha unatimiza
malengo hayo.
Kuna ushahidi kwamba mara nyingi binadamu huongozwa
na hamu ya "kupunguza hasara" - yaani, huwa mara nyingi tunaongozwa na
kufuta hasara ambayo tumepata badala ya kupiga hatua mbele.
Kuweka
maazimio kwa njia ambayo lengo lako zaidi litakuwa kupunguza au kufuta
hasara, kwa maana ya kupata kitu ulichokipoteza, huenda yakawa rahisi
kutimiza kuliko maazimio ya kukipata kitu kipya.
Mfano, inaweza
kuwa rahisi kwako kuurejelea uraibu uliokuwa nao awali au kujiweka sawa
kimwili kufikia kiwango cha awali kuliko kuboresha muonekano wako au
uwezo wako kufikia viwango ambavyo haujawahi kuvifikia awali.
Hili
pia linatuelekeza kwenye ushauri mwingine muhimu unapojiwekea malengo yako
ya mwaka - lazima yawe na uhalisia na yanayoweza kutimizika.
Washirikishe wengine
Mwanafalsafa
katika Chuo Kikuu cha Warwick Dkt John Michael hutafiti kuhusu mambo
mbalimbali ya kijamii yanayowasaidia watu kutimiza malengo na ahadi zao.
Anasema kuwa
kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kutimiza ahadi na maazimio iwapo
tutayatazama kuwa na umuhimu kwa watu wengine - kwamba maslahi ya
wengine yatakuwa hatarini iwapo tutashindwa.
Hii huenda ikawa ni kwenda darasani na rafiki yao.
Ufanisi
unaweza kuwa hata zaidi iwapo utalipa karo mapema - ukihisi kwamba mtu
amewekeza pesa na muda wake, na kwamba vyote vitapotea, basi kuna
uwezekano kwamba utajizatiti kutimiza malengo hayo.
Utafiti wa
Dkt Michael pia unaonesha kwamba watu huenda wakahamasishwa kuendelea na
kazi wasiyoipenda iwapo mtu mwingine wa maana kwao amewekeza kitu hapo.
Sifa na hadhi ya mtu huwa muhimu sana, na vinaweza kutumika kama kichocheo.
Kuyafanya maazimio yako wazi kunaweza kukuhamasisha kuyatimiza kwani utahofia kwamba hadhi yako itashuka iwapo hutayatimiza.
"Huwa
hakuna anayetaka kupata sifa za kuwa mtu asiyeaminika, kwa hivyo kutangaza mipango yetu hadharani kunaweza kukupatia motisha. Kuweka dau
kunaweza pia kuwa kichocheo zaidi," anasema Prof Neil Levy wa Chuo
Kikuu cha Oxford.
Vitu vya kukukumbusha
Kuweka maelezo zaidi na ufafanuzi kwenye maazimio yako pia husaidia, anasema.
Mfano
kwenda kwenye chumba cha mazoezi Jumanne alasiri na Jumamosi asubuhi,
kwa mfano, ni bora kuliko kusema tu kwamba utaenda kufanya mazoezi mara
nyingi zaidi, anasema Prof Levy.
Anapendekeza uhusishe maazimio yako na viashiria au vitu fulani vya kukukumbusha.
Iwapo
unataka kujifunza lugha nyingine, unaweza kwanza kuweka ahadi ya
kusikiliza makala ya lugha hiyo kila asubuhi ukisafiri kwenda kazini
asubuhi.
Kisha, ndipo ujiwekee nafasi ya kufanikiwa zaidi, unaweza
kuweka ujumbe wa kukukumbusha kufanya hivyo kwenye simu yako au kidhibiti mweleko wa
gari kila jioni kabla ya kulala.
Hapo, unaeleza nia na pia kuchukua hatua kuhakikisha unaitekeleza nia hiyo.
Kuweka masharti
Prof Levy anaonya pia dhidi ya kujiwekea masharti ambayo yanaweza kuwa kielelezo baadaye.
"Kubali
wazi kwamba kuna baadhi ya mambo yanayoweza kukuzuia kufanya jambo
(Sitakwenda kwa mazoezi iwapo nyumba itawaka moto). Lakini usipanue
masharti haya au kuyafanya kuwa mtindo kwani yanaweza kukuzuia
kutekeleza maazimio yako.
"Siku yangu ya kuzaliwa, inaweza kuwa
siku ya kipekee na inakubalika. Lakini nikianza kutambua mambo
yanayofanyika mara kwa mara - pengine iwapo ni wiki ya mwisho ya mwezi,
kuwepo kwa baridi kali - basi itakuwa mazoea," anasema. Yafanye maazimio yako kuwa sehemu ya mipango yako ya muda mrefu
Kufanya maazimio kuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu
Naye Dkt Anne Swinbourne, mwanasaikolojia katika chuo kikuu cha James Cook,
Australia, anasema kuwa maazimio bora zaidi ni yale ambayo yanaoana na malengo ya
muda mrefu ambayo umejiwekea wewe binafsi, kuliko yale ambayo hayana
msingi au ni matamanio tu.
Iwapo hujawahi kuonesha nia ya
kushiriki katika michezo, kujiwekea malengo ya kuwa mwanariadha stadi ni
lengo ambalo bila shaka utatatizika kutimiza.
Kwa sababu umekuwa
na ndoto ya muda mrefu ya kusafiri sana kujionea ulimwengu kabla ya
kutimiza miaka 50, lengo la kusafiri zaidi linaweza kutimizika.
Na pia, kutimiza malengo yote hutegemea mipango yako.
Tambua
ni mambo gani yanakuchochea kufanya mambo usiyoyapenda au usiyoyapenda.
Iwapo hutaki kunywa pombe sana, panga kukutana na marafiki au wageni
wako kwenye mgahawa badala ya baa, vilevile, ukipanda kuacha kuvuta
sigara, vyema zaidi ni kuacha kujihusisha na wavutaji sigara sana.
Malengo yako ya mwaka ni vyema ukayaandika vizuri na kuyabandika mahali ambapo utayasoma mara kwa mara mfano kwenye kitanda chako !!!!!
Mwanamume asiye na makazi amepata pesa nyingi uwanja wa ndege Ufaransa
Mwanamume ambaye
alipata pauni 260,000 baada ya kuegemea mlango wa kampuni ya Charles de
Gaulle kwenye uwanja wa ndege nchini Ufaransa na mlango ukafunguka na kukuta kitita cha fedha anaaminiwa kuwa mtu asiye
na makazi.
Polisi wanasema kuwa walimtambua mwanamume huyo kupitia
kwa kamera za CCTv kama mmoja wa watu wanaolala karibu na uwanja wa
ndege.
Mlango wa kampuni inayoshughulikia masuala ya fedha ya
Loomis terminal 2F, ulikuwa umeachwa bila kufungwa na mwanamume ambaye
umri wake unakisiwa kuwa miaka 50 hivi alitoka nje akiwa na mifuko
miwili ya pesa.
Kwa sasa anasakwa na polisi.
Mwendo wa saa (16:30 GMT) Ijumaa iliyopita king'ora kililia katika kampuni hiyo inayohusika na masuala ya fedha.
Maafisa waliochunguza video ya cctv waligundua kuwa mwananamume
huyo alikuwa akichakurachakura kwenye ndoo za taka nje ya ofisi hizo ili kupata chochote kitu, na
kuonekana kushangazwa wakati mlango aliokuwa ameegema ulipofunguka ghafla.
Aliingia ndani na muda mfupi baadaye akaondoka akiwa amebeba mifuko miwili.
Mwanamume huyo aliacha mfuko wake nyuma lakini haukuwa na stakabadhi yoyote ambayo ingesababisha atambuliwe.
Pesa alizochukua zinatajwa kuwa jumla ya pauni 260,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 750. AMELALA MASKINI AKAAMKA TAJIRI usikate tamaa hadi uingie kaburni!!!!.
Mpanda majengo marefu afariki baada ya kuanguka China
Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amehofiwa kufariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.
Wu
Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya
kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya
majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.
Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.
Mpanda majengo marefu akionesha manjonjo huko China
Swati Reddy (kulia) na mpenzi wake wanadaiwa kumuua mume wake Sudhakar (kushoto) mwezi uliopita
Wapenzi wiwili
nchini India wamekamatwa kwa kumuua mume wa mwanamke na kisha kujaribu
kumfanyia upasuaji wa kubadilisha sura mwanamume mpenzi ili aweze
kuchukua mahala pake,
Tindi kali ilimwagwa kwenye uso wa
mwanamume, mpenzi wa mwanamkea, katika shambulizi lililopangwa, huku
wapenzi hao wakipanga kusema kuwa sura yake ilikuwa imebadilika baada ya
upasuaji.
Lakini ndugu wa bwana wa mwanamke aligundua mpango huo alipofika hospitalini.
Alitoa malalamiko yake kwa polisi ambao walifanya uchunguzi wa vidole na kugundua njama huyo.
Mke,
Swati Reddy amekamatwa. Polisi waliiambia BBC kuwa watamkamata pia
mpenzi wake, Rajesh Ajjakolu mara atakapotibiwa majeraha yake na
kuruhusiwa kuondoka hospitalini. Rajesh Ajjakolu alilazwa hospitalini akiwa na majeraha ya uso
Bwana Sudhakar Reddy anadaiwa kuuliwa usiku wa
tarehe 26 Novemba na mwili wake kutupwa siku iliyofuatia. Hadi sasa
mwiwi huo bado haujapatikana.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo amekiri kuwa walimuua mume wake.
Rajeshi
Ajjakolu alilazwa hospitalini tarehe 28 Novemba huku Bi Reddy
akiwajulisha familia ya mume wake kuhusu shambulizi la tindi kali.
Polisi
wanasema kuwa wazazi wa Bw. Reddy waliamini kuwa mwanamume ambaye
alikuwa akipata matibabu alikuwa ni mtoto wao na kulipa hadi dola 7,758
kama bili ya hospitali.
Njama hiyo haikugunduliwa hadi tarehe 9
mwezi Disemba, wakati ndugu yake Reddy, alifika hospitalini humo na
kuwajulisha polisi aliposhuku kuwa mwanamume huyo hakuwa ndugu yake.
Raila Odinga
Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA,
umetangaza kuahirishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa
muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na
makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya.
Shughuli hiyo ilikuwa imepangwa kufanyikasiku ya Jumanne tarehe 12 mwezi huu.
Katika
taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya
kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya
wananchi itatangazwa baadaye.
Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.
Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu,
baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi
wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Wakati wa kuapishwa kwake
tarehe 28 mwezi uliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuunganisha taifa
katika muhula wake wa pili uongozini katika sherehe ambayo ilisusiwa na
viongozi wa upinzani.
Akihutubu baada ya kula kiapo uwanjani
Kasarani, Nairobi, kiongozi huyo alisema ameyasikia baadhi ya
mapendekezo ya upinzani na atazingatia baadhi.
Hata hivyo aliwahimiza viongozi wa upinzani kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo.