Jumatatu, 29 Desemba 2014

ATOMIA KRENI KUPOSA LAKINI MAMBO YAKAENGA MRAMA

'Kreni' ilitumbukia ndani ya nyumba wakati ikimbeba mwanamume aliyekuwa anamposa mpenzi wake
Mwanamume mmoja raia wa udachi amejikuta akikimbilia usalama wake baada ya jaribio la kutaka kumposa mpenzi wake kwa mbwembwe kwenda mrama.
Mtu huyo ambaye hakutajwa kwa jina anayeishi mjini Ijsselstein alikodisha 'kreni' au Crane na kuipanda akipanga kwamba kreni hilo imtoe chini na kumpandisha hadi dirishani mwa mpenzi wake ambapo angemchezea wimbo na kisha kumposa.
Badala yake yaliyomkuta hakuyatarajia kabisa.Kreni hiyo ilianguka chini na kupita dirishani kwa mpenzi wake huku ikiangukia nyumba za majirani.
Mwanamume huyo alilazimika kukimbilia usalama wake na hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililowaacha wengi wakiangua kicheko.
Kwa mujibu wa jarida la Algemeen Dagblad, mpenzi wake mwanamume huyo alimkubali na kusema yuko radhi kuolewa naye licha ya tukio hilo.
Baada ya kuongea na polisi, wawili hao walisafiri kwenda mjini Paris Ufaransa kusherehekea.
Kreni hio ilianguka tena kwa mara ya pili ilipokuwa inainuliwa na hata kuharibu zaidi nyumba za majirani. Meya wa mji huo, amezomewa na wengi baada ya eneo hilo kusemekana kutokuwa salama.(TK)

BMW YAZINDUA GARI LINALOJIEGESHA KWA SAA

Kampuni ya BMW imezindua kifaa ambacho kinawezesha gari lako kujiegesha lenyewe
Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye gorofa nyingi.
Lakini hivi karibuni hutahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindua kifuaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hiyo kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa hicho.
Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.
Gari hili linaweza kujiegesha lenyewe kwa kutumia saa ya mkononi ambayo inabonyezwa na dereva
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hiyo ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.
Gari hilo linatumia miale ya Leser inayoweza kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.
Dereva anaporejea kutoka alikokwenda, analiamrisha gari kutoka sehemu ilikojiegesha na kuja kumchukua dereva
Teknolojia hio inajulikana kama ' Remote Valet Parking Assistant,' na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.
Badala ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.
Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema.
Kwa mujibu wa waliotengeneza gari hilo, gari hilo linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.
Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mengine. (TUKUO)

MVUA YALETA KIZAAZAA DAR

Daladala ikiwa imeanguka katika maji



CHENI ZINAONDOKA NA MAJI

VILIO VYATANDA KUPOTEA KWA NDEGE YA AIR ASIA



 Rubani wa Ndege Iliyopotea Ya Air Asia

 Ndugu wa Abiria wakilia kwa uchungu
 Ni vilio na Majonzi

AJALI YA LORI YAKATA MAWAS9L9ANO KATI YA TRINGA NA MIKOA YA KUSINI

Sehemu ya msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Sehemu ya Lori lililopata ajali
Wafanyakazi wa Lori hilo wakitafakari nini cha kufanya

Edwin Moshi wa Eddy Blog
Watumiaji wa barabara ya Iringa Mbeya wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261 BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita. 
 Mtandao huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya Njombe Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama kwenye msururu huo.

Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa. 
Baadhi ya abiria na madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia ufinyu wa vifaa vya kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo muda mrefu (karibia siku moja). 

 Hali hiyo iliendelea hadi majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo yakaendelea na safari. 

Jumapili, 28 Desemba 2014

MMILIKI WA NYUMBANI PARK AVAMIWA NYUMBANI KWAKE MJINI MOROGORO NA KUPORWA

Sehemu alizoathirika 
Mkurugenzi mtendaji wa Nyumbani Park & Samaki Sport Farida Mess Matlou alivamiwa na majambazi na kumjeruhi. Tukio hilo lilitokea usiku wa Trh 19 kuamki 20 maeneo ya nyumbani kwake Kihonda.

Kwa taarifa zilizofikia mtandao huu ni kwamba tayari watu wawili wamekatwa kuhusishwa na tukio hiloMkurugenzi huyu alivamiwa usiku wa saa saba 

NDEGE YA KAMPUNI YA AIR ASIA YAPOTEA

Ndege ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.Ndugu, jamaa na marafiki wa abiria waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa na majonzi wakati wakisubiri taarifa kuhusu ndugu zao katika Uwanja wa Ndege wa Surabaya, Indonesia.
Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa. Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.

Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

AJALI MBAYA SINGIDA NI YA BASI LA ZUBERI NA COASTER


Bas la Zuberi No. 3 Limegongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster. Hakuna aliyetoka kwenye costa na imekwisha  nyang'anyang'a. Hali hii imepelekea waliokuwa kwenye magari mengine kushuka na  kuokoa majeruhi. Ni Mbele kidogo ya Singida mjini. 
 Yaani costa imeisha na imeanguka miguu juu. Bado kuna abiria ambao wanahisiwa kuwa wapo chini ya hiyo costa. 

Jumatatu, 22 Desemba 2014

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WA TZ WAISHIO QATAR

unnamedWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio nchini Qatar baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha, Desemba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed2Baadhi ya washiriki wa Mkutano kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Watanzania waishio nchini Qatar  wakimsiliza  Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha Desemba 21,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed3unnamed4Baadhi ya washiriki wa Mkutano kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Watanzania waishio nchini Qatar  wakimsiliza  Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha Desemba 21,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed1Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Qatar, Mzee Said akisoma risala  katika mkutano kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na watanzania waishio Qatar uliofanyika kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha Desemba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed6Baadhi ya Mawaziri na viongozi mbalimbali wa serikali walioongozana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.unnamed7Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio nchini Qatar baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha, Desemba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed8Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakizungumza na Mwinyi Kazimoto ambaye ni Mtanzania anayecheza soka la kulipwa katika timu ya  Al Markhiaya nchini Qatar, katika mkutano kati yake na watanzania waishio nchini humo  uliofanyika kwenye  hoteli ya Sheraton mjini Doha Desemba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed9Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto kwake) akizungumza na baadhi ya washiriki wa   mkutano kati yake na watanzania waishio nchini Qatar uliofanyika kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha, Desemba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BODABODA YAGONGA MTU DAR NA KUKIMBIA


 Watu wawili wamenusurika kifo baada ya dereva wa bodaboda kumgonga mtu mmoja aliyekuwa akivuka katika barabara ya Kawawa Kinondoni na kisha dereva wa boda boda kukimbia kusikojulikana huku abiria wake pamoja na mvuka barabara huyo wakiwa katika hali mbaya.
Tahadhari juu ya uendeshaji salama vyombo vya moto barabarani umeendelea kupigiwa kelele kila uchao haswa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka lakini bado inaonekana kama hadithi za sungura na fisi

JK AKUTANA NA JAKOB ZUMA IKULU DAR LEO

unnamed1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini leo ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)
unnamed2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini leo ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)

MAMA AKUTWA AKILISHA PANYA WAKE

KIFO CHA AISHA MADINDA WALIOKUWA NAYE WASAKWA

Kimenuka! Baada ya kuwepo kwa utata mkubwa juu ya kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya Bongo, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, inadaiwa kwamba waliohusika na kifo chake sasa wanasakwa kila kona.

Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ enzi za uhai wake. 
 
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, zilidai kwamba jeshi hilo ndilo lililozuia mazishi ya staa huyo hadi mwili ufanyiwe uchunguzi.“Ukweli ni kwamba majibu ya kilichomuua hayajawekwa wazi lakini wote waliokuwa naye dakika za mwisho wanasakwa kwani kuna madai mazito kwamba alipewa kitu na watu wasiojulikana

Ijumaa, 12 Desemba 2014

ALBINO BADO WANAISHI KWA MASHAKA TANZANIA

Kampenzi kubwa imezinduliwa nchini Tanzania, ikiongozwa na Raisi Jakaya Kikwete, kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo imekuwa na matukio mengi ya mauaji ya albino kwa imani za kishirikina huku wahusika wakiamini kwamba viungo vya walemavu hao vinaweza kuwapatia utajiri.

Pesa itakayokusanywa kutokana na kampeni hiyo, itatumika katika elimu kwa umma .
Mwandishi wa BBC Salim kikeke anaarifu kutoka mjini Mwanza kaskazini mashariki mwa Tanzania.

LOWASSA ANGURUMA ARUSHA

Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa akihutubia wananchi wa Mto wa Mbu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa eneo la Migombani, Mto wa Mbu jijini Arusha jana

PUNDA WAMPELEKEA KENYATTA UJUMBE MZITO

Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa jiji la Nairobi baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.
 Baadhi ya wananchi walishangaa Punda walikuwa wanafanya nini mjini kumbe wanaharakati ndio waliowaleta huko kuonyesha kuchoshwa kwao na kuzorota kwa usalama nchini humo.
 Kauli mbiu hio ilitumiwa mashambulizi yalipofanywa dhidi ya wakenya mjini Mandera Kaskazini mwa Kenya ambapo wanaharakati walipiga kambi katika ofisi ya Rais wiki kadhaa zilizopita kulalamikia ukosefu wa usalama.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.
Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori hilo alisema kuwa alilipwa na mtu fulani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.
Polisi wamesema wanachunguza kujua nani waliofanya kazi hiyo.
Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema mwanaharakati mmoja huku akiwasukuma Punda hao kutoka kwenye Lori.

Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo hicho.