Jumanne, 30 Septemba 2014

RAILA ODINGA ACHAPWA MIJELEDI

Raila Odinga alichapwa mara mbili kwa kiboko katika tukio lililowashangaza wengi
Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kumtandika mijeledi kiongozi huyo wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga
Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alizidiwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanamume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wanasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kuzindiwa nguvu na walinzi hao wa Raila,

FESIBUKU YAPATA MPINZANI WA NGUVU

Ello
Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.

RAIS UHURU KENYATTA SHURTI AHUDHURIE ICC

                      Rais Uhuru Kenyatta akiwa katika kikao cha mahakama ya ICC                  

Majaji wa mahakama ya jinai ya ICC wameamua kuwa rais wa Kenya hana budi kufika mahakamani binafsi Oktoba tarehe 8.

Majaji hao wamekatalia mbali ombi la mawakili wa rais Uhuru Kenyatta la kutaka aruhusiwe kuhudhuria kikao hicho kupitia kwa njia ya Video ama kikao hicho cha ana kwa ana kiahirishwe hadi siku nyingine kwani alikuwa amekabiliwa na kazi nyingi katika majukumuyake kama rais wa Kenya.

Majaji hao wanasema kuwa Rais Uhuru Kenyatta hakutoa sababu madhubuti ya kukosa kuhudhuria kikao hicho maalum.

Majaji hao aidha wanasema kuwa Bwana Kenyatta lazima awepo ili kujibu maswali muhumu kuhusu ushirikiano wa serikali yake na kujadili maswala muhimu yatakayowasilishwa katika kikao hicho.

Kenyatta alikuwa ameiambia mahakama kuwa amepangiwa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha uhuru wa Uganda katika kipindi hicho.

Kauli hiyo inatolewa wakati ambapo mwendesha mashataka wa mahakama hiyo Fatou Bensouda alikuwa amepinga ombi la rais Kenyatta la kuahirisha kikao hicho ama kuruhusiwa kushiriki kikao hicho kwa njia ya video.

Bi Bensouda alikuwa ameilalamikia mahakama hiyo akidai kukosa ushahidi wa kutosha baada ya serikali ya Bw Kenyatta kumnyima stakabadhi alizotaka ili kuimarisha kesi dhidi ya kiongozi huyo wa Kenya.

Bw Kenyatta kwa upande wake naye alikuwa amewasilisha ombi mahakamani ya kutaka kesi dhidi yake itupiliwe mbali baada ya bi Bensouda kukiri kuwa hakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake

KUNYWA POMBE NA KUENDESHA GARI NI NOMA: PHELPS APIGWA FAINI

Michael Phelps akiwa na moja ya medali ya dhahabu aliyotwaa hivi karibuni                  

Muogeleaji wa kimataifa wa michuano ya Olympic nchini Marekani Michael Phelps amekamatwa kwa kuendesha gari kwa kasi akiwa amekunywa pombe.

Polisi mjini Baltimore, jimboni Maryland,wanasema walimsimamisha Phelps katika kizuizi cha njiani akiwa ameendesha kasi ya km 135 kwa saa mapema wiki hii.

Mr Phelps alipokamatwa na polisi wa usalama barabarani alitoa ushirikiano wa dhati na alipo wekewa kipimo cha upimaji kiwango cha kilevi alikutwa amelewa na alipigwa faini kisha kuachiliwa aendelee na safari yake,ingawa baaye aliomba radhi kupitia mtandao wa twitter, kwa kusema anatambua makosa yake na anajua hataeleweka sasa lakini kwa wale wote watakao hisi amewaangusha anaomba radhi..

Mpaka sasa Phelips ameshatwaa medali 22 katika michuano hiyo ya Olimpic na kumfanya kuwa muogeleaji pekee mwenye medali nyingi kuliko mwingine yeyote.

Phelps, mwenye umri wa miaka 28, ameamua kustaafu michuano hiyo ya Olimpic kuogelea baada ya kutwaa medali yake ya 22 katika michuano ya London kwa mwaka 2012 na akatangaza kustaafu mapema mwaka huu.

Na hii si mara ya kwanza kwa nguli huyo wa uogeleaji kukamatwa na kupigwa faini kwa makosa ya kuendesha akiwa amekunywa pombe kwani mwaka 2004 alikamatwa na kupigwa faini kwa kosa hilo hilo.

WAKURDI WAREJESHA MPAKA MUHIMU SYRIA

Wapiganaji wa kikurdi nchini Iraq

Wanajeshi wa kikurdi nchini Iraq wameripotiwa kurejesha tena mpaka muhimu kuingia nchini Syria kutoka kundi la dola la kiislam la Islamic State .

Wapiganaji wa kikurdi walifanya shambulizi la mapema asubuhi katika eneo la Rabia, inayomiliki njia kuu inayounganisha Iraq na Syria.

Kulikuwa na makabiliano kutoka kundi la kiislam IS, ambapo watu takribani watano walijilipua kwa bomu ndani ya gari na kusababisha vifo vya wapiganaji muhimu kikurdish.

Ndege za kivita za Uingereza zifanya shambulizi la kwanza kwa kuwalenga wapiganaji wa dola ya kiislamu IS nchini Irang wakati ndege za kivita za Marekani ziliwashambulia wapiganaji hao karibu na mji wa Kobani nchini Syria karibu na mpaka wa Uturuki ambapo mapigano makali yanaendelea kati ya wakrudi na wapiganaji wa IS.

PROGRAM YA KUFUNDISHA HISABATI KWA SIMU YAJA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo akizungumza katika uzinduzi huo.
Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akizungumza katika uzinduzi huo. Kampuni ya Tigo, Nokia na Microsoft ndio wadau mpango huo.
Meneja Mawasiliano wa Microsoft Mobile Devices, Lilian Nganda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika
uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo (katikati), akiangalia simu wakati akiwaelekeza namna ya kutumia simu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania, Peter Riima (kushoto) na Mrashani Katebeleza, wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.

Jumatatu, 29 Septemba 2014

SIDE MNYAMWEZI HATUNAE


Muimbaji wa muziki wa Bongo Fleva Said Salim 'Side Boy Mnyamwezi' enzi za uhai wake.
Muimbaji wa muziki wa Bongo Fleva, Said Salim aliyekuwa akitumia jina la kisanii la Side Boy Mnyamwezi amefariki dunia. Side Boy amefariki leo katika Hospitali ya Nyangao iliyopo mkoani Lindi. Aliwahi kutoa nyimbo kadhaa zikiwemo ‘Hujafa Hujaumbika’, ‘Usidharau Usiyemjua’ na ‘Kua Uyaone.’

MESSI AFUNGA BAO 400

Messi amefunga jumla ya mabao 401
Mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi amesema kuwa hakuwahi kufikiria kuwa atawahi kufunga mabao 400.
Mchezaji huyo aliyewahi kutwaa taji la mchezaji bora duniani mara nne aliwahi mabao mawili katika mechi yao dhidi ya Grenada vigogo hao wa ligi kuu ya Uhispania walipofunga mabao 6-0 .
Mshambulizi huyo wa Argentina alifunga mabao mawili ya 400- na 401.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique alimsifu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 akisema kuwa ilikuwa ni mafanikio makubwa.
Tangu atue Uhispania Messi ameifungia Barcelona mabao 359 akaifungia Argentina mabao 42 katika jumla ya mechi 506 alizoshiriki.
Kiungo huyo machachari ameisaidia sana Barcelona kutwaa mataji 21,yanayuojumuisha 6 ya ligi kuu ya Uhispania La Liga na 3 ya kombe la mabingwa barani Ulaya katika muongo mmoja uliopita.
Kibinafsi Messi alishinda mataji manne ya Ballon d'Ors,ambayo hutuzwa mchezaji bora duniani kuanzia mwaka wa 2009 hadi 2012.
"nitajitahidi zaidi kunogesha talanta yangu''

KATIBA MYA KUPIGIWA KURA LEO


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge akichangia baada ya kupewa nafasi kuhitimisha mjadala wa bunge hilo.

UPIGAJI kura kupata Katiba Inayopendekezwa, unatarajiwa kuanza leo ambapo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walio bungeni na nje ya Bunge, watapiga kura ya kuikubali, au kuikataa kwa njia ya wazi na siri.


Kwa wajumbe watakaokuwa nje ya ukumbi huo, wakiwemo watakaokuwa nje ya nchi, tayari utaratibu wa kupiga kura popote walipo kwa njia ya nukushi (faksi) na intaneti, umeshaandaliwa.

Akizungumza bungeni juzi wakati wa kuhitimisha mjadala wa mapendekezo ya mabadiliko ya Rasimu katika Katiba Inayopendekezwa, aliyekuwa Mwenyekiti Kamati ya Uandishi wa Bunge, Andrew Chenge alisema mjumbe wa Kamati hiyo, Dk Tulia Akson ndiye atakayewasilisha marekebisho yaliyofanywa katika rasimu hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliagiza kamati zote 12 za bunge hilo kukutana jana saa nane mchana bila kuwapa ajenda ya kikao hicho, ambacho alisema wenyeviti wa kamati hizo watakuwa nayo.

Jana gazeti hili lilimtafuta Katibu wa Bunge, Yahya Khamis Hamad kujua idadi ya watu watakaopiga kura nje ya ukumbi wa Bunge, watakaokuwa nje ya nchi na vituo vyao, lakini simu yake ilikuwa imezimwa.

Hata hivyo, taarifa kutoka miongoni mwa watendaji wa bunge hilo zilizofikia gazeti hili, zilieleza kuwa mpaka jana mchana kazi ya kuhakiki wajumbe ambao hawatakuwepo katika Ukumbi wa Bunge, ilikuwa ikiendelea.

Tayari Ofisi ya Bunge la Katiba, ilitoa taarifa kuwa itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba Inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge waliokwenda Hijja ambao wanatarajiwa kuwa zaidi ya wanane.

Mbali na Makka, pia mabalozi wa Tanzania nchi za nje, wanatarajiwa kuwa wasimamizi wa kura zitakazopigwa kwa faksi na intaneti na baada ya hapo zitawasilishwa katika ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kujumlishwa.

Theluthi mbili

Akizungumza juzi baada ya kupewa nafasi kutoa neno la kuunganisha wajumbe, mjumbe mzee kuliko wote, Kingunge Ngombale Mwiru aliwataka wajumbe wasiangalie mambo binafsi ambayo hayakuwekwa katika Katiba Inayopendekezwa, bali waangalie matakwa ya nchi.

“Wananchi wanataka Katiba, tusije tukazuia Katiba bora kwa sababu tunataka kila kitu kiingie katika Katiba. Nataka tufikirie nchi yetu na hatima yake. “Ili Katiba hii ipite, lazima ipate theluthi mbili ya wajumbe wa Tanzania Bara na theluthi mbili Zanzibar na hapa maana yake ni kura…kitendo cha kusema mh, tunaweza kukwama na mkwamo huo hauna tija kwa wafanyakazi, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo na wanawake,” alisema.

Alisisitiza kuwa yaliyowekwa katika Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, yanatosha kufanya Tanzania ipige hatua mpya katika miaka hamsini ijayo.

Ubora wa Katiba

Akielezea ubora wa Katiba inayotakiwa na wananchi, Kingunge alisema wajumbe wote kwanza watambue kuteuliwa kwao na makundi yao kwa upande mmoja na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, kwa upande mwingine, hatimaye wametumwa na wananchi, ambao wanataka Katiba mpya.

Katiba hiyo ili iwe bora kwa mujibu wa Kingunge, inatakiwa iimarishe mafanikio ya miaka 50 ya Tanzania, na ili kufanikisha hilo Bunge hilo lilikataa muundo ambao ulikuwa ukielekea kusambaratisha nchi.

Kigezo cha pili cha Katiba bora, Kingunge alisema ni uwezo wake wa kuondoa kero za wananchi na kutoa mfano wa uamuzi wa Bunge Maalumu la Katiba, kurudisha nafasi ya Rais wa Zanzibar, kuwa Makamu wa Pili wa Rais.

“Uamuzi wetu wa nyuma (kumuondoa Rais wa Zanzibar katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ulikuwa na upungufu…tuliangalia zaidi ujio wa vyama vingi na kusahau walioungana walikuwa pande mbili za Zanzibar na Tanganyika,” alisema na kusisitiza kwa mabadiliko hayo, Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa ni bora.

Eneo jingine la Katiba bora kwa mujibu wa Kingunge, ni Katiba husika kuingiza mambo mapya ambapo kwa sasa Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, imeimarisha nafasi ya wananchi katika nchi.

“Ndio maana tunazungumzia haki kwa mara ya kwanza ya wakulima, wafugaji, wachimbaji wadogo, wanawake, vijana, walemavu na makundi mengine,” alisema.

Alisema baada ya mkutano huo wa Bunge Maalumu la Katiba, Tanzania haitakuwa kama ilivyokuwa huko nyuma, kwa kuwa makundi yote ya jamii, yamekutana na kufanya uamuzi.HABARILEO

WANAUME WALA KICHAPO


Hizi ni picha zinazoonesha wanaume wakipata kichapo kutoka kwa wake zao.



UINGEREZA YAIONDOA KENYA KWENYE TAHADHARI

Serikali imeondoa tahadhari iliyowekea raia wake kuingia Kenya
Uingereza imeondoa tahadhari iliyokuwea imetoa kwa raia wake dhidi ya Kusafiri Kenya.
Tahadhari hiyo kwa ukubwa likuwa inalenga maeneo ya mitaa ya mabanda, na baadhi ya maeneo ya Pwani ambako ilihofiwa kuwa raia wa kigeni wanalengwa kwa mashambulio ya kigaidi.
Hatua hiyo ya kuondolewa tahadhari kwa raia wa Uingereza kusafiri Kenya, inaanza kutekelezwa mara moja.
Tahadhari hiyo ilikuwa imewekwa baada ya machafuko yaliyotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu yapata miaka saba iliyopita.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imewasiliana na wizara ya ndani ya nchi hiyo kwamba hali ya hatari imeshuka kwa kiasi kikubwa.
Wizara hizo zimesema kuwa tahadhari kama hizo hutolewa kuambatana na sera za nchi hiyo za kuwatolea usalama raia wake kote duniani licha ya taifa linalozungumziwa.
Serikali ya Kenya ilikuwa imelalamika kuwa tahadhari kama hizi zinazotolewa na mataifa ya Magharibi hazina msingi na zinaathiri uchumi wa nchi hiyo.

GHANI ALIPOAPISHWA KUWA RAIS MPYA WA AFGHANISTAN

Ashraf Ghani rais mpya wa Afghanistan
Ashraf Ghani ameapishwa kuwa rais mpya wa Afghanistan, akichukua nafasi ya Hamid Karzai katika sherehe zilizofanyika ikulu ya rais mjini Kabul.
Kuapishwa kwa Bwana Ghani kunakuja baada ya miezi sita, huku kukiwa na mvutano mkubwa kuhusu kulalamikia udanganyifu katika kupiga na kuhesabu kura.
Kwa mujibu wa mkataba uliosimamiwa na Marekani Bwana Ghani atashirikiana madaraka na mshindi wa pili katika uchaguzi wa urais Bwana Abdullah Abdullah ambaye atakuwa afisa mtendaji mkuu.
Kundi la Taliban limeupuuza mkataba huo kwa kuuita "igizo la Marekani". Mlipuko karibu na uwanja wa ndege wa Kabul umeua watu wapatao saba.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Sediq Sediqi amesema mtu aliyajilipua alishambulia kituo cha usalama cha ukaguzi katika barabara ya uwanja wa ndege inayoenda ubalozi wa Marekani.
Askari wanne wa usalama wa Afghanistan na raia watatu wameuawa na watu kadhaa kujeruhiwa, amesema.

Mabadiliko ya Kikatiba

Bwana Ghani ameapa kutii katiba katika sherehe za kuapishwa zilizohudhuriwa na viongozi 100.
Amesema atafanya kazi ya mpango wa amani ya muda mrefu, ameahidi kupambana na rushwa na kusema kuwa mabadiliko ya katiba yanahitajika

PhD YA WIKI MBILI MHHH

Chama cha wanachuo nchini Zimbabwe, Ijumaa hii kimeutaka uongozi wa chuo kikuu cha Zimbabwe kujiuzulu baada ya kumpatia mke wa rais Robert Mugabe, PhD miezi miwili tu baada ya kuanza masomo.
Huchukua zaidi ya miaka mitatu hadi minne kwa mwanafunzi wa kawaida ili kupata PhD.
PhD hiyo ilitolewa kwa Grace Mugabe, 49 aliyekuwa mpiga chapa wa zamani kwenye ofisi ya rais, wiki mbili zilizopita. Mke wa Mugabe alivalishwa kofia ya kuhitimu masomo hayo na mume wake pamoja na wahitimu wengine.
Utaoji wa PhD umetafsiriwa kama njia ya kifisadi ya kupandisha CV ya mke wa Mugabe ili aje kugombea urais pindi rais huyo akifariki.

Alhamisi, 25 Septemba 2014

WALINZI NA POLISI WANYANG"ANYWA SILAHA ILI KUZIPIMA

Kenya: Walinzi  wawili ( bodyguards) ambao walikuwepo eneo la Bunge la  Makueni siku ya Jumanne ambapo yalitokea majibizano ya risasi wamenyang'anywa silaha zao.

Bunduki zao pamoja na risasi 8zimepelekwa kwa mako makuu ya Upelezi ili kuainisha ni silaha gani iliyohusika katika vurugu hizo.

 

Pamoja nao Askari polisi watano waliokuwa eneo hilo nao wamenyang'anywa silaha zao.

 

Mkurugenzi wa Upelelezi bwana Ndegwa Muhoro alisema kuwa wanataka kujua ni silaha gani zilitumika kabla ya kuchukua hatua kali.

 

Alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kulikuwa na uzembe katika matumizi ya silaha za moto.

"Silaha hizo zinafanyiwa uchunguzi katika uchungu wetuwa tukio hilo. Hata hivyo imeonekana wazi kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya silaha na tunataka kupata ushahidi wa kina kuhusu jambo hilo," Alisema.

Aliongeza kuwa Mkuu wa CID  Nyeri Bwana Mohamed Amin ndiye anayeongoza timu ya wapelelezi kutoka Nairobi kuchunguza wa tukio hilo la aibu.

"Zama za uhuni wa aina hii zimepita na watu wanapaswa kujua kuwa mambo yameebadilika.," alisema Muhoro.

Watu sita walijeruhiwa katika tukio hilo.

MAJAMBAZI YAWATUPIA PESA WATU WALIOKUWA WAKIWAFUKUZA WAFANIKIWA KUTOROKA

Nairobi, Kenya: Kituko kilitokea mtaa wa Banda jijini, Nairobi leo baada ya majambazi wenye silaha walipowarushia fedha wananchi wenye hasira na kufanikiwa kutoroka kwenye duka la  Mpesa ambapo walikuwa wamepora sh milioni 1.4 za kenya sawa na milioni 20 za kitanzania.

 Majambazi hayo manne yaliyokuwa na bastola walivamia duka hilo la Mpesa lililoko kwenye ghorofa ya chini ya Gilfilan House yalipora fedha hizo na kisha kuanza kuondoka kwa miguu.
Mhudumu wa duka hilo alamua kuwafukuza huku akiomba msaada kwa wananchi.

Mashuhuda wa tukio hilo alidai kuwa aliona jambazi mmoja akiwa ameshikiliwa na wananchi hao waliokuwa na kiu kubwa ya kumwaga damu yake karibu na msikiti wa Jamia.

Ilibidi achukue bunda la noti katika mkoba aliokuwa ameweka hela hizo na kwatupia wananchi hao. .
Wananchi hao walipoona noti zile walimwacha na kuanza kugombania noti zile ingawa mama huyo mhudumu wa duka aliendelea kugutia mwizi.
Mama huyo, Shaheen Afzal, aliendelea kuwafukuza huku akipiga kelele za mwizi ambapo baada ya mita 50 jambazi mwingine alitupa noti karibu na  Bazaar Plaza kitu ambacho kilifanya wananchi waache kuwakimbiza na kwenda  kugombania pesa hiyo na wao kufanikiwa kutoroka.

Shaheen lisema kuwa majambazi hayo pia yalidondosha pochi yake waliyoiba pale dukani na kuchanyikana na raia waliokuwa wanatembe barabara ya Moi na kutoweka.

Baba yake Shaheen aitwaye Mohamed Afzal alosema kuwa majambazi hayo yaliingia dukani kwake saa 5 wakijifanya wanunuzi na kuwa walitaka kutuma pesa.
“Mmoja wao alikuja na kuketi akijifanya ni mteja ndipo wale watatu walipfika na kuanza kutuvuruga. Mmoja alisimama mlangoni na kuzuia wateja kuingia,” alisema Afzal.
Afzal alisema kuwa walivunja makabati na kuchukua hela hizo zilizokuwa tayari kupelekwa benki.

MAN CITY YAFANYA KUFURU TENA

Wachezaji wa Manchester City

Manchester City imeweka historia ya ushindi wa mabao saba kwa mara ya tatu katika kombe la ligi, mvua ya magoli iliwanyeshea Sheffield W. kipindi cha pili cha mchezo.

Hapo jana Historia ilijiandika kwa klabu ya Sheffield ikiwa ni mara ya kwanza kwao kupokea kipigo cha zaidi ya mabao sita .

Katika mechi nyingine zilizochezwa, Chelsea ilitoka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Bolton, Newcastle United iliibuka na ushidi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Crystal Palace, Westbromwich Albion ikatoka na ushindi wa mabao matatu dhidi ya mawili ya Hull city.

INUKA KUWAINIU WATUMISHI MORO

Mratibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya maendeleo ya wanawake tanzania (INUKA), David Msuya kushoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mikakati ya kuboresha maisha ya watumishi wa sekta binafsi na serikali mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG

Watumishi wa wa sekta binafsi na serikalini wameanza kuwekewa mikakati ya kuboresha maisha na asasi isiyo ya kiserikali ya maendeleo ya wanawake Tanzania ya Inuka yenye lengo la kuwapunguzia makali ya maisha katika mkoa wa Morogoro.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Mratibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya maendeleo ya wanawake Tanzania (INUKA), David Msuya alisema kuwa asasi hiyo imeanza kuboresha maisha ya watumishi wa wa sekta binafsi na serikalini kwa kutoa mikopo ya riba nafuu.

Msuya alisema kuwa asasi hiyo ilifanya utafiti wa kina na kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa na hofu ya kuchukua mikopo katika taasisi za fedha kutokana kuwepo kwa masharti magumu.

Inuka ilianza kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo na sasa wameelekeza mkakati wa kuwakopesha watumishi wa serikali na binafsi kuanzia shilingi mil.25 alisema Msuya.


“Lengo la utekelezaji wa mpango huo wa kuboresha makazi ya watumishi ni moja ya hatua ya kusaidiana na serikali katika kupunguza kero na makali ya maisha kwa wananchi hususan watumishi wa serikali ambao licha ya kuwa ni sehemu ya jamii lakini mishahara wanayopata hakidhi mahitaji halisi ya ukali wa maisha.”Aalisem Msuya.

Msuya aliongeza kwa kusema kuwa asasi hiyo kabla ya kutoa mkopo mwa mtumishi hupewa elimu ya ujasiriamali pamoja na mfumo rasmi wa matumizi ya fedha kabla ya kukabidhiwa ili malengo walijiwekea kwa mujibu wa mkataba yaweze kuleta tija kwa taifa.


Mbali na mikakati hiyo changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa wateja wao baadhi yao sio waaminifu pindi wanapopata mikopo hushindwa kurejesha kwa wakati na wengine hutomokea kabisa jambo ambalo linarudisha nyuma malengo ya asasi hiyo katika kuwahudia wananchi kwa wingi zaidi.alisema Msuya.


Asasi hiyo katika mkoa wa Morogoro imeweza kuwahudia wananchi 200 kutoka Morogoro mjini, Gairo, Kilombero ambapo jumla ya shilingi mil.24 zilitumika kuwakopesha wajasiriamali wadogowadogo ili kuwaongezea mitaji yao.

SASA MBU KUANZA KUPAMBANA NA HOMA YA DENGUE

Watafiti wanaamini kuwa Mbu hao wenye viini watapambana na homa ya Dengue
Watafiti nchini Brazil, wameachilia maelfu ya Mbu wenye viini vya Bakteria ili kupambana na homa ya Dengue.
Wanatumai kuwa Mbu hao watazaana kwa haraka idadi yao ikiwa kubwa zaidi nchini Brazil na hivyo kuangamiza homa hiyo ya Dengue.
Mradi huu ni sehemu ya programu ambayo pia inafanyika nchini Australia, Vietnam na Indonesia.
Viini vya Bakteria vilivyotumika kuambukiza Mbu hao, hawana madhara kwa binadamu.
Programu hiyo iliyoanza mwaka 2012, kwa mujibu wa mmoja wa watafiti, Luciano Moreira, ambaye anaongoza utafiti huo.
Watafiti hao walitembelea mitaa minne mjini Rio, na kudadisi Mbu waliotolewa kutoka sehemu mbali mbali.
Mbu elfu kumi wataachiliwa kwenda katika maeneo ya watu kila mwezi kwa miezi minne.

'Viini vizuri vya Bakteria'
Viini hivyo vya Bakteria vinajulikana kama Wolbachiana na vinapatikana katika asilimia 60 ya wadudu.Vinafanya kazi kama chanjo kwa Mbu, ambao wana virusi vinavyosambaza homa ya Dengue, vinavyozaana mwilini.
Viini hivyo pia vinazuia kuzaana kwa Mbu wanaoeneza homa ya Dengue.
Utafiti huo, ulianza katika Chuo Kikuu cha Monash nchini Australia mwaka 2008.
Watafiti waliruhusu Mbu hao kunyonya damu kutoka kwenye mikono yao kuona ikiwa wanaweza kuambukiza homa ya Dengue.
Homa ya Dengue ilianza kuwa kero tena nchini Brazil mwaka 1981, baada ya kupotea kwa miaka 20.
Miaka 30 iliyofuata, matukio milioni saba vya maambukizi yaliripotiwa.
Brazil ndiyo nchi yenye matukio mengi vya maambukizi ya Dengue, huku watu milioni 3.2 wakiambukizwa na wengine 800 wakifariki kati ya mwaka 2009-2014

MKWEWE OSAMA AFUNGWA MAISHA


Osama bin Laden enzi za uhai wake 
Mkwe wa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda , Osama bin-Laden amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama moja mjini New York. Alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya ugaidi.
Jaji wa mahakama hiyo amemwambia Suleiman Abu Ghaith kuwa alionekana kuwa na nia na tayari kutekeleza ajenda ya mauaji kwa niaba ya al-Qaeda'

Suleiman Abu Ghaith mwenye umri wa miaka 48, alifanywa kuwa msemaji wa Al Qaeeda baada ya shambulizi la 9/11 na anasemekana kuwa afisa wa ngazi ya juu wa Al Qaeeda kufikishwa mahakamani Marekani tangu kutokea kwa mashambulizi hayo.

Alikamatwa nchini Jordan mwaka jana na kupelekwa Marekani alikokabiliwa na mashitaka hayo
.

Pia alitetea kazi yake akisema ni jukumu lake la kudini kuwaambia waisilamu wapambane na maadui wao

Mnamo mwezi Machi, jopo la majaji wa kiraia lilimpata na hatia ya njama ya kuwaua wamarekani pamoja na kulisaidia kundi la al-Qaeda.

Kanda za video zinazomuonyesha Abu Ghaith akitoa vitisho dhidi ya Marekani akisema analenga kuangamiza Marekani kwa kutumia ndege zilionyeshwa kwa majaji hao.

Abu Ghaith alisema kuwa jukumu lake ni la kidini kwani alikuwa akiwaaasa waisilamu kupambana na maadui wanaowakandamiza.BBC

ASAMOAH AKANA KUMTOA KAFARA NDUGU YAKE

Familia ya Gyan imeelezea kushangazwa na tetesi kuwa alimtoa kafara rafiki yake
Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amekanusha madai kuwa alimtoa kafara kaka yake ambaye pia alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana Castro.
Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina msingi.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa anaimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats, ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki yake Janet Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na Gyan ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.
Madai katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka kwa rafiki ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa kafara mwanamuziki huyo.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.
Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea kusambazwa mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali kuhusu madai hayo.
Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkamata kwa lengo la kumfungulia mashitaka.
Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi waendelee na uchunguzi wao.
Taarifa hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya huku madai na tetesi zikienezwa kila upande katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu tunaficha ukweli, bali kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa sababu tunataka polisi wafanye kazi yao bila kuingiliwa.''

INDIA NCHI YA NNE DUNIANI KUPELEKA CHOMBO MARS

India imewakilisha 'Mangalyaan katika sayari ya Mars

Wanasayansi wa anga za juu nchini India wanasema kuwa chombo chao cha safari za anga za juu kwa sasa kinazunguka sayari ya Mars.

Hii ndiyo mara ya kwanza kwa India kutuma mtambo wake kwenda kwa sayari hiyo, safari ambayo imepata umaarufu kutokana na gharama yake ya chini kabisa ya dola milioni 75 pekee.

India ndilo taifa la nne duniani kufaulu kufikisha chombo katika sayari ya Mars.

Mataifa mengine ambayo yamewasilisha vyombo vya utafiti wa anga za juu katika sayari hiyo ni Marekani, Urusi na muungano wa mataifa ya Ulaya.

www.cardealpage.com kwa mahitaji ya kununua gari lililotumika kutoka Japan kwa bei nzuri

Chombo hicho ''The Mangalyaan robotic probe'' kinatarajiwa kuanza upekuzi na uchunguzi wa hali ya anga katika sayari hiyo nyekundu.

Waziri Mkuu nchini India Narendra Modi ambaye alishuduia mafaniko ya chombo hicho kilichoanza safari yake miezi kumi iliyopita aliwapongeza wanasayansi hao kwa ufanisi huo mkubwa. Roketi ya India 'Mangalyaan iliyotua katika sayari ya Mars
Aliwaambia kuwa mafanikio ya safari za anga za juu nchini India ni mfano mwema wa hatua ambazo taifa hilo linaweza kupiga akisema kuwa ana mpango wa kuboresha kitengo hicho.

Shirikisho la anga za mbali la Marekani NASA ambalo lilifikisha chombo chake ''Maven'' katika sayari ya Mars Jumatatu wiki hii, liliwapongeza wanasayansi wa India kwa ufanisi wao.

Kupitia kwa ujumbe wa mtandao wa Twitter NASA iliandika kuwa ''Tunawapongeza @ISRO kwa kuwasili katika sayari ya Mars. Mtajiunga na @MarsOrbiter kutathmini hali ilivyo katika sayari hiyo. BBC

UCHUNGUZI KUANZA HUKO CAR - ICC

Mahakama ya ICC inasema ina taarifa za kuaminika kuhusu uhalali wa kivita uliotendwa nchini humo.
Mahakama ya kimataifa ya ICC imeanzisha rasmi uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu wa kivita katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Mwendesha mkuu wa mashitaka katika mahakama hiyo, Fatou Bensouda, amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya ubakaji, mauaji na watu kufurushwa kutoka makwao kwa lazima, mateso na maasi mengine tangu mwaka 2012.
Amesema pande zote zimehusika kwenye mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo ambao umegeuka na kuwa mzozo wa kidini kati ya waisilamu na wakristo hasa waasi wa Kiisilamu na wakristo.
Takriban robo ya idadi yote ya watu nchini humo wametoroka makwao.

'Watoto jeshini'
Mgogoro ualianza baada ya waasi wa Seleka kuchukua mamlaka kati ya nchi hiyo yenye idadi kubwa ya wakristo, mwezi Machi mwaka 2013.
Kiongozi wa waasi, Michel Djotodia alijiuzulu kama Rais mwezi Januari kufuatia shinikizo kali kutoka kwa viongozi wengine wa kanda hiyo.
Waisilamu, walilazimika kutoroka mashambulizi ya kulipiza dhidi yao yaliyofanywa na wapiganaji wa kikrsto, waliojulikana kama Anti-Balakas.
Rais Catherine Samba Panza alichaguliwa kama Rais wa Muda kumaliza ghasia lakini hali bado haijabadilika
Mwezi jana serikali ya muungano iliundwa, lakini haijamaliza taharuki katika nchi hiyo ambayo imegawanyika kwa misingi ya kidini.
Bi Bensouda, aliyeanzisha uchunguzi wa awali mwezi Februari, alisema ofisi yake imetathmini taarifa za kuaminika kuhusu uhalifu huo.
Bensouda alisema kuwa uhalifu mwingine wa kivita pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu, ulijumuisha mashambulizi dhidi ya mashirika ya misaada na kuwatumia watoto kama wanajeshi.
''Orodha ya uhalifu uliotendwa ni ndefu sana. Siwezi, kupuuza madai yanayosemekana kufanywa,'' alisema katika taarifa yake.
"Huu unapaswa kuwa ujumbe wa mwisho kwa wanaotenda uhalifu huu kwamba muda wao umekwisha, kilichosalia ni kukabiliwa na sheria,'' aliongeza kusema Bensouda.
Mapema mwezi huu Umoja wa Mataifa ulichukua jukumu la kulinda amani nchini humo kutoka kwa kikosi cha Muungano wa Afrika.

FASTJET HIYOOOO ENTEBBE


Captain Sagar Chavda ambaye ndiye Muongozaji wa Ndege Kutoka Dar es salaam kuelekea Entebbe
Jean Uku Commercial Manager akiwa anaongea na wateja wa Fastjet
Kushoto ni Jean Uku Commercial Manager wa Fastjet na Jimy Kibati General Manager wa Fastjet wakizindua Rasmi safari za Kwenda Entebe kutokea Dar es salaam.(P.T)
Wageni wakikaribishwa katika Ndege ya Fastjet kutokea Dar kwenda Entebe
Timu nzima ya Fastjet Baada ya sherehe fupi za uzinduzi huo
Ndege kati ya miji hii mikuu miwili zitaruka siku za Jumanne na Alhamisi kwa wiki za kwanza za mwezi Septemba na zinatarajiwa kuongezwa hadi mara nne kwa wiki kuanzia tarehe 29 Septemba.
Entebbe inakuwa kituo cha nne cha kimataifa kwa Fastjet ukitoa Harare, Johanesburg na Lusaka.
Mwelekeo huu mpya utapaisha ndege za moja kwa moja kati ya Entebbe na Dar es salaam kwa bei murua kabisa ukilinganisha na mashirika mengine ya ndege ambayo hutoa huduma zisizo za moja kwa moja kati ya miji hii mikubwa miwili.
Tiketi za safari hii zinapatikana kupitia www.fastjet.com kwa bei ya chini kabisa ya kuanzia Tshs. 80,000/= kwa safari moja (bila kodi).

BOKA HARAM WAJISALIMISHA

Wanamgambo wa Boko Haram
Jeshi nchini Nigeria limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo limesema katika mapambano limemuua mtu mmoja ambaye huwa anaonekana kwenye picha za video za propaganda za Boko haram wakishuku kuwa huenda ni Kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa majuma ya hivi karibuni Boko Haram imeshindwa kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa wakipambana kudhibiti eneo karibu na mji wa Maiduguri.
Jeshi limesema wafuasi 135 wa Boko Haram wamejisalimisha wakiwa na silaha zao katika majimbo ya Biu na Borno, halikadhalika wafuasi wengine 133 wanahojiwa na Jeshi

AJALI YA GARI ZA NOAH YAUA WAWILI MBEYA

Gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM iliyopata ajali jana maeneo ya Igurusi mkoani Mbeya.
Gari hiyo ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali.
 
GARI ndogo aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM limepata ajali na kuua watu wawili jana eneo la Igurusi mkoani Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko Igurusi kilometa 45 kutoka Mbeya Mjini na kuua dereva aliyefahamika kwa jina moja la Rashid na mama mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika

NDEGE ZA MAREKANI ZAFANYA KWELI ISIS

Ndege za Marekani zikienda kwenye shambulizi
Majeshi ya Marekani yameanza rasmi mashambulizi ya anga nchini Syria yakilenga kundi la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria). Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani yameeleza kuwa wanafanya mashambulizi ya mchanganyiko kwa kutumia mabomu, wapiganaji wa ardhini pamoja na majeshi ya Anga kutoka nchi za Mashariki ya Kati zinazowaunga mkono. Lakini habari za mashambulizi yaliyoanza zilitolewa na raia wa Syria aliyetweet kuhusu kile anachokisikia katika mji wa Raqqa ambako kuna makao makuu ya kundi hilo.
Mtu huyo anayetumia jina la Abdulkader Hariri aliandika kuwa milipuko mikubwa imelenga makao makuu ya ISIS na kwamba anga lote limejaa ndege za kivita na drones.
Baadaye Agency ya wanaharakati nchini Syria ilipost video fupi inayoonesha kwa mbali mashambulizi hayo.
Tazama video hapa chini (Kama simu yako haisomi player hii. Bonyeza >>>HAPA)

Jumatano, 24 Septemba 2014

FEDHA ZA SILAHA ZALETA UTATA


Maafisa wa serikali ya Nigeria wamekamatwa Afrika Kusini na zaidi ya dola milioni 9.3 pesa taslimu
Takriban wabunge 50 walikurupuka kutoka bunge la waakilishi la Nigeria baada ya mpango wa kujadili mswada unaohusiana na kuagizwa kwa silaha kutoka Afrika Kusini Kupingwa.
Wiki iliyopita, iliripotiwa kuwa maafisa wa serikali walibeba takriban dola 9.3 millioni pesa taslimu wakaenda nazo Afrika Kusini kununua silaha.
Naibu spika wa Baraza la waakilishi alisema kwa suala hilo linahusu usalama wa taifa na hivyo haliwezi kujadiliwa hadharani.
Bunge la juu pia liliwaita wakuu wa usalama nchini ili kujadili suala hilo.
Waandishi wa habari nchini Nigeria wanasema kuwa habari hizo zimewashangaza wananchi huku wengi wao wakitoa wito uchunguzi kufanywa ili kuzuia ubadhirifu wa mali ya umma.
Kashfa hiyo iligunduliwa Polisi nchini Afrika Kusini walipowakamata raiya wawili wa Nigeria na Muisraeli mmoja wakiwa na kitita hicho cha pesa zikiwwa kwenye mabegi matatu .
Hata hivyo watatu hao waliowasili Afrika Kusini kwa ndege ya kibinafsi hawakushtakiwa.
Mwandishi wa habari wa BBC ambaye yuko mjini Abuja, Haruna Shehu-Tangaza alisema kuwa wengi wa wabunge waliondoka kwa hasira walikuwa kutoka vyama vya upinzani.
Baadhi ya wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakidai kuwa Boko Haram wamejihami zaidi yao
Wabunge hawa walidai kuwa chama tawala cha People's Democratic Party (PDP) ndicho kilipinga mpango huu kupitia naibu wa spika,Emeka Ihiodioha.
Wachambuzi wanasema kuwa huenda Nigeria ikakabiliwa na vikwazo vya ununuzi wa silaha kutoka baadhi ya nchi, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, kwa sababu ya rekodi yake mbaya ya haki za binadamu.
Kwa muda mrefu wanajeshi wa Nigeria wanaokabiliana na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram kaskazini mwa taifa hilo wamekuwa wakidai kuwa wapiganaji hao wamejihami kuwazidi wanajeshi.
Aidha kumekuwa na visa kadha vya wanajeshi kutoroka kazi na kukaidi amri kwa sababu hawakuwa wamejihami ipasavyo wakilinganishwa na kundi hilo.

lori laua huko mbeya


WATU WANNE WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.200 AKQ AINA YA ISUZU LORI IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KISHA KUIGONGA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.614 BUK AINA YA T-BETTER ILIYOKUWA PEMBENI YA BARABARA NA KISHA KUPINDUKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 22.09.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO MLIMA NYIMBILI, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, BARABARA YA KAMSAMBA/MLOWO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI 1. SELA MKISI (30) MKAZI WA NTUNGWA 2. ENEA MGALA (42) MKAZI WA NKANGA 3. LUSIANO MTENDA (50) MKAZI WA MKOMBA NA 4. ELITA MASHAKA (02) MKAZI WA NTUNGWA.
AIDHA WATU KADHAA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI VWAWA KWA MATIBABU. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOPSPITALI YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA

ABNU QATADA AACHIWA HURU

Mshirikishe mwenzako
Abnu Qatada alikabiliwa na tuhuma za kupanga njama ya mashambulizi ya kigaidi nchini Jordan

Mhubiri muislamu mwenye utata ambaye alihamishwa kutoka Uingereza mwaka 2013, Abu Qatada, ameachiliwa huru nchini Jordan baada ya mahakama kutompata na hatia.
Alikuwa ametuhumiwa na kosa la kuhusika katika njama ya kupanga mashambulizi ya kigaidi ambayo ilitibuliwa mwaka 2000.
Jopo la majaji waliokuwa katika mahakama hiyo, hawakumpata na hatia yoyote bwana Qatada kutokana na madai kuwa alihusika na njama hiyo ya ugaidi.
Uamuzi huo umetolewa baada ya Abu Qatada kutopatikana na hatia mwezi Juni katika kosa lengine la kupanga njama ya mashambulizi mwaka 1998 nchini Jordan.
Abu Qatada alitimuliwa kutoka Uingereza mwezi Julai mwaka 2013 kwa madai ya kueneza itikadi kali Uingereza ikitaka afunguliwe mashitaka nchini Jordan.