Jumamosi, 10 Januari 2015

POLISI NCHINI UFARANSA WAWASAKA WASHIRIKA WA MAGAIDI

 
Washukiwa wa shambulizi za Ugaidi Ufaransa
Polisi nchini Ufaransa wamesema kuwa wanawasaka washirika wa mhusika wa shambulizi la kigaidi Amedy Coulibady aliyeuawa katika majibizano ya risasi na polisi katika supermarket jana ijumaa. Hata hivyo polisi wamemtaja Hayat Boumeddiene kuwa miongoni mwa watu hatari katika kundi hilo la magaidi.
Harakati za kuwaokoa mateka katika Jengo hilo la maduka kulifanyika huku ikidaiwa na vyombo vya usalama kuwa kulikuwa na milio ya risasi katika mji mwingine Kaskazini Mashariki mwa Paris.
Eneo la maombolezo Ufaransa
Ndugu wawili Said na Cherif Kouachi walioendesha mashambulizi siku ya jumatano dhidi ya gazeti la Charlie Hebdo waliuawa wakati wakikimbia kutoka katika jingo huku wakijibishana risasi na Polisi.
Mwendesha mashitaka wa Polisi anasema kuwa watu watano wanaotuhumiwa kuhusika katika shambulizi hilo wanashikiliwa na Polisi.
Watu 17 waliuawa katika shambulio hilo,huku idara ya usalama ikibaini kuwa kulikuwa na mawasiliano ya simu mara 500 mwaka jana, ambapo makundi tofauti ya magaidi hao walikuwa wakipanga njama zao

DR MAGUFULI AHUDHURIA MAIISHI YA FIDEL CASTRO RAILA ODINGA

Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mfiwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mh. Raila Odinga wakiongozana kuelekea sehemu maalum ya kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabla ya kuzikwa kwake.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabla ya kuzikwa kwake. Kushoto ni Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu akimuombea mwanae.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli yupo nchini Kenya akiiwakilisha Tanzania kwenye mazishi ya mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga aitwaye Fidel Odinga aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita. Mazishi hayo yanafanyika huko Bondo, Kisumu, Kenya leo. (TK)

Ijumaa, 9 Januari 2015

DAFTARI LA WAHALIFU KUANZISHWA DAR KUDHIIBITI PANYA ROAD




KUIBUKA kwa makundi ya vijana ya uhalifu Dar es Salaam, kumesababisha uongozi wa mkoa kuanzisha daftari maalumu la kudumu la taarifa za wahalifu wote wa jiji hilo, ikiwa ni harakati za kumaliza tatizo hilo. 
Daftari hilo ambalo litakuwa na kazi ya kutunza orodha ya wahalifu wote kuanzia ngazi za mitaa, litasaidia kuwapata wahalifu kiurahisi watakapofanya matukio katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua mpango wa kunusuru kaya masikini wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Awamu ya Tatu.
Akifafanua kuhusu kurahisisha kuwapata wahalifu, kutokana na taarifa katika daftari hilo, Sadiki alisema wahalifu watakaorodheshwa katika daftari hilo, kutakuwa na taarifa zao kamili na makosa wanayotuhumiwa nayo, hivyo watakapofanya makosa itajulikana ni akina nani.


“Tunaanzisha benki ya wahalifu ambapo ndani ya daftari hilo kutakuwa na orodha yote ya wahalifu kwa maana hiyo kama mtu kafanya uhalifu eneo fulani, itafuatiliwa kwenye daftari na kujua ni wahalifu gani watakusanya na watakaokuwa hawana hatia wataachiwa,” alisema Sadiki.

Alisema katika hilo, hakutakuwa na uonevu wa aina yoyote kwa mtu yeyote, bali watafanya hivyo kwa kufuata haki na sheria. Aidha, alisema madaftari hayo yatakuwepo kuanzia ngazi ya chini ya mitaa hadi ofisi ya mkuu wa mkoa.
“Hapa leo tumezindua mpango mzuri sana, lakini hata tuwe na mipango ya maendeleo mazuri kiasi gani bila kuwa na amani ni sawa na bure, nawaomba chokochoko zozote zinazoweza kuvunja amani tusizifumbie macho,” alisema.

Aliwataka madiwani waliohudhuria mkutano huo, kuhakikisha wananchi wao wanaishi kwa usalama na amani kwa kusaidia kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, ikiwemo kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa katika kudhibiti makundi ya uhalifu.
“Kuna makundi ya vijana wahuni kama hawa wanaojiita panya road, mbwa mwitu na mengine ya aina hiyo hawa ni wahalifu, tushirikiane kudhibiti makundi haya kwa kutoa taarifa hata kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na ofisi nyingine za serikali,” alisema.

Aidha, Sadiki alionya tabia iliyozuka ya vyama vya siasa kukataa matokeo ya uchaguzi kwa kufanya vurugu. Alisema kufanya hivyo hakuimarishi demokrasia, bali ni kuizorotesha na kuiua.
“Jana tulishuhudia vurugu zilizotokea wakati wenyeviti wa mtaa wa Manispaa ya Kinondoni wakiapishwa, kundi la watu liliibuka na kufanya vurugu, lilijeruhi watu eti wanadai wanapinga wale wanaoapishwa, jamani mbona sheria iko wazi na bahati nzuri kuna watu wanashikiliwa kutokana na tukio hilo,” alisema.

Alisema kama watu hao hawakuridhika, walipaswa kufuata taratibu, ikiwemo kwenda mahakamani, lakini demokrasia ya makonde haikubaliki. Alisema amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuwachukulia hatua waliofanya tukio hilo bila kujali vyeo au vyama vyao.

WAUAJI WAUAWA NCHINI UFARANSA

Polisi wakiwafuatilia wanaume wawili waliokuwa wamejihami na waliowaua wandishi wa habari wa jarida la vibonzo la Charlie Heblo
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kwamba washukiwa wawili waliohusika na mauaji ya Charlie Hebdo wameuawa.
Wawili hao walisakwa kwa siku mbili na polisi baada ya kutoroka baada ya kuwaua wandishi habari wa jarida la Charlie Heblo.
Maafisa wa usalama walivamia eneo ambako vijana hao walikuwa wamejificha wakiwa na mateka mmoja na kuwaua vijana hao ambao walikuwa ndugu.
Milio ya risasi ilisikika huku moshi mkubwa ukionekana kufuka kutoka katika jengo hilo huku makomando wakionekana wakivamia jengo hilo.
Duru zinasema washukiwa hao walikuwa wamejihami walifyatulia risasi makomando hao kabla ya kuuawa.
Walisema waliwaua wandishi wa habari kama hatia ya kulipiza kisasi hatua ya wahariri wa jarida hilo kuchora vibonzo kumkejeli mtume Mohammed wa dini ya kiisilamu.
Iliarifiwa kuwa walikipora kituo cha mafuta wakiwa mbioni huku wakiwateka mateka na kwenda nao katika kiwanda ambako walikuwa wamejificha.
Mateka mmoja aliweza kuokolewa.
Kwingineko milipuko na milio ya risasi ilisikika ndani ya duka la jumla la kiyahudi, Kaskazini mwa mji huku watu watano waliokuwa wametekwa nyara na mshambuliaji mmoja wakiuawa.
Baada ya operesheni ya polisi kukamilika baadhi ya mateka waliokuwa wamezuiliwa ndani ya duka hilo walionekena wakitoka nje

POLISI WAKAMATA MABASI YENYE PICHA YA RAIS

Gari la kubeba abiria lililochorwa picha ya rais Uhuru Kenyatta
Licha ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuruhusu magari yanayobeba abiria nchini Kenya kuchorwa ama hata kupaka rangi yoyote ile, mabasi mawili yaliochorwa picha yake yamekamatwa na maafisa wa polisi mjini Mombasa Kenya.
Maafisa wa trafiki mjini Mombasa waliyakagua magari hayo na kuyakamata magari yote yaliokuwa yamechorwa picha pamoja na magari yenye madirisha yasioonyesha ndani.
Magari sita yakiwemo mawili yaliokuwa na picha ya Uhuru yalikamatwa, licha ya agizo la rais kuruhusu wamiliki wa matatu kuchora picha katika magari.
Uhuru alikuwa amesema kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana kutumia vipaji vyao ili kuweza kujinufaisha kimaisha.
Uchoraji katika magari hayo na muziki ulipigwa marufuku mnamo mwaka 2003 na aliyekuwa waziri wa uchukuzi John Michuki.

WACHEZAJI WA AFRICAN LYON WAPIGWA NA MASHABIKI WA LIPULI

3Mchezaji wa Africa Lyon, Rajab Khamis aliumia mkono kufuatia kupigwa na mashabiki wa Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliopigwa juzi na kumalizika kwa suluhu.

1Raizan Hafidh aliumia nyama za paja baada ya kukatwa mtama na kukanyagwa katika paja na mashabiki wa Lipuli
2Kasim Simbaulanga naye aliumia mkono kutokana na fujo hizo

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALIAMTEMBELE SPIKA ANNE MAKINDA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne

Makinda akimkaribisha ofisini kwake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju wakati alipofanya ziara fupi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akitia saini kwenye kitabu cha wageni wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kubadilishana mawazo. Ziara hiyo fupi imefanyika ofisi ndogo za bunge Dar-es-salaam.Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju akiwa kwenye mazungumzo ya kubadilishana mawazo na Spika wa Bunge Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kwenye ofisi ndogo za bunge Dar-es-salaam.

FIDEL CASTO ODINGA ASAFIRISHWA KWENDA KISUMU









January 4 mwaka 2015 Kenya imeingia kwenye majonzi baada ya kumpoteza mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, Fidel Casto Odinga ambaye alifariki nyumbani kwake ghafla baada ya kurudi kutoka matembezi na kufikia kumpumzika na hadi umauti ulipomkuta. 
 
Leo mwili wa marehemu Fidel Odinga umesafirishwa na Ndege ya jeshi la Kenya Kenya Air Force hadi katika mji wa Kisumu ambapo msafara wake utaanzia hapo hadi kwenye kijiji cha Opoda kilichopo Kisumu Kenya tayari kwa mazishi yatakayofanyika siku ya kesho Jumamosi tarehe 8 January 2015

MWANAYE JACKIE CHANG JELA KWA BANGI

Jackie chan na mwanawe Jacee Chan
Jacee Chan mwana wa mwana nyota wa filamu Jackie Chan amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kutumia mihadarati.
Jacee Chan mwenye umri wa miaka 32 alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya wiliaya ya mjini Beijing Dongcheng kwa kuwaficha wengine ili kutumia dawa za kulevya.
Polisi walivamia nyumba yake mnamo mwezi Agosti na kupata gramu 100 za bangi (marijuana).

Kukamatwa kwake kunajiri kufuatia msako wa dawa za kulevya nchini Uchina ambapo watu kadhaa mashuhuri walikamatwa.Jacee Chan na babaake Jackie Chan

Mnamo mwezi Juni mwaka 2014, rais Xi Jinping aliwaagiza polisi kutumia mikakati mikali ili kusitisha utumizi wa mihadarati.

Kukiri kwa mwana wa mcheza filamu mashuhuri nchini Uchina kunatoa ujumbe muhimu kutoka kwa serikali ya Uchina.

Hakuna aliye na kinga nchini Uchina katika msako huo wa dawa za kulevya.

Chan na nyota wa filamu kutoka Taiwan Kai Ko mwenye umri wa miaka 23 walikamatwa pamoja katika nyumba ya Beijing mnamo mwezi Agosti huku polisi wakisema kuwa walipatikana wametumia bangi.

YAYA TOURE AWEKA REKODI YA UANASOKA BORA AFRIKA MARA YA NNE MFULULIZO

yaya-toure

Bertha Lumala na mitandao
Kiungo wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika wa Shirikisho l;a Soka barani Afrika (CAF) kwa mwaka wa nne mfululizo.
Kiungo huyo ametwaa tena taji huilo baada ya kumbwaga  Mnigeria Vincent Enyeama, ambaye alionekana kuwa tishio kwake mwaka huu.
Hata hivyo, taifa lililong’ara zaidi usiku huu wakati wa kutunuku tuzo hizo, ni la Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika, Algeria.
Timu ya Taifa hilo imetangazwa kuwa Timu Bora ya Mwaka, Klabu ya ES Setif Algeria imetangazwa kuwa Klabu Bora ya Mwaka na kocha swao mkuu, Kheireddine Madoui ametawazwa Kocha Bora wa Mwaka.

Katika kung’arisha zaidi tuzo hizo, Kinda wa Algeria, Yacine Brahimi ametangazwa kuwa ndiye Kinda Mwenye Kipaji Zaidi wa Mwaka Anayechipikia.
Wanawake wa Nigeria nao hawakuachwa nyuma wakati Falcons hao wakitangazwa Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka na Asisat Oshoala akaongeza tuzo nyingine kwa kuibuka Mchezaji Bora Kinda wa Mwaka na Mwanasoka Borav wa Kike wa Mwaka barani.
Tuzo ya Refa Bora wa Mwaka imekwenda kwa Papa Bakary Gassama, wakati Tuzo Mwanasoka Bora wa Mwaka anayecheza ndani ya Afrika imekwenda kwa Firmin Ndombe Makala