Jumanne, 4 Julai 2017

Rugemalira na Sethi wa IPTL waongezewa mashitaka 6




WAFANYABIASHARA wawili, Harbinder Sethi na James Rugemalira wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya pili na kusomewa mashitaka mapya sita likiwamo la utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Dola za Kimarekani milioni 22.1 na Sh bilioni 309.4.
Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL) na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Power African Power (T) Limited (PAP), walisomewa mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi, yakifanya sasa wakabiliwe na mashitaka 12 baada ya awali kupandishwa kizimbani Juni 19, mwaka huu, ambako walikabiliwa na mashitaka sita.
Akiwasomea mashitaka hayo, Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia serikali hasara na kutakatisha fedha. Kimaro alidai kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jijini Dar es Salaam, walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.
Alidai katika mashitaka ya pili kati ya Oktoba 8, 2011 na Machi 19,2014 jijini Dar es Salaam, wakiwa siyo watumishi wa umma walishirikiana na watumishi wa umma kutekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.
Katika mashitaka ya tatu yanayomkabili Sethi, inadaiwa kuwa Oktoba 10, 2011 katika Mtaa wa Ohio Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai, alighushi fomu namba 14 A ya usajili wa kampuni na kuonesha kuwa yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau, Masaki wakati akijua sio kweli.
Pia Sethi anadaiwa alitoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14 A ya usajili wa kampuni kwa Ofisa Msajili wa Kampuni, Seka Kasera kwa njia ya kuonesha kwamba yeye ni Mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau, Masaki Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aidha, Kimaro alidai katika mashitaka ya kujipatia fedha kwamba kati ya Novemba 28 na 29, 2011 na Januari 23,2014 katika Makao Makuu ya Benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi, Tawi la Mtakatifu Joseph, kwa ulaghai washitakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dola za Marekani 22,198,544.60 na Shilingi za Tanzania 309, 461,300,158.27.
Pia washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic, Tawi la Kinondoni, kwa vitendo vyao waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Kimaro alidai kati ya Novemba 29,2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam, kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT ambazo ni dola za Marekani milioni 22.1 na Sh bilioni 309.4 wakati wakijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Katika mashitaka ya nane, Kimaro alidai kuwa Novemba 29, 2013 katika Tawi la Benki ya Stanbic Tanzania, Wilaya ya Kinondoni, Sethi alitakatisha fedha kwa kuchukua kutoka BOT dola za Marekani milioni 22.1 wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Aidha, Sethi anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14,2014 katika Tawi la Benki ya Stanbic Kinondoni, Dar es Salaam alitakatisha fedha Sh bilioni 309.4 kutoka Benki Kuu ya Tanzania wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao uhalifu.
Katika mashitaka ya 10, inadaiwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi, Tawi la St Joseph Cathedral, Rugemalira alitakatisha fedha ambazo ni Sh bilioni 73.5 kutoka kwa Sethi wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.
Pia inadaiwa Januari 23, 2014 katika tawi hilo la Benki ya Mkombozi, Rugemalira alitakatisha fedha ambazo ni dola za Marekani milioni 22 kutoka kwa Sethi wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
Kimaro pia alidai Sethi anadaiwa kuwa Januari 28, 2014 katika Tawi la Benki ya Stanbic, Kinondoni alihamisha Rand za Afrika Kusini 1,305,800 kwenda kwenye akaunti namba 022655123 katika Benki ya Standard Land Rover Sandton ya Afrika Kusini wakati akijua katika kipindi anahamisha fedha hizo zimetokana na zao la kujihusha na genge la uhalifu.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Hata hivyo, upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na washitakiwa wamerudishwa rumande hadi Julai 14, mwaka huu kwa kuwa mashitaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana.

Jumatatu, 3 Julai 2017

Kangaroo afariki katika kiti akiwa na mvinyo Australia

Kangaroo apigwa risasi na kufariki akiwa ameketi katika kiti na mvinyo mkononi

 Kangaroo apigwa risasi na kufariki akiwa ameketi katika kiti na mvinyo mkononi
Maafisa wa polisi wanachunguza baada ya kangaroo kupatikana amepigwa risasi huku akishikilia mvinyo wa pombe mjini Melbourne Australia.
Maafisa wa wanyama pori nchini Australia wanasema mnyama huyo aliigwa risasi mara tatu na baadaye kufungwa akiwa ameketi katika kiti.
Iliripotiwa mwezi uliopita lakini mamlaka ilitoa picha wiki hii katika harakati za kutafuta habari.
Hukumu ya mauaji ya myama huyo kinyume cha sheria ni faini ya hadi dola 36,500 za Australia na hadi kifungo cha miaka miwili jela.
Idara ya mazingira, ardhi, maji na mipango ilisema kuwa inashirikiana na maafisa wa polisi kutatua uhalifu huo.
Lazima ilichukua muda mrefu kumuweka kangaroo huyo katika hali aliyokuwa kanda kando ya barabara.
Hesabu ya hivi karibuni ya kangaroo nchini Australia ni milioni 34.3

Mwanamume akatwa kidole kwa kung'atwa harusini Australia

Police speak with witnesses after the violent altercation

 Polisi wakiongea na watu nje ya tukio
Mwanamume mmoja amekamatwa kwa madai kuwa alimng'ata na kukata kidole cha mtu mwingine wakati was sherehe ya harusi mjini Sydney Australia.
Mvamizi huyo mwenye umri wa miaka 42 aliingia katika sherehe moja ya harusi siku ya Jumamosi usiku na kujaribu kuiba mkoba.
Wakati wageni walipomkabili, mvutano ukatokea ambapo mwanamume huyo alingata kidole cha mtu mwingine.
Kidole kilichong'atwa hakiwezi kuokolea, kwa mujibu wa vyomo vya habari.
Mwanamume aliyeumia alipelekwa hospitalini ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.
Hizo hazikuwa ghasia za mwisho usiku huo kwani polisi walilazimika kuvunja mapigano yaliyotokea nje ya klabu

Ijumaa, 23 Juni 2017

Idadi ya watu duniani kufika bilioni 10 mwaka 2050

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inakadiria idadi ya watu India itaipiku ya China katika kipindi cha miaka saba ijayo na Nigeria inatarajiwa kuipiku Marekani na kuwa taifa la tatu duniani lenye idadi kubwa ya watu ifikapo 2050
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya uchumi na masuala ya kijamii ya shirika la  kushughulikia idadi ya watu duniani katika Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa idadi ya hivi sasa ya watu duniani ya takriban bilioni 7.6 itaongezeka hadi watu bilioni 8.6 ifikapo mwaka 2030, bilioni 9.8 ifikapo 2050 na bilioni 11.2 ifikapo mwaka 2100.
Inaripotiwa kuwa karibu watu miliioni 83 wanazaliwa duniani kila mwaka, dalili zinaoonyesha ongezeko litakaloendelea hata kama viwango vya uzazi vitashuka kama inavyoshuhudiwa tangu miaka ya 1960.

Jumatano, 21 Juni 2017

Shambulio la bomu Brussels: mtuhumiwa auawa

Polisi katika eneo la tukio

Polisi katika eneo la tukio
Wanajeshi wa Ubelgiji wamemuua kwa kumpiga risasi mlipuaji wa bomu wa kujitoa muhanga, katika kituo kikuu cha reli mjini Brussels.
Idara ya polisi imesema kuwa mtu huyo alikuwa amevalia kile kilichoonekana kuwa mkanda wa vilipuzi na kuwa kulitokea mlipuko mdogo.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa mshukiwa huyo amefariki.
Watu waliokuwa katika kituo Kikuu cha mabasi mjini Brussels na eneo la karibu la mnara ambalo hufurika watalii wote waliondolewa.
Wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mjini Brussels tangu kulipotokea shambulio la kujitoa mhanga katika eneo la Uwanja wa ndege na kwenye mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi mwaka uliopita .

Jumanne, 20 Juni 2017

Je uko tayari kuambukizwa ugonjwa kwa malipo ya pauni 3,526?

Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.

Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.
Je ni pesa ngapi zinaweza kukushawishi kukubali kuambukizwa kikohozi ili kusaidia uvumbuzi wa kisayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.
Wanataka kutengeneza chanjo bora ili kuwalinda watoto, na watu wazima ambao wapo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo.
Ili kusaidia ni sharti uwe na umri wa kati ya miaka 18-45, uwe na afya bora, uwe tayari kutengwa kwa siku 17 na kuimba.
Kikohozi ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa haraka na huenezwa kupitia hewa ya kikohozi kutoka kwa mtu ambaye ameambukizwa .
Kundi hilo kutoka mjini Southampton linataka kuwaambukiza watu walio na afya nzuri kwa kuwawekea puani viini vinavyosababisha maambukizi hayo na kuwachunguza.
Baadhi ya watu waliojitolea watakuwa wagonjwa, lakini wanasayansi wanataka wale ambao hawatakuwa na dalili zozote licha ya kuwekewa viini hivyo katika pua zao.
Kile wanachotafuta ni wale wanaobeba viini hivyo kwa siri na watu ambao wanakinga ya ugonjwa huo.
Wale wanaobeba ugonjwa huo kwa siri huwaambukiza watu wengine lakini huwa hawapatwi na ugonjwa huo.
Huonekana kuwa na kinga ya kutosha ya kukabiliana na ugonjwa huo licha ya kwamba hawajapewa chanjo.

AFUNGISHWA NDOA NA MAREHEMU NCHINI MSUMBIJI

Dola za Marekani

Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikendi iliopita kulingana na chombo cha habari cha taifa.
Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua, nduguze walimlazimisha mpenziwe kulipa ''Lobolo'', wakionya kwamba la sivyo hatozikwa.
Nduguze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu marehemu mkewe, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 (sawa na shilingi za Kitanzania1,760,000) na kufanya haruasi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Nduguye kijana huyo Irmao do Jovem alielezea matatizo yao.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 (sawa na shilingi za Kitanzania 387,200) tu. Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi''.
Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali kulipa, walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.
Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Msumbiji hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
Hili ni funzo kwa vijana wengi ambao wanapenda kuishi na wanawake bila kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamke husika na kufunga nao ndoa.

Jumatano, 31 Mei 2017

Watafiti: Uendeshaji baiskeli za abiria hatarini kutozaa

Mhudumu wa bodaboda Bwaise, Kampala nchini Uganda mwaka 2008
Kijana akisubiri abiria kwa kutumia baiskeli katika biashara ya uchukuzi wa abiria.


Watafiti nchini Kenya wanasema kunaweza kuwa na changamoto nyingine - kwamba wahudumu wa kubeba abiria kwa baiskeli maarufu kama bodaboda nchini Kenya wanakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wao wa uzazi.
Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba waendeshaji boda boda walikuwa katika hatari ya kutoweza kutanua mishipa ya damu kwenye uume wakati wa kushiriki tendo la ngono.
Mmoja wa watafiti hao Isaac Wamalwa ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta aliambia BBC kwamba suluhu huenda likawa ni kutumiwa kwa kiti maalum ya waendesha baiskeli ambayo hakitadhuru uume wa waendeshaji.
Bw Wamalwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi alifanya utafiti miongoni mwa vijana eneo la Bungoma, magharibi mwa Kenya.
Walichunguza wahudumu 115 wa boda boda wa umri wa chini ya miaka 40 eneo hilo, wakishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.
"Tuliwachunguza vijana waendeshaji wa bodaboda Bungoma na matokeo yalikuwa ya kushangaza. Kwa jumla, tuligundua kwamba zaidi ya theluthi moja ya waendeshaji bodaboda, asilimia 35.9, ya washiriki walikuwa na matatizo ya kuweza kusimika," aliambia gazeti la Standard la Kenya.
Anasema tatizo lilitokana na kuendesha baiskeli hizo kwa muda mrefu.
Bw Wamalwa anasema wote walioendesha baiskeli kwa zaidi ya saa 60 kwa wiki, walikuwa na matatizo ya kiafya.
Anatahadharisha pia kwamba maelfu ya vijana wanaofanya mazoezi kwenye vituo vya mazoezi mijini, kwa Kiingereza gym, ambapo huendesha baiskeli zisizo na gia, wanakabiliwa na hatari sawa na hiyo.
"Ujumbe wetu ni muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao. Anasema wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao kitandani.
Wataalamu wengine sita kutoka Chuo Kikuu cha Moi walifanya utafiti mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya, na kupata matokeo yanayokaribiana na ya Bw Wamalwa.
Waliwachunguza wahudumu wa dbodaboda 131 wa umri wa kati ya miaka 18 na 65, umri wa kadiri ukiwa miaka 40.
Waligundua kwamba asilimia 76 kati yao walikuwa na matatizo kitandani.
Watafiti hao pia walidokeza kwamba tatizo hilo huenda linatokana na kuendesha baiskeli kwa muda mrefu.

Alhamisi, 25 Mei 2017

Wakongwe waliozoea kufanya kazi duniani hawa hapa





Prince Philip
  Mwanamfalme Philip anasema atajiuzulu baadaye mwaka huu

Wakati Mwanamfalme Philip, anafikisha miaka 96 mwezi Juni anastaafu majukumu yake ya kifalme baadaye mwaka huu, tunawaangazia baadhi ya watu wanaofurahia kazi zao kiasi cha kuamua kuendelea kufanya kazi - wengi wao hata kumpita Kiongozi huyo wa Edinburgh.
David Goodall, Mwansayansi mkongwe Australia
Mkongwe huyo wa miaka 103 mwaka jana alishinda kesi kuendelea kufanya kazi katika chuo kikuu kilichoko magharibi mwa Australia cha Edith Cowan huko Perth.
Dr Goodall aliagizwa kufanya kazi akiwa nyumbani 2017 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wake, lakini chuo hicho baadaye kilisema, nafasi nzuri imepatikana katika tawi la chuo hicho lililoko karibu na makaazi ya mwanasayansi huyo.

Jumanne, 23 Mei 2017

MASHOGA WAPO? Wanaume waliofumaniwa wakifanya mapenzi Indonesia wamechapwa viboko 85 kila mmoja

 Wanaume waliofanya mapenzi wachapwa vikobo 85 Indonesia
Wanaume waliofanya mapenzi ya jinsia moja wakichapwa vikobo 85 Indonesia
Wanaume wawili wamechapwa viboko 85 kila mmoja kwenye mkoa wa Ace nchini Indonesia baada ya kufumaniwa wakifanya mapenzi.
Wanaume hao walisimama kwenye jukwaa wakiwa na mavazi meupe wakiomba, huku kundi la wanaume likiwachapa vikobo kwenye migongo yao
Indonesia imeharamisha mapenzi ya Jinsia moja na Mkoa wa Acheh hutawaliwa na sheria ya kidini- Sharia.
Adhabu hiyo ilitolewa mbele ya umma.